Luhaga Mpina: Waziri Mwigulu Nchemba anahusika na ufisadi wa trilioni 1.7 mradi wa SGR

Luhaga Mpina: Waziri Mwigulu Nchemba anahusika na ufisadi wa trilioni 1.7 mradi wa SGR

Waziri wa zamani wa uvuvi Luhaga Mpina ametoa tuhuma kwa Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba kuwa ameiibia Serikali pesa katika miradi wa SGR zaidi ya trilioni1.7 .

Hii ni zaidi ya ile kelele ya trilioni 1.5 ya utawala wa hayati Magufuli na ni nusu ya wizi wote alioutaja CAG katika report yake ya jumla ya trilioni 3.5 kwa wizara yote.

Kumbe yale mabasi na matimu ya mpira ni pesa za walipa kodi

USSR

View attachment 2595078
Wasuku.a wana nongwa na watu watatu
January
Nape
Mwigulu
Siku hawa watu wakiondolewa itakuwa sherehe kwao
Hana lolote huyo anaichafua tu serikali na kuna watu wapo nyuma yake dawa ni kukata jina lake 2025
 
Wizi wa Magufuli tunaoujua ni 1.5 trilioni lakini ule wa Magufuli alioshirikiana na Biswalo Mganga ni zaidi ya hapo labda unaweza kufika trilioni 10 na ushee.

CCM ni walewale na mambo ya wizi na upigaji na matumizi mabaya ya fedha za Wananchi masikini ni yale yale.
Tatizo linaanzia hapo. Wanaiba! Wanatajana! Wanasafishana! Uchaguzi ukija wanaibua propaganda utafikiri ccm ni chama kinasajiliwa upya kila uchaguzi!
Wananchi wamepigwa upofu!
Ujinga umetamalaki!!
 
Pamoja na haya, ajabu Rais akaishia kuvunja bodi tu ya shirika la Reli, wakati inaonekana kuna uozo mkubwa zaidi unafichwa..

Mwigulu anastahili kufikishwa mahakamani kwa hizi tuhuma kama zikithibitishwa, licha ya kuhusishwa kwake na huu wizi kunakoendana nae kuonekana kuwa na mali nyingi zaidi ya kipato chake, bado yupo ofisini miguu juu akibuni tozo mpya kwa ajili yetu.

Kiongozi kama huyu ingefaa kabisa awekwe pembeni kupisha uchunguzi dhidi yake, bahati yake ni miongoni mwa watoto pendwa wa mama, awamu hii imekuwa incompetent sana.
Mpina anaongea jumla jumla kwa maana hiyo basi wizara zote madudu yake yabebwe na wazir wa fedha maana ndo mlipaji?
Huyu bwana haongei haya kwa kuwa ni mzalendo sana hapana. Huyu anawakilisha watu fulani hivi
 
Inawezekana nawe umesahau lililpoanzia hili jambo la SGR na mabadiliko hayo ya 'Single Source'.

Hili jambo alilizungumzia Samia mwenyewe lilipokuwa likifanyika.

Hapa akina Mpina ni namna tu ya kushindwa kueleza linakotokea tatizo kwa kuogopa uzito wa aliyeruhusu lifanyike, badala yake wanaona ni rahisi waelekeze mashambulizi kwa waziri.

Simtetei Mwigulu kwa jambo lolote, lakini ufafanuzi huu inabidi utolewe ili watu wajue tatizo linaanzia wapi.

Serikali ya Samia, nadhani kwa pamoja walikaa chini na kuamua kutafuta vyanzo vya pesa kwa malengo waliyo nayo wenyewe ndani ya chama chao.
Hizi ni hela zinazokusanywa kwa lengo hilo maalum.

Hayo maigizo anayofanya Samia kwa kuvunja Bodi ya wadhamini, utadhani kuwa hata yeye hakumbuki alichowahi kuzungumzia wakati wakifanya maamuzi hayo.
Na kwa jinsi nchi yetu ilivyo sahaulifu, mbinu zao kila mara hufanikiwa kwa kuvungavunga tu mambo bila ya kuweka ufumbuzi unaoeleweka.

Hizi peas anazodaiwa kuzichota Mwigulu, huo ni mpango maalum ndani ya chama chao wa kukusanya pesa.
Mwigulu, kama Mwigulu hana uwezo wa kukwapua kiasi hicho cha pesa, bila ya mpango kama huo.
Kweli nilisahau, huu ni mpango wao wa kuchota, ndio maana hata zile za tozo siku hizi hatuambiwi zimekwenda wapi wala zimekusanywa ngapi, tupo chini ya kundi la majambazi.
 
Mahakama zipo.....

Mfungulie kesi ili tujue mbivu na mbichi.....

Kinyume chake ni UZUSHI NA KUCHAFUANA TU.....

