Lukuvi: Nina Hofu na Uislaam aka "Islamophobia".

Lukuvi: Nina Hofu na Uislaam aka "Islamophobia".

Status
Not open for further replies.
Usiogope greater is he who is in me than who is against me; siyo bahati mbaya nipo sober!

Mkuu,

Mie sijaogopa maana sikuona vitisho vyovyote mle ndani ya bayana yako, au weye ulikusudia kutisha watu!? Daah!

Pia walaa sijakwambia yakua ati ulilewa au hukuwa timamu!?...sasa hiyo khabar ya sobriety yajia nini,Yakhe!?

Ahsanta sana!
 
Jaji warioba wakati anawasilisha rasimu,aliwaasa wajumbe wa bunge maalumu la katiba kuwa,ili katiba mpya ipatikane,MAONI ya wananchi yalimo yenye kwenye Rasimu ni la lazima yaheshimiwe. Tunachokiona sasa ni janja ya kutunga kanuni za kupitisha maoni ya watawala badala ya maoni ya wananchi
 
Mkuu,

Nakhis watumia mno lugha za tashtit na kebehi, ambazo haijengi asilan!...bali zazidi kuhatarisha hii hali tete inayolikabili Taifa letu changa kwa sasa!

Kama labda unajikhis una ghadhab nyingi!?... basi, kwanini usiketi kando na kuwaachia Wanajamvi wanzio wenye kumudu stahamala na staha ili kuendeleza mjadala huu!? Daah!

Ahsanta.

Naona katumia lugha nyepesi inayotoa taswira halisi ya hoja yenyewe,ingekuwa bora kuivunja vunja hiyo hoja,mathalan mtoa hoja hashabikii ccm? Na lukuvi si kiongozi wa serikali ya ccm? Na hakuteuliwa na m/kiti na rais wa ccm? Na lukuvi na pinda hawawakilishi ideology za ccm? Na kama mfumo kama anavyotaka kutuingizia akilini ni mfumo kristo si yeye anayeushabikia kwa nguvu zote na kuwakejeli wanaoipinga,leo unauona ni mfumo kristo isnt it a confused mind?
 
Jamani watanzania akili zenu mmepeleka wapi! mleta mada ameharibu argument aliyokuwa anaijenga kwa sababu zisizo na mashiko, udini. Haileti maana kabisa, nchi yetu kwa sasa viongozi wakubwa karibia wote ni wa dini ya kiislamu, inawezekanaje wote kwa pamoja waendeleze huo mfumo kristo? mleta mada anatulazimisha kuamini kuna tatizo katika dini ya uislamu kwamba unaweza kuwa ni muumini lakini wakati huo huo ukawa mfuasi wa ukristo!

Serikali yenye viongozi wakubwa kutoka dini ya kiislamu watumie dira za kikristo kuongoza nchi kuwagandamiza waislamu, it does not make sense! Lukuvi kaharibu, na sisi kwa upofu wetu tumekimbilia kwenye dini! Ningeliona mtoa mada ana argument ya maana kama angehusisha chama cha CCM na kauli hii. Lakini kwa kuwa ni mfuasi kindakindaki amejitoa ufahamu kwa makusudi. Inaleta maana zaidi kusema CCM inaamini katika mfumo kristo maana sera zake ndizo zinaongoza nchi, lakini ajabu ni kuwa viongozi wake wengi ni waislamu.

Hivyo hitimisho ni kuwa viongozi waislamu wa CCM wanaongoza nchi kwa kutumia ukristo! Funguka mtoa mada katika upofu uliokushika, tatizo si dini, tatizo ni viongozi wa CCM.
 
Mkuu,

Mbona watuletea hizo "siasa za uwanja wa fisi"!? Daah!

Tatizo lenu nyinyi "wataalamu" wa Bavicha/Ufipa...yaani takriban kila jambo basi mnahusisha ile vita ya walevi...yaani Chadema Vs CCM,sio!? Daah!

Ahsanta.

Wakati wewe unataka aihusishe na vita vya ukristu na uislam? Mkuu hebu tujuze alienda kama kiongozi wa serikali au wa kidini?
 
