Lukuvi, mbio za sakafuni huishia ukingoni; jitafakari

Kumbuka
Msoga imerudi kazini, ilisemekana Lukuvi alitaka taratibu zifuatwe Msoga inapotaka kuimeza Dakawa, Msoga ikaona huyu ni mfitini, Msoga iliporudi mezani ikamkataa Lukuvi na kujigawia kiti cha msaidizi wa Lukuvi ili itimize azma yake ya kuimeza Dakawa

Decript the code
 
David Mwakalebela ndiye nani?
 
David Mwakalebela ndiye nani?
Alikuwa msemaji wa Yanga, badae akaingia kwenye siasa na kugombea ccm kupitia iringa mjini. Alishinda kwa kishindo kwenye kura za maoni na jina lake likakatwa kwa sababu za rushwa. CCM wakaweka mtu mwingine. Kikachafuka balaa. Hapo zikapigwa kura za hasira kwa msigwa.

Arusha nako aliyekuwa mbunge wa ccm ndugu felix mrema mmiliki na mfanyabiashara wa mashamba ya maua alipigwa chini kwenye kura za maoni wakati akitetea nafasi yake na nafasi akapewa batilda buriani, mrema wa ccm akahamishia majeshi kwa mrema wa chadema. Mwanamama Batilda hakufurukuta tena na kura zikaenda chadema.

Mbeya mjini nako makundi yakapasuana kura zikaenda chadema.
 
[emoji1] [emoji1787] [emoji23] huwa hawajui kustaafu hawa
Wanataka waonekane kwenye majukwaa tu
Aende akawe padri huko akamwage sumu
Nchi viongozi huwa hawastaafu

Yupo mwingine smbdy wasira ska ngoma ngumu

Ova
 
Mind you, LUKUVI aliwahi kumshikisha Mbabe mmoja Rushwa wakati wa JPM na kuwatia adabu sana Wanyang"anyi wa Ardhi sasa hao wahuni aliowatia adabu nyakati hizo kwa sasa ndio wameshika hatamu. Unategemea nini?
 
Viongozi waliomo CCM, hawajui kujijenga kwa wananchi moja kwa moja, hata kama wanaonekana kufanya kazi vizuri, badala yake utumishi wao wanaukabidhi kwa hao wanaowateua, na mara wanapoachishwa hizo nafasi, hawajui pa kuanzia ili kuwaended wananchi.
Kalemani aliweza hili, alikubalika sio tu kwa wananchi wake bali kwa wananchi wote.
Hajawahi kutokea mtia nia kwa nafasi ya urais kama Edward Lowassa,alikitikisa chama, serikali na organs zake,very strategically,wengine ni wakina
Dk. Medadi Kalemani ajilipue na kutia nia, jamaa atafaa sana.
 
kutetea ugali tu ndgu hakuna kingine
 
Nyie ndo mnawaponza na kutuletea balaa! Mtu kashatumika miaka yote bado mnalazimisha awepo! Let him go apumzike.
 
A
Aliporudi mara ya pili bado kura zilikuwa za huruma!?

Tunajisahaulisha kuwa hii nchi ni ya Watanzania wote wana haki sawa ya kuchagua na kuchaguliwa kuwa kiongozi ikiwa wana kidhi sifa za kuwa kiongozi.

Ndiyo maana katiba ya JMT haikusema mgombea yeyote lazima atoke CCN
 
Matamko ya hovyo aliyowahi kutoa mzee lukuvi ni kuhusu muungano kama video aliyoshare mdau hapo juu,,nyingine ni wakati akisuluhisha mgogoro wa ardhi iliyomuhusisha aliyesemakana ni mtoto/mjukuu wa mtemi huko rock city.
Kilikua ni kipindi kuna uvumi kuwa aliyekuwa Raisi ameshatangulia mbele za haki pasipo taarifa rasmi ya serikalee.
Mjukuu yule hakuridhishwa na namna waziri wa ardhi alihandle ule mgogoro hivyo akasema atahakikisha anaipata haki yake kwa kumuona Hayati Magufuli(huku mtu mzima akibubujikwa machozi)
Majibu ya mh Lukuvi wakati huo yalikua hivi kwa uchache ... nenda ukamueleze huyo raisi wako kama atakusaidia kuipata haki yako(kauli hii ilijaa jeuri sana)
Mwenye ilie video atakumbushe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…