Luhaga Mpina: Waziri Mwigulu Nchemba anahusika na ufisadi wa trilioni 1.7 mradi wa SGR

Luhaga Mpina: Waziri Mwigulu Nchemba anahusika na ufisadi wa trilioni 1.7 mradi wa SGR

Waziri wa zamani wa uvuvi Luhaga Mpina ametoa tuhuma kwa Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba kuwa ameiibia Serikali pesa katika miradi wa SGR zaidi ya trilioni1.7 .

Hii ni zaidi ya ile kelele ya trilioni 1.5 ya utawala wa hayati Magufuli na ni nusu ya wizi wote alioutaja CAG katika report yake ya jumla ya trilioni 3.5 kwa wizara yote.

Kumbe yale mabasi na matimu ya mpira ni pesa za walipa kodi

USSR

View attachment 2595078
Mpigaji balaa. Halafu analeta mabasi waziwazi kujifanya hajaiba kitu. Mama timua huyo.
 
Pamoja na haya, ajabu Rais akaishia kuvunja bodi tu ya shirika la Reli, wakati inaonekana kuna uozo mkubwa zaidi unafichwa..

Mwigulu anastahili kufikishwa mahakamani kwa hizi tuhuma kama zikithibitishwa, licha ya kuhusishwa kwake na huu wizi kunakoendana nae kuonekana kuwa na mali nyingi zaidi ya kipato chake, bado yupo ofisini miguu juu akibuni tozo mpya kwa ajili yetu.

Kiongozi kama huyu ingefaa kabisa awekwe pembeni kupisha uchunguzi dhidi yake, bahati yake ni miongoni mwa watoto pendwa wa mama, awamu hii imekuwa incompetent sana.
Bado wapo wanaoisifia mkuu awamu ya sita,lakini ni kweli,awamu hii ni very incompetent.Lakini tangu lini watu wa pwani wakawa serious,wanejaa uswahili Swahili tu.
 
Mwigulu ni mzalendo Mwigulu sio Tajiri na hana ujanja wa kuiba 1.7 Trilion hiyo akili Hana kinachomponza Mwigulu ni dharau na upole wake na kupenda kukubalika ndio maana anawaacha watu wajichotee Mihela wamuone ni Mshkaji
 
MPINA: WAZIRI MWIGULU ANAHUSIKA NA UFISADI WA TRILIONI 1.7 MRADI WA SGR

"Kulikuwa na kutokufuata sheria ya manunuzi wakati wa kutoa zabuni ya mradi wa SGR.Kwa mujibu wa ripoti ya CAG ya mwaka 2021/2022 inaonyesha kuwa gharama ya ujenzi wa SGR Lot. Na. 3 na Lot. Na. 4 ziliongezeka kwa dola za Marekani milioni 1.3 na milioni 1.6 kwa kilomita moja ya SGR baada ya TRC kuacha njia ya ushindani na kutumia njia ya Single Source na kusababisha hasara ya jumla ya Tsh. Trilioni 1.7 Licha ya PPRA na bodi ya zabuni ya TRC kukataa sharti la kutumia mzabuni mmoja, lakini TRC ilitoa zabuni hiyo kwa njia ya Single Source kwa kampuni ya Yapi Merkezi.Maamuzi haya yalitokana na
maelekezo ya Wizara ya Fedha na Mipango chini ya Waziri @mwigulunchemba1 kwa barua yenye Kumb: PST/GEN2021/01/55" Mhe.Luhaga Mpina Bungeni
Ni ajabu sana jinsi watu wanavyojifanya hawakumbuki maswala muhimu, hadi hapo yasiyotegemewa yanapoibuka.

Hili swala la "single source" alilizungumzia Rais mwenyewe, wakati huo walipoamua kuachana na utaratibu uliokuwepo.

Sasa hivi kila lawama anatupiwa waziri, kana kwamba ni yeye aliyefanya maamuzi yote!

Na hata baada ya waziri huyo kuelezea rais kuwa na taarifa hizo, bado watu wanang'ang'ana na waziri tu!

Waziri peke yake ataweza vipi kufanya uhujumu wa aina hiyo bila uwepo wa ushiriki wa serikali nzima, akiwemo na rais mwenyewe?
 
Pamoja na haya, ajabu Rais akaishia kuvunja bodi tu ya shirika la Reli, wakati inaonekana kuna uozo mkubwa zaidi unafichwa..

Mwigulu anastahili kufikishwa mahakamani kwa hizi tuhuma kama zikithibitishwa, licha ya kuhusishwa kwake na huu wizi kunakoendana nae kuonekana kuwa na mali nyingi zaidi ya kipato chake, bado yupo ofisini miguu juu akibuni tozo mpya kwa ajili yetu.

Kiongozi kama huyu ingefaa kabisa awekwe pembeni kupisha uchunguzi dhidi yake, bahati yake ni miongoni mwa watoto pendwa wa mama, awamu hii imekuwa incompetent sana.
Inawezekana nawe umesahau lililpoanzia hili jambo la SGR na mabadiliko hayo ya 'Single Source'.

Hili jambo alilizungumzia Samia mwenyewe lilipokuwa likifanyika.

Hapa akina Mpina ni namna tu ya kushindwa kueleza linakotokea tatizo kwa kuogopa uzito wa aliyeruhusu lifanyike, badala yake wanaona ni rahisi waelekeze mashambulizi kwa waziri.

Simtetei Mwigulu kwa jambo lolote, lakini ufafanuzi huu inabidi utolewe ili watu wajue tatizo linaanzia wapi.

Serikali ya Samia, nadhani kwa pamoja walikaa chini na kuamua kutafuta vyanzo vya pesa kwa malengo waliyo nayo wenyewe ndani ya chama chao.
Hizi ni hela zinazokusanywa kwa lengo hilo maalum.

Hayo maigizo anayofanya Samia kwa kuvunja Bodi ya wadhamini, utadhani kuwa hata yeye hakumbuki alichowahi kuzungumzia wakati wakifanya maamuzi hayo.
Na kwa jinsi nchi yetu ilivyo sahaulifu, mbinu zao kila mara hufanikiwa kwa kuvungavunga tu mambo bila ya kuweka ufumbuzi unaoeleweka.

Hizi peas anazodaiwa kuzichota Mwigulu, huo ni mpango maalum ndani ya chama chao wa kukusanya pesa.
Mwigulu, kama Mwigulu hana uwezo wa kukwapua kiasi hicho cha pesa, bila ya mpango kama huo.
 
Waziri wa zamani wa uvuvi Luhaga Mpina ametoa tuhuma kwa Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba kuwa ameiibia Serikali pesa katika miradi wa SGR zaidi ya trilioni1.7 .

Hii ni zaidi ya ile kelele ya trilioni 1.5 ya utawala wa hayati Magufuli na ni nusu ya wizi wote alioutaja CAG katika report yake ya jumla ya trilioni 3.5 kwa wizara yote.

Kumbe yale mabasi na matimu ya mpira ni pesa za walipa kodi

USSR

View attachment 2595078
Uongo na majungu matupu
 
Back
Top Bottom