Lukuvi: Nina Hofu na Uislaam aka "Islamophobia".

Status
Not open for further replies.
Ndiyo maana nnamuomba Kikwete amstaafishe huyu kabla madhara hayajawa makubwa, Waislaam watajibu na Wakristo watajibu, itakuwa mtafuruku mkubwa kama hatua za haraka hazijachukuliwa za kumuondoa huyu William Lukuvi kwenye duru za siasa.

Ieleweke kwamba Lukivi amerudia kile ambacho Kikwete alikitamka katika ufunguzi wa Bunge la Katiba, hicho ndicho kinachomtia kigugumizi Kikwete ana serikali kumtolea uvivu Lukuvi. Kikwete alitoa vitisho hivyo alipofungua Bunge, wa kwanza kumnyooshea kidole ni Kikwete mwenyewe.
 

Hujatutendea Haki, Mimi ni Mkristo tena mkristo kwelikweli na nilishajibu hii hoja iliyokaa vema na kisawa sawa. Na wala sijamkejeli kwa kuwa Faiza ni muumini wa Uislamu. Wewe ndiwe mwenye shida na imani za dini badala ya hoja!
 
Nikuulize kwanza dada Faiza,,Unaunga mkono maoni yote ya Rasimu ya tume ya Warioba?Wewe ni mwanaCCM damu,nasisi wengine huku tunaona mapungufu mengi sana ya utawala huu wa CCM zaidi hata ya huo uhuni wa LUKUVI,Wananchi tunaumizwa sana na ufisadi,matumizi ya ovyo ya fedha bila huruma,kushamiri kwa kulindana kwenye biashara haramu na mengine mengi.Lakini ninachokushangaa kila linapokuja suala la uislamu kuguswa unajifanya mkali sana!Ni lini umeshawahi kukemea wanaCCM wenzako au hata humu kuhusu wenzako kuutajataja ukristu na CHADEMA?Kwa sasa CCM haina hoja za maana tena kwa wananchi zaidi ya vihoja!MWISHO KAMA UNATAKA UMMA TUKUELEWE KIKANE CHAMA CHAKO KWA MAOVU YOTE NA SI KWENYE UISLAM TU NDIYO KIKUUME,VINGINEVYO UTAONEKANA NI MDINI TU NA HUNA LOLOTE WEWE NA CCM YAKO YOTE.
 

Nilikua namwona wamaana sana faiza leo kanichefua sana
 
Ukiwa na viongozi Neutral mambo kama haya yanayotokea huwezi kuyaepuka,KIKWETE na PINDA ndicho wanachokifanya kwenye uongozi wao yaani hawataki kuchukiwa na yeyote hivyo wamekosa misimamo imara.Tuikumbuke hii nukuu ya Socrates kwamba "IF YOU ARE NEUTRAL IN THE SITUATION OF INJUSTICE,YOU HAVE CHOOSEN THE SIDE OF THE OPPRESSOR".Kwa nukuu hiyo tutegemee machafuko makubwa hapa kwetu Tanzania kwa siku za usoni kwa sababu ya kuwa na VIONGOZI LEGELEGE.
 
Hii thread ya unafiki mkubwa.lini wewe umeisema serekali vizuri.
 
Nchi za wenzetu kiongozi akikosea huwa anajiuzulu mara moja sasa hawa wa kitanzania hawaelewi kama wamekosea huwa wanaziba masikio na kama kawaida ya watanzania baada ya muda mfupi inakuwa siyo issue tena.
 
Look-v ameenda pale kama kiongoza na amemuwakilisha PM acha kudanganya kwa tukio ambalo limetokea within a month

hivi unaelewa kiswahili lakini? sikiliza tena kauli yake utaelewa, au haujui mtu akisema "mimi" anamaanisha nini?
 
Mimi naona umepanick zaidi.....sometimes mtu akitamka kitu you read between the line...kwa mfano alisema hayo kwa mazingira gani na amerefer nini....
 
majungu tu kwa mleta mada mbona aliongea mambo mazuri tu na hayakuwa na maana yoyote ile sasa wewe umetumia ujinga hili ni neno zuri kweli acheni kudanganya watu kwa kuzalisha uongo
 
Mimi naona umepanick zaidi.....sometimes mtu akitamka kitu you read between the line...kwa mfano alisema hayo kwa mazingira gani na amerefer nini....

Kutamka na kuhutubia ni vitu viwili tofauti, hiyo ni hatuba ya William Lukuvi Kanisani, umeisikiliza?
 
Siungi mkono serikali mbili, ila naunga mkono maudhui ya serikali mbili kama yalivyotolewa na Lukuvi kanisani na baadaye kufafanuliwa bungeni.

cc: Muanzisha mada
 
Kukosea kwa Lukuvi hakuhalalishi Uchochezi wa UKAWA. Mkitaka Serikali basi tayari zipo. Ya Muungano, ya Zanzibar na Kivuli ya Kina Mbowe.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…