Lukuvi: Nina Hofu na Uislaam aka "Islamophobia".

Status
Not open for further replies.
Lipumba aliufahamisha Umma kuwa kila wakati waislamu wanapoomba dua (kwa kiarabu mara zote), wanaomba kuwa Mwenyezi Mungu awanusuru na Makafir, awaepushe na mbinu za Makafir. Akajibiwa Takbir.

Makafir ndio wakina nani?

Amandla.......
Mkuu............wala usipate tabu.

A confused mind is a lost mind.
Mnaipenda CCM ya LUKUVI, na Kuipenda Serikali ya Kikwete, ambayo ni ya Mfumo Kristo...
.....wtf !!is that?
 
FaizaFoxy kila siku nakwambia CCM hawafai siku zote unakana na kuwatetea. Wakati CUF ina nguvu walisema ni ya Kiislamu na CUF wamekuja na majambia kuua watu kumbe ilikuwa ni propaganda ya kutaka ushindi. Ikaja Chadema mliona walivyoeneza propaganda eti cahama cha Wakristo na Kikanda na nia yao ilikuwa ni ushindi, inakuja Muungano wanasema tukiruhusu nchi tatu Zanzibar watakuwa nchi ya Kiislamu na Jeshi litatawala. Leo hii wamesahau wananchi kwa maoni yao kupitia Tume ya Rais (Ingawa wao wanaita tume ya Warioba) ikiongozwa na Mheshimiwa Judge Warioba Former makamu wa pili wa Rais, Waziri Mkuu, Waziri wa sheria, mwanasheria mkuu wa serikali, judge wa kimataifa wa mambo ya bahari, judge wa jumuia ya Africa Mashariki, Ahmed Salum, Former Waziri mkuu, waziri wa Ulinzi, Katibu mkuu wa Africa, katibu wa Kudumu katika umoja wa Maifa,; Mh. Judge Ramadhan, Former Jaji Mkuu, Brigedia general wa jeshi, Mwenyeki wa Tume ya Uchaguzi na wengine watu wengi mashuhuri lakini CCM wanasema hawa watu ni wapuuzi

Ndio ujue kwamba hawa watu CCM hawaitakii nchi mema na wapo tayari kutumia hata jeshi ili kufanikisha mambo yao

 
Huyu ajuza FaizaFoxy ni mnafiki sana..

Kwa hili halilolisema ni la ukweli asilimia zote! Unafiki huko wapi hapo? Kama kuzungumza lukuvi kazungumza kila mtu amesikia.

Na hapa amewapa majibu waislam yaliyo wazi kuwa hii serikali ni ya inaendeshwa kivatican.
 
Last edited by a moderator:

Mkuu,

Nakhis watumia mno lugha za tashtit na kebehi, ambazo haijengi asilan!...bali zazidi kuhatarisha hii hali tete inayolikabili Taifa letu changa kwa sasa!

Kama labda unajikhis una ghadhab nyingi!?... basi, kwanini usiketi kando na kuwaachia Wanajamvi wanzio wenye kumudu stahamala na staha ili kuendeleza mjadala huu!? Daah!

Ahsanta.
 
Dogo kajifunze Afaghanstan ishakwisha habari yake.Halafu wewe sio gaidi ni mtoto wa mama flani hivi.Kaa pembeni ngoja nikuitie wenye vielement vya ugaidi uone povu lao.Haya @Bhoko Haram njoo kuja huku umfundishe ugaidi huyu kijana mpenda dunia.
 

Serikali ya CCM haina maslahi kwa Watanzania, wewe pia unalijua hilo ingawa kila kukicha unaipigania hapa lakini zikija issues ndiyo unanza kuja na haya ya serikali Kristo blah blah blah. With CCM Tanzania haitafika popote ........... ni siasa tu hakuna maendeleo zaidi ya propaganda. Juzi juzi tu watu walikuwa wanauponda walaka wa Lema wakati una ukweli ndani yake. Udini unanuka Bongo noma na chanzo ni CCM!!
 
Leo nimeshuhudia wale wanaotugawa kwa kutumia Dini na hata ukabila,Lukuvi na chama chake hakika hawakwepi yatokanayo na kauli zenye kupandikiza chuki za Kidini.
Kwa kauli aliyoitoa Lukuvi na hakika madhara yake yanaweza kuigharimu Muungano hata kuliko hiyo serikali Tatu wanayoisingizia
 
wakati lukuvi anatamka (kujipaka mavi kanisani kama ulivyo sema) huo uharo alikuwa kajivua uanachama wa CCM?.

Mkuu,

Mbona watuletea hizo "siasa za uwanja wa fisi"!? Daah!

Tatizo lenu nyinyi "wataalamu" wa Bavicha/Ufipa...yaani takriban kila jambo basi mnahusisha ile vita ya walevi...yaani Chadema Vs CCM,sio!? Daah!

Ahsanta.
 
Hivi kwa nini Mheshimiwa Lipumba ametumia neno Interahamwe na sio Janjaweed? Wote hawa si vinara wa ethnic cleansing? Au ndio yale yale ya Umma?

Amandla.....
 
