Pre GE2025 Luhaga Mpina: Nchi sita za Afrika zilizopindua Serikali zao zilikuwa sahihi

Pre GE2025 Luhaga Mpina: Nchi sita za Afrika zilizopindua Serikali zao zilikuwa sahihi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Salaam, Shalom!!

Akiongea kupitia press aliyoitisha nje ya Bunge amedai kuwa UMOJA wa Afrika haupasi kuzisimamisha uanachama Nchi SITA zilizopindua Serikali zao Kwa sababu Watawala waliopinduliwa hawakujali sauti na matakwa ya wananchi.

Amedai kuwa RUSHWA ikitamalaki, ukiukwaji wa HAKI za binadamu ukiota mizizi, Wizi wa kura ukitamalaki, wizi wa Raslimali za umma ukitamalaki, dhuluma ikizidi katika JAMII, hakuna njia ingine wananchi wanaweza kufanya zaidi ya kupindua Serikali zao Kwa njia mbalimbali.

Ndugu Mpina ameitaka Serikali ya Rais Samia Kutoa tamko kushauri Nchi hizo zisizuiliwe uanachama katika ushirika wa AU.

Chanzo: Uhondo Tv.

Mungu ambariki na kumlinda ndugu Mpina,

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿

HAKI ikatawale katika Taifa. Amen

Karibuni 🙏
Kila zama Na watu wake....magufuri alikupa ulaji Mpina, Leo magufuri hayupo....inatakiwa nyote mliobebwa Na magufuri kuwa magufuri hayupo tena
 
Sababu kuu za mapinduzi ni RUSHWA kutamalaki, wizi wa kura na WA raslimali za nchi.

Kwani imeshindikana CCM kujitenga na wizi wa kura Ili tusiende huko kama Nchi?
Baada ya kupindua Rushwa zikaisha au? Sudan huko kinachowagombanisha ni nini?

Kwa taarifa Yako sababu za mapinduzi ni uroho wa madaraka na Ufisadi hakuna Kingine,hivyo vingine Huwa ni vijisababi vya kutafuta kuhalalisha mapinduzi
 
Wanaodai Katiba Mpya ndio hao hao wanatumia Rushwa na ngumu kuchaguana ,mpaka hapo hao wanataka madaraka ya Umma Kwa malengo binafsi.

Mwisho Katiba Mpya haijawahi leta ugali walakutatua shida za watu ila ni njia ya Wanasiasa walioko Nje ya serikali kuingia humo wapate ulaji
Yani wewe akili yako imeishia hapo?. Yani uchaguzi wa CHADEMA umekuuma kiasi kwamba unatunga uongo kujustyfy kutokuwepo na Katiba Mpya?. Be serious.
 
Yani wewe akili yako imeishia hapo?. Yani uchaguzi wa CHADEMA umekuuma kiasi kwamba unatunga uongo kujustyfy kutokuwepo na Katiba Mpya?. Be serious.
Ndio umeniuma sana Kwa sababu waliotarajiwa kuonesha utofauti wameishiwa kupigwa bei kama matikiti.

Mpaka hapo Kuna haja gani ya kuwa na Vyama Vya waganga njaa? 🤣🤣
 
Kama haikusaidii Kaa pembeni endelea kulima matembele hapo Misungwi, wale ambao itawasaidia acha waendelee na harakati.
Niko.hapa kuelimisha Umma kwamba Utapeli ule ule wa kupinga Rushwa ndio wametumia Rushwa kuchaguana.

So Utapeli wa Katiba Mpya eti itasaidia ndio huo huo mnataka kudanganya wajinga Ili mkapate madaraka muendelezo wizi 😁😁
 
Ndio umeniuma sana Kwa sababu waliotarajiwa kuonesha utofauti wameishiwa kupigwa bei kama matikiti.

Mpaka hapo Kuna haja gani ya kuwa na Vyama Vya waganga njaa? 🤣🤣
Tuseme ni kweli rushwa ilitokewa kwenye huo uchaguzi, je unahalalisha mchakato wa Katiba Mpya usiwepo?. Kosa la CHADEMA ndilo lifanye Katiba Mpya isiwepo.
 
Back
Top Bottom