JAMANI HUO UAMSHO NI KITU GANI HASA?KATIBA.UONGOZI,MOTO, na UTENDAJI WAKE UPO JE?WALIO NA TAARIFA ZA KWELI AU WANAOWEZA
KUZICHOTA KWENYE GOOGLE WATULETEE HAPA ILI WATU WASIOGOPE VITU VIZURI
 
Hebu iweke picha ya mzungu aliyevaa nepi anayeabudiwa na wakristu. Ukishindwa utakuwa na tofauti gani na wale wazungu waliochora katuni za Mohamed?



Amandla.........

Naona sasa mmepotoka. Badala ya kujadili mada mnaanza kutofautiana kwa mitazamo ya Udini. Mnavyofanya ndivyo anavyopenda mtawala. Na nawahakikishia, mkiendelea hivi, mtaendelea kutawaliwa milele. Kuna watu humu wako TISS wanapenda na wanafurahi kwa jinsi mlivyohama kutoka kwenye mada kuu nao wanazidi kuchochea na nyie mnaendelea kupigana wenyewe kwa wenyewe kuhusu Ukristo na Uislam wakati wenzenu wanawacheka.
 
Aidia
Hivi uelewa wako ni mdogo kiasi hiki? Suala la DINI limekujaje kwenye kunywa cha kiongozi wa serikali tena akiwa kanisani, heri labda angekuwa ni muislam, kiongozi huyu ni mkristo then anadiriki kutamka haya, si UCHOCHEZI huo? Miye nasema atalayeleta maafa nchi atatoka ccm.
 
huyo ni mnadhimu na anachokifanya hapo
ni kueneza sera za chama ndani ya Bunge kwahiyo msimzuie
ametumwa na chama tawala.
 
Wewe kweli kilaza, ongeza ufahamu mara moja moja kwa kusoma magazeti na kusikiliza taarifa za habari za radio na TV!

Kasema mwenyewe kwamba Waziri Mkuu ndio alomtuma kwenda pale Kanisani!

Unadhani tunamzulia kama vile wewe ulivyozoea kuzua?!

Nyambafu mkubwa, Lukuvi mwenyewe kasema alikuwa anaelezea hisia zake, mimi nimemsikia mwenyewe wewe unaniambia habari za magazeti.
 
Naona sasa mmepotoka. Badala ya kujadili mada mnaanza kutofautiana kwa mitazamo ya Udini. Mnavyofanya ndivyo anavyopenda mtawala. Na nawahakikishia, mkiendelea hivi, mtaendelea kutawaliwa milele. Kuna watu humu wako TISS wanapenda na wanafurahi kwa jinsi mlivyohama kutoka kwenye mada kuu nao wanazidi kuchochea na nyie mnaendelea kupigana wenyewe kwa wenyewe kuhusu Ukristo na Uislam wakati wenzenu wanawacheka.

Aliyeleta mada hii aliileta kwa malengo ya kidini. Alidai kuwa Lukuvi ni mfano wa mfumo kristu ambao unatawala nchi yetu. Wewe kote huko haukuona udini mpaka pale tulipoamua kupinga hoja yake?

Amandla.......
 
Lukuvi amekiri bungeni aliyoyasema kanisani
Alisema ameamua kusema kile alichokichangia katika kanisa hilo wakati wa kusimikwa kwa Askofu Joseph Bundala kwa kuwa hana tabia ya unafiki na alitaka maneno hayo yarekodiwe kwenye kumbukumbu za Bunge.


"Nayasema yote haya kwa kuwa naamini huo ndiyo msimamo wangu na utakuwa msimamo ambao wakati wote utaendelea kuwa hivyo na ninawataka ndugu zangu kuacha unafiki," alisema.

Alikanusha madai kwamba ni mchokozi badala yake akarusha tuhuma hizo kwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Shariff Hamad.

Alinukuu hotuba ya kiongozi huyo wa chama kikuu cha upinzani Zanzibar aliyoitoa mwezi uliopita katika Uwanja wa Kibandamaiti Zanzibar kwamba imekuwa ikipotosha hotuba ya Rais Kiwete kwa sehemu kubwa kuhusu mchakato mzima wa Katiba.