#SiempreJMT
 
Waziri wa zamani wa uvuvi Luhaga Mpina ametoa tuhuma kwa Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba kuwa ameiibia Serikali pesa katika miradi wa SGR zaidi ya trilioni1.7 .

Hii ni zaidi ya ile kelele ya trilioni 1.5 ya utawala wa hayati Magufuli na ni nusu ya wizi wote alioutaja CAG katika report yake ya jumla ya trilioni 3.5 kwa wizara yote.

Kumbe yale mabasi na matimu ya mpira ni pesa za walipa kodi

USSR

View attachment 2595078
HV luhaga mpina c ana Akili timamu?tuhuma Hz ingekuwa ulaya mwigulu alipaswa kujiudhulu kupisha uchunguzi.cdhani kama vyombo vyetu vya dola Viko sirias.vingelala mbele na mtoa tuhuma na mtuhumiwa mpaka mbivu na mbichi ijulikane.
 
Kweli nilisahau, huu ni mpango wao wa kuchota, ndio maana hata zile za tozo siku hizi hatuambiwi zimekwenda wapi wala zimekusanywa ngapi, tupo chini ya kundi la majambazi.
Lakini jambo la kusikitisha sana sasa, hata akina CHADEMA husikii wakiyaibua haya, sijui ni sehemu ya maazungumzo ya maridhiano?
CHADEMA nao wamekubali kushirikishwa kwenye "kundi la majambazi"? CHADEMA wanapata mgao wao pia kutokana na uharamia huu?

Sasa tutakimbilia kwa nani sisi wananchi tupate wa kutusemea, mbali ya hawa akina Luhaga Mpina, hata kama wanafanya hivyo kwa maslahi yao!
 
mwiguu.jpg


Wakuu za sahizi nimeona picha sehemu fulani ya muigulu nchemba kuchota 1.7T kama ni kweli basi hiyo hela inatosha kuliisha vizazi 30
Mfano kama jamaa ana
-watoto 4
Na hao watoto 4 wakampatia
-wajukuu 16
Na hao wajukuu 16 wakampatia
-vitukuu 75
Na hao vitukuu 75 wakampatia
-vilembwe 300
Na hao vilembwe 300 wakampatia
-vilembwekeza 1400
Na hao vilembwekeza 1400 wakampatia
-viningina 6000
Jumla itakuwa vizazi vya watu 6000+1400+300+75+16+4=7795

Hawa watu 7795 ni approximately 7800.

Tuseme gharama za kusomesha shule nzuri za necta schools from year 1 mpaka to form 6 ni 50M
Na chuo abroad ni 70m.

Hivyo gharama za;
A. Kusomesha 140m roughly kwa mtoto mmoja pamoja na additional expenses.
B. Za extra za nyumbani na baada ya chuo 60m.

Total gharama kwa mtoto mmoja ni 200m.

Haya kizazi cha watu 7800 × 200m = 1.56T

Haya kachota 1.7T - 1.56T = 140B inabaki 🙄🙄🙄🙄🙄🙄

Wabongo hata kama mseme nini huyu jamaa anapesa ya kulisha vizazi saba na kuwapa elimu ya kutosha.

#pambaneni na umasikini wenu#

======

MATUMIZI NA MIKOPO NJE YA BAJETI: Mwigulu alikopa zaidi ya shilingi trilioni 1 kwa siri bila Kibali cha Bunge

"Kama mbunge nimeuliza mara kwa mara hapa bungeni, juu ya serikali kukopa nje ya bajeti. Lakini waziri wa fedha alishindwa kutoa majibu ya kina kueleza serikali imekopa kiasi gani nje ya bajeti, imekopa mikopo ya ziada kwa shughuli gani na sababu za kulikwepa bunge ni zipi (Hansard ya Bunge inajieleza).

Leo CAG ameweka wazi ukweli uliokuwa unafichwa. Kama fedha hizi zilikopwa kwa nia njema na kwa maslahi ya taifa kwanini zipokelewe na kutumika kwa siri? Huku ni kupoka madaraka ya bunge na kuna harufu ya ufisadi wa kutisha.

Kwa mujibu wa taarifa ya CAG 2021/2022 serikali kuu jedwali na 17, linaonyesha kuwa serikali imekopa nje ya bajeti iliyoidhinishwa na bunge na bila ridhaa ya Bunge kiasi cha shilingi trilioni 1.285.

Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba alikopa fedha hizi kwa ajili ya shughuli gani na kwa ridhaa ya nani? Fedha na kazi zilizopangwa katika bajeti 2021/2022 zilipitishwa na kuidhinishwa na bunge tena kwa kupigiwa kura ya NDIYO.

Fedha za ziada alizokopa Waziri wa Fedha ni kwa ajili ya shughuli gani na kwa ridhaa ya nani?" Luhaga Mpina, Mbunge wa Kisesa (CCM).

Jambo TV
Screenshot_20230423-000354~2.png
 
Back
Top Bottom