lumumba the son
JF-Expert Member
- Jun 16, 2011
- 207
- 60
- Thread starter
-
- #41
Nadhani ni vyema vijana kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali ila kama njia kama hii ya kutumia mitutu kutaka kufupisha safari za wengine ni jambo la hatari sana.Hendry Kileo kugombea ubunge jimbo LA mwanga 2015 kila lakheri kileo
Mmeamua kuja na hoja nyingine pale mnapoona hamkubaliki mnaingiza propaganda kama hizi ili wale wanaokubalika PoliCCM waweze kuwakamata na kuwapa vitisho, jambo linalotupa wasiwasi juu ya hii habari yako haina viambatanisho vya kuipa uzito na hii nafikiri itakuwa haina tofauti na yale tuliyoyaona jana kule Kalenga wale jamaa wa CCM walikuwa wameshika vigogo vilivyopigiliwa misumali wakisema vilikuwa vimewekwa na wana CDM ili eti wapate pancha wasiweze kufika