Lukuvi pia aliituhumu Ukawa kwamba imepanga kuigawa Tanzania katika vipande, kwamba Zanzibar itatawaliwa na CUF, Tanzania Bara na Chadema halafu CCM ipewe urais wa Muungano.

"Kutokana na hilo, nani ambaye hatakuwa na wasiwasi juu ya haya mambo? Nataka niwahakikishieni katika Katiba hii hakuna chombo chochote wala mtu yeyote atakayenizuia kusema ninachokiamini ilimradi nasema ukweli na ninayoyaamini," alisema.

Alisema kama maneno yake yamewachukiza zaidi wapinzani, basi waendelee kugoma zaidi alichofanya kilikuwa kwenda kusimamia masilahi ya serikali mbili zenye masilahi kwa wananchi.

Lukuvi alisema wakati wote wananchi hawataki serikali tatu, bali wanataka maendeleo ikiwamo maji, barabara na vitu vingine lakini vyote viwe kwa kupitishwa kwa serikali mbili.

Wapi alipokiri Lukuvi kuwa katumwa na Pinda kusema aliyoyasema? Hata haya hamna?

Amandla......
 
Kama kawaida yenu, unaogopa kuwakosoa wana Ummah wenzio. Aliyekwambia Gene Robinson mlutheri nani?

Kuhusu mtu kuoa mbwa? Soma hapa:FAKE NEWS: Calif. Allows State-Recognized Human Animal Marriage
Gazeti lililochapicha hiyo nEWS linaitwa National Report. Ukiliamini hilo utaamini The Onion! Sisi wakristu tuna kitu tunaita satire. Una uhuru wa kukosoa, kuchambua, kutania n.k. imani yako bila chizi mmoja kukutangazia fatwa.

Kama Uislamu si Pakistan, Taliban etc. sasa kwa nini mnataka Zanzibar iwe nchi ya kiislamu?

Amandla.....
Nimekutajia Rev Gene Robinson kwa makusudi kumbe unamjua vizuri kama ni shoga.

Ni kiongozi wa Kanisa Anglican, ni shoga vipi ndiyo ukirsto huo?

Haya hautaki habari za Mbwa,je habari za mashoga wa jinsia moja kufunga ndoa Kanisani vipi ndiyo Ukirsto.

Uzuri wa Uislam hauwezi kuulizwa habari za nchi nyingine unaulizwa umeufanyia nini Uislam pale ulipokuwepo Zanzibar wana haki kama nchi yao kujiamulia mambo yao.

Una hofu sana na Uislam.
 
JokaKuu,

Unawashauri warejeshe membership cards za CCM ili wende wapi,jamani!? Daah! Teeh! Teeh! Teeh!

Mkuu Ritz anadai yakua hata hao Chadema ati role model yao ni CCM!?...yaani Chadema ni branch tu ya wachovu waliofukuzwa/wasiotakiwa ndani ya CCM!? Daah!

Yule Dr Slaa mwenyewe, japo yupo pale Ufipa/Chadema...lakini mpaka kesho ana membership card ya CCM na anailipia,au!? Duuh!

Ahsanta.

Huwezi penda ccm halafu ukatetea upuuzi unaofanywa na viongozi wa ccm kwa unafiki uitoe kwenye makosa na kuwatupia wakristu,mbaya zaidi hujasikia viongozi wake si tanganyika wala zenj waliokanusha,kisha uwalaumu na kuwakejeli chadema wakati si waliokosea, jibu ni nini,chadema inaongozwa na padri wa zamani mkristu ambae kwako ww ni adui kuliko hao waliolikoroga ccm. You are confused lot
 
Wapi alipokiri Lukuvi kuwa katumwa na Pinda kusema aliyoyasema? Hata haya hamna?

Amandla......
Wewe ndiyo hata haya hauna una mhaba sana na Lukuvi, pitia majibu ya Lukuvi anayomjibu Prof. Lipumba, siyo kila kitu unapinga au tukuletee audio?
 
Aidia
Hivi uelewa wako ni mdogo kiasi hiki? Suala la DINI limekujaje kwenye kunywa cha kiongozi wa serikali tena akiwa kanisani, heri labda angekuwa ni muislam, kiongozi huyu ni mkristo then anadiriki kutamka haya, si UCHOCHEZI huo? Miye nasema atalayeleta maafa nchi atatoka ccm.

Inaelekea wewe umebahatika kuwa na taarifa zaidi.Hivi huu UAMSHO unaomuoogopisha LUKUVI ni kitu gani haswa.Je UKAWA watakuwa na UAMSHO huko Zanzibar?
 
tatizo mleta mada ni mdini sana inamana hujui kuwa uamsho ndyo wanaochoma makanisa?na haohao ndyo wanaodai jamhuri ya zanzbr mbona hujawahi kuwalaani wanaochoma makanisa.tatizo hamtaki ukweli .mi binafsi nataka serekali 1

uamsho walichoma makanisa kuna ushahidi gani? Ni mwaka sasa waliwekwa kizuizini kutafutwa uo ushahidi wa waliyoyafanya haupo una habari kwamba kesi yao moja imefutwa kwa kukosekana ushahidi? Hii ni nchi ya propaganda ndugu kila anaetaka lake anaingiza propaganda yake afanikiwe
 
Faiza wewe uko mdini sana. Muda mwingine nakufatilia na nakusoma chuki zako kwa Nyerere na hata viongozi wake waandamizi.

Kwa taarifa yako Nyerere huo uhuru hakupata mwenywe,na hii nchi sio ya wakristo. Tena waislam walimsaidia sana Mwalimu katika kupata uhuru wa nchi na hata kufika mpaka hii leo.

Wewe ni mtu hatari sana katika jamii ya waafrica na watanzania kwa ujumla. Chumvi au mbegu unayopandikiza hapa haitakuacha, itakutafuna mpaka kaburini mwako na hata mpaka wewe na watoto wako naa wajukuu zako.

Kuna ubaya gani kutoleta hoja bila kuleta udini au kuzungumzia na kuukashifu ukristo??
Mimi nilikulia msasani. Majirani zangu asilimia tisini walikuwa waislam. Kipindi cha holy month of Ramadhan walikuwa wanatuleta daku au hata futari nasi tunawapa chochote kilichopo hata maji baridi bure barabarani wanpotoka msiktini.Sikuwahi kuona chuki wala kusikia neno,walisheherekwa pamoja nasi sikuku zao na sikuku zetu kwa pamoja.
Until lately watu kama nyinyi mashetani na yule gaidi serikali inamfunga sijui sheikh nani mnapanda chuki kwa watz.

Mimi nafanya kazi serikalini. Nachokuambia nyinyi mnabahati Dr KIkwete ni mtu mpole na mtaratibu. Baada ya 2015 leteni ujinga huu kutenganisha watz tutawasaka hadi makwenu.

Waambieni waliowatuma kwamba tutaenda mfumo wa jicho kwa jicho. Hamwezi kutuharibia nchi yetu kwa tofauti za kidini na kikabila. Hata siku moja.

Lukuvi hawakilishi wakristo wote wala serikali kwa ujumla. Yule mtu ni mjinga sijapata kuona. Na watu kama hawa wanaongea wanavyotaka hawajui madhara katika nchi ndio wanaleta shida.

Wewe kuleta hoja na kuunganisha mawazo yako serikali na mfumo wake nathani ni kupungukiwa fikra kama sio ugaidi ulionao ndan. Na kwa taarifa yako Tanzanja haiweze kuwa nchi ya kiislam wala ya wakristo. Utakufa wewe utaiacha na wajinga wenzako wote wenye hila za kigaidi.





The king.

Mkuu,

Umezungumza mangi mno dhidi ya Mkuu FaizaFoxy...nina hakika mwenyewe yupo hapa anakusoma na takupatia majawaba yako murua...kama akipata fursa na ikilazim!?

Kama weye unajikhis umo Serikalini kama unavyotujuza!?...sasa kwanini watumia lugha hiyo ya vitisho na dharau!?

Kwa context ya hiyo bayana yako ya kipuuzi...yaani unajaribu kutuaminisha yakua huyo Rais Kikwete "Boss wako", "udhaifu" na "ustaarabu" wake ndo chanzo cha haya matatizo unayodai yanafanzwa na akina "FaizaFoxy na genge" lake kama ulivyotuambia!?

Wee kweli ni mpuuzi na mnyama wa hali ya juu!...yaani unawatisha Wanajamvi hapa yakuwa utawasaka baada ya 2015!?...kwa uhakika upi uliokua nao na kwa vigezo vipi!? Embu tujulishe hapa hapa jamvini!?

Usituletee story zako za vijiweni hapa!

Sasa, mie binafsi nakuhakikishia yakua weye ni kiumbe mduchu mno kwenye hiyo system/serikali hapo nyumbani! Na walaa hizi siasa chafu/za kuchafuana sio level yako au game yako...asilan abadan!

Weye ni mtoto mduchu mno...katafute chandimu ukacheze na wanzio! Ebo!

Yaani unatuletea vitisho vya kitoto na ukosefu wa adab hapa jamvini,sio!?

Wee unajaribu kumshutumu vikali Mkuu FaizaFoxy yakua ati yakua yeye na "genge lake" wanahatarisha hiyo myth yenu ya "umoja na amani" hapo nchini!?...sasa weye mwenyewe umejisoma kwa makini huo uharo wako ulotuletea hapa!?

Kwa hiyo hayo ndo maoni au mtazamo wa baadhi ya nyinyi wafanyikazi wa serikali baada ya hiyo 2015!?

Sasa je unafahamu kiundani athari za matamko ya kiharamia kama hayo yako!?...khasa kama hao unaowashutumu wakiamua kuyachukulia serious, na labda nao kuamua kujiandaa ili kukabiliana na vitisho vyako vya kitoto!?...ambavyo ati unajaribu kutuaminisha yakua ndo msimamo wa wafanyikazi wenye madaraka ya juu serikalini sio!?

Embu tutajie weye unafanzia idara ipi huko serikalini!?...kama utasema kweli, basi nakuhakikishia japo leo ni w'end lakini kama una wadhifa wowote nyeti kama unavyojaribu kutuaminisha...basi, utaitwa leo hiihii ukajieleze kwa Boss wako yeyote hapo!?

Wacha nipate coffee hapa kiduchu, nitakurejea!

Ahsanta sana!
 
ccm wakitaka kitu watatumia kila njia ili mradi kipatikane:
1. Wataua yeyote ili wasafishe njia, na kwa mchakato huu wameishaua tayari ili kutoa kiwingu na kutishia watakaojitia kiherere.
2. Wataamsha hisia za udini, ukabila, ukanda. Wameisha fanya hayo na wanaendelea.
3. Watatoa chochote kwa yeyote ili mradi azima yao itimie. Walitoa kila kitu kwa tume ya mzee warioba walidhani watafanya kwa matakwa ya ccm hata wapinzani walikuwa na hofu ya maoni ya wananchi kuchakachuliwa. Mungu akaepusha uzalendo wa kweli umeonyeshwa na tume. Ujumbe ktk tume ulikuwa hongo ya ccm.
4. Wataiba popote na kwa namna yeyote km ilivyokuwa epa na dada zake.
5. Watamnunua yeyote km walivyowanunua baadhi ya wasomi km shivji na wengineo.
6. Watazinunua mpaka taasisi na ngo km ilivyofanya kwa taasisi/ngo ya tiba asili wamchague kingunge aingiie aliko sasa.

Lukuvi ni wakala tu katika mambo ambayo ccm wanaweza kufanya.

Kikwete ni wakala mzuri wa ccm, na ndiye aliyechochea udini 2010 ili mradi aonewe huruma na kupewa kura za waislamu.

Yote yanafanyika kwa ujinga na woga wa watanganyika na wazanzibari. Tuamke na kukataa upumbavu huu. Ina maana ccm ndio raia halisi, na kuwa mzalendo ni lazima uwe ccm. Hapana, ccm ni waroho wa madaraka na wanafiki wakubwa. Udhibitisho ni huu ktk bunge la katiba.

Wengi na mengi yatasemwa yaliyo mabaya zaidi ya yale alosema lukuvi, tujiandae kuyasikia.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom