M/kiti wa UVCCM Wilaya ya Mwanga na Katibu Msaidizi Mkoa wa Vyuo Vikuu washambuliwa kwa Risasi

M/kiti wa UVCCM Wilaya ya Mwanga na Katibu Msaidizi Mkoa wa Vyuo Vikuu washambuliwa kwa Risasi

Hendry Kileo kugombea ubunge jimbo LA mwanga 2015 kila lakheri kileo
Nadhani ni vyema vijana kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali ila kama njia kama hii ya kutumia mitutu kutaka kufupisha safari za wengine ni jambo la hatari sana.
 
Mmeamua kuja na hoja nyingine pale mnapoona hamkubaliki mnaingiza propaganda kama hizi ili wale wanaokubalika PoliCCM waweze kuwakamata na kuwapa vitisho, jambo linalotupa wasiwasi juu ya hii habari yako haina viambatanisho vya kuipa uzito na hii nafikiri itakuwa haina tofauti na yale tuliyoyaona jana kule Kalenga wale jamaa wa CCM walikuwa wameshika vigogo vilivyopigiliwa misumali wakisema vilikuwa vimewekwa na wana CDM ili eti wapate pancha wasiweze kufika kwenye mkutano.

Pia naomba ufafanuzi wa neno hili (
kauli mbiu ya “..CCM Mwanga Ukimya sasa Basi..”)


nilitegemea mpiga picha kuwa muwazi kwa kupiga picha namba ya gari walau picha moja kwa mbele.

Napata ukakasi wa taarifa hii
 
Hendry kileo sialishaa tangaza nia mwanga ambapo tukio limetokea
 
ina maana hizo picha haujaziona ama..??? tumia kichwa sio ukitumwa kuandika unakuja spidi na kuandika bila mpangilio..kwanza hapa haijatajwa chadema mbona mnajishuku..au mmehusika..??


kwanini uwazi haupo kutuweka wazi walau picha moja kuonesha usajiri wa gari? Lengo kama kunamwenyekuweza kufatilia na kuthibÍtisha, isijekuwa watu wamechukuwa picha kwenye gari iliyopata majanga mengine na mahala tofauti
 
Taarifa iliyotufikia hivi punde inaeleza kuwa Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Mwanga Kilimanjaro Ndugu Japhar Mghamba na Katibu Msaidizi wa Mkoa Maalum wa Vyuo Vikuu wilaya ya Dar es salaam Ndugu Daniel Zenda wameshambuliwa kwa Risasi na watu wasiojulikana.

Viongozi hao ambao wapo wilayani Mwanga Mkoa wa Kilimanjaro kwenye operesheni maalum inayojulikana kama operesheni Kokoro ambayo inalenga kuhamasisha vijana wa upinzani na wasio na vyama kujiunga na CCM, kuhamasisha Vijana wa CCM kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi ujao wa Serikali za mitaa hapo baadae October mwaka huu, na kukagua, kuhamasisha na kuelezea katika matawi na kata juu ya Utekelezaji wa Ilani ya Chama kwa kauli mbiu ya “..CCM Mwanga Ukimya sasa Basi..”

Viongozi hao wa Jumuiya na Chama cha Mapinduzi wamekumbwa na Mkasa huo wa kusikitisha wakiwa wamemaliza sehemu ya kwanza ya Ziara hiyo katika Kata ya Kisangara na wakirejea mwanga mjini, Kwa bahati Njema hakuna aliyepoteza maisha na tayari taarifa zimesharipotiwa kituo cha Polisi Mwanga ambapo taratibu za Uchunguzi zinaendelea.

Matukio ya vurugu na vitisho vimeanza kutawala kwa kasi kubwa katika ulingo wa Siasa za ndani hapa nchini kwetu, ni vyema sasa Serikali ikawa macho katika kuangazia upande wa Siasa kama eneo hatari (Danger Zone) ili kulinda Uhai wa Vijana na wananchi kwa Ujumla.
Mmebakisha mkakati wa kumuuwa Zitto na kusingizia Chadema
 
Pole zao,ila Kama Daniel Zenda ni yule niliyesoma naye Udom basi nazidi kuamini kuwa CCM imeshakosa wanasiasa na viongozi pia.Kumbe hata kuwatafutia waheshimiwa viburudisho unaweza kupewa cheo?
 
CCM siku zote wakizidiwa haya ndo matendo yao ili mikutano ya kisiasa ipigwe marufuku kama ilivyo Lindi na Mtwara. Haiwezekani hao kama sio CCM wasijulikane kwani CCM iko kila mahali. Hii ni janja ya nyani........indi bichi
 
Mbinu chafu ya ccm kuendesha siasa kihuni wajipiga risasi wenyewe halafu wadai ni wapinzani.
 
Pole Ma Comrade wetu, wanashindwa kwenye Masanduku ya kuru, sasa wanatafuta ushindi kupitia Risasi. Hasira zetu waliziona kwenye uchaguzi mdogo wa Serikal za mitaa 24-3, wataziona kwenye hili Bunge la Katiba, Uchaguzi wa Kalenga na wa Chalinze. Wakatafute Makontena ya Silaha kabisaaa!

Acha kuharibu ushahidi dada Salome, hakuna mtu asiyejua kuwa hiyo ni vita ya ndani ya chama. Chadema inatishwa na hao viroboto? Jogoo hafi kwa utitiri wala sio sera ya Chadema kuwashambulia wanao wapinga. Hizo ni sera zenu huko, mara kuwamwagia watu tindi kali na kuwapeleka hospitali ili mtembeze ka mdoli. Mara muwatoboe macho ili mpate huruma za wasikilizaji. Poleni sana ila msipoteze uchunguzi kikulacho ki nguoni mwako. Mmetoka sera ya kutoboa macho sasa mmeingia ya risasi za moto! Kaazi kwel
 
Hayo ni matokeo ya Makundi ccm mwanga.
Kuna kundi kutoka ugweno na kundi Mwanga na kundi Tambarare kila kundi lina mtu wao kumrithi magembe.
 
Haaa..nlipita jana nikakuta hiyo issue..kuna sehemu kuna Humps karibu na chuo cha Veta pale Kisangara..Duuhh..pole yao..huyu mmoja c ndo mmiliki wa Mabasi ya Kirumo..???
 
Chadema hawakwepi hili suala hata wafanye vipi hii tabia ya kipumbavu sana.
Kwa akili za matope kama hizi wahalifu hawezi kupatikana.

hawa vijana walijipiga wenyewe, au kama ni wahalifu wana huruma.
kulenga kioo cha nyuma manake walitaka asiumie mtu,
au kupunguza hasara kwa kuwa kioo cha nyuma elf 50 wakati cha mbele laki tatu.

hawa lazima walijipiga.....
 
huenda tatizo ni mke wa mtu....maana hawa vijana..ni kama copy ya mwigulu.
yaani we chalii hamnazo aisee..,mtu anafikwa na tukio very serious like this then mijitu mingine inaleta hoja za kipumbavu.
 
Ccm mumebakiza sera yakujichoma Moto tu mkibahatisha kuhulumiwa nawananchi maana hiyo nanyingine nyingi tumeona mumetekeleza kwenye operation tokomeza
 
Huo ni utapeli wa kisisasa! kauli mbiu yenu “..CCM Mwanga Ukimya sasa Basi..” mnataka kuhadaa jamii kwamba mumeshambuliwa kumbe ni nyinyi wenyewe mumepanga mipango ya kiipuuzi.Watanzania wa leo yatupasa kuelewa na sio kudanganywa tena.Hata nini vijana munaanza kujifunza kufanya mambo ya hila? Taifa hili linakwenda wapi?


 
kikwete ni mtu mmoja mbaya sana nina uhakika lazima atakwenda the hague haisezekani anaendesha nchi na chama kimafia huyu mzee ni mtu hatari sana
 
Kwa hiyo matukio yote haya hapa chini wameyafanya CHADEMA na hawajachukuliwa hatua! TAFAKARI NDUGU KABLA YA KUPOST UJINGA HAPA JF.

1. Aliyemmwagia Tindikali Said Kubenea
2. Aliyemteka na kumtesa Dr. Ulimboka
3. Aliyemuua Mwangosi
4. Waliomuua kwa kumchinja Mwenyekiti wa CHADEMA kule Usariver
5. Wale vijana wa UVCCM waliowashambulia wabunge wa CHADEMA kule Mwanza
6. Waliomteka na kumtesa Kibanda
7. Waliomuwekea sumu Mwakyembe
8. Waliomgonga kwa makusudi Mwakyembe kwa lengo la Kumuua
9. Waliomuua yule Kada wa CHADEMA kule Igunga
10. waliolipua Bomu katika Mkutano wa CHADEMA pale Soweto
11. Waliolipua Kanisani Olasit, Yule kijana waliyemrundikia zile tuhuma sidhani kama ni mtuhumiwa halali.
12. Waliomuua Padri kule Zanzibar
13. Waliowamwagia Tindikali wale Mabinti wa UK
14. Waliomshambulia Dr. Mvungi hadi kusababisha kifo chake
15. waliomsababishi kifo Waziri wa fedha Mgimwa
16Waliowamwagia Tindikali yule Shehk na mtoto wake jana kule Arusha.
17. Waliowatuma akina Masogange kupeleka ile Sembe Kule South Africa na kuwasaidia kuififisha ile kesi na kugeuza madawa kutoka Heroin/Cocaine na kuwa PHENOBABITONE

imekuaje kwenye hiyo Orodha Hayati Chacha Zakayo Wangwe Hayupo ? au kwa kuwa wananchi wa Tarime walishachukua Hatua yakurudisha Jimbo kwa Chama cha Mapinduzi ili kuepuka Vifo visivyo vya Lazima vya Wabunge wao?
 
Back
Top Bottom