Wewe mwanamke always umekuwa na udini sana kila jukwaa upo. Huwa nafuatilia hoja zako zisizo na miguu wala kichwa naomba upunguze udini na kuwachukia wakristo maana wewe kila siku roho yako mbaya ni kwenye ukristo tu why. Jaribu kustaarabika
 

Angalia nawe usije ingia mtegoni kuuchukia ukristo kwa sababu ya Lukuvi. Lukuvi hakutumwa na wakristo. Kumbuka kampeni za Makamba Arusha wakati akimnadi Batilda,alipoingia msikitini na kutaka waislamu wampe kura. Wanasiasa wetu wanadhani hayo yanaishia ktk siasa tu. Wamevuka mipaka!

Somo kubwa kabisa ktk maelezo ya mtu kama Lukuvi, ni imani yangu kwamba nchi hii inaongozwa na watu hovyo kabisa! wote tunahisia binafsi na watu mbalimbali ktk maisha yetu na hata ktk familia zetu. mengine yanastahili kuwa ni siri ya moyo wako na hasa unapokuwa huna ushahidi. Huyu kiumbe naamini kwa viwango vyote vya ngazi zote, tangu kijijini hadi taifa, hakuna anapostahili kushika madaraka. Lakini jiulize Rais wetu ambaye ni muislamu, naye ana hisia hiyo? Kama ni hapana kwa nini mtu huyu aendelee kuwa ni public figure?
 
Last edited by a moderator:
Mkuu,

Mbona watuletea hizo "siasa za uwanja wa fisi"!? Daah!

Tatizo lenu nyinyi "wataalamu" wa Bavicha/Ufipa...yaani takriban kila jambo basi mnahusisha ile vita ya walevi...yaani Chadema Vs CCM,sio!? Daah!

Ahsanta.

ndivyo anavyopaswa kujibiwa yule mwanamama mwana CCM.hutakiwi kutumia upeo mkubwa kumjibu FF.saa zingine ni bora kucheza na akili yake ndogo.
BTW wewe unadhani muungano wa tz bara na znz una ukatoliki?!.kama sio akili ndogo nini hicho.
 

Yes! Huyu FaizaFoxy nimesoma mara nyingi maandiko yake, hudhani CCM ni mtetezi wake, ni kinga yake, ni mkombozi wake, n.k. Lakini anashindwa kabisa kuelewa kwamba huwezi kumutegemea CCM wakati unajua ni kundi lisilo na ethics. Watakufanyia lolote!

Leo sasa wamemuning'iniza na badala ya kuona ni kasoro ya CCM bado anapinda na kusema ukristo sijui ni nini!.... hai hoi hai hoi! Next time unapowasifia CCM ujue ni kazi ya kusafisha paka. Hakuna faida na sana sana tegemea makucha.
 
!
!
iyena iyena iyena iyeeena iyena iyeena sisiem nambari wani...
!
!
nadiriki kusema kwamba mbali nu kumpond lukuvi humu ndani ya jf hakuna lolote ambalo aidha waislamu au wakristo wanaweza kufanya.
!
!
selikali mbili ni lazima......tutake tusitake ila la maana tu kama wanavyohubiri kuwa hii ni ndoa,ni muda muafaka kutuambia katika ndoa hii nani mwanamke na ni nani mwanaume,baasi!...ili sasa baba mwenye nyumba aongoze familia yake.
 

FaizaFoxy na Ritz mbona mnakinzana na CCM chama adhimu ?? Kwanini safari hii mnajitenga na kuweka dini mbele?
Nimekuwa nikiwauliza swali rahisi sana, kama katiba mpya ni kwa ajili ya vizazi vijavyo, kwanini CCM wanataka kuidominate?
 
Last edited by a moderator:
Nadhani haumfahamu Ritz vizuri mimi sishikiwi akili na viongozi wa siasa kama nyie mnavyoshukiwa akili na Mbowe na Dr.Slaa, mimi naangalia dini yangu kwanza, wewe mbona hautaki kufuata tamko la Pengo anataka serikali mbili. mimi ni Mtanganyika nataka huu muungano uvunjike tuwakabidhi Zanzabar nchi yao halafu tupambane sisi kwa sisi huku Tanganyika, nyie wakirsto si mnafundishwa makinisani kwenu kuwa mchague serikali mbili, tusubiri tuone.
 


Mkuu mimi ni Mkristo Mkatoliki. Tumtofautishe Prof. Lipumba,Mwenyekiti wa CUF Taifa na Waziri ktk Serikali yetu ya JMT. Lukuvi amefanya makosa makubwa,kama ingekua nchi nyingine ameisha jiuzulu!
 
Lipumba aliufahamisha Umma kuwa kila wakati waislamu wanapoomba dua (kwa kiarabu mara zote), wanaomba kuwa Mwenyezi Mungu awanusuru na Makafir, awaepushe na mbinu za Makafir. Akajibiwa Takbir.

Makafir ndio wakina nani?


Amandla.......

Wote wenye hofu na Uislaam "Islamophobia" kama vile Lukuvi, eti hiyo ni khofu yake binafsi!

Wewe vipi? huna hofu?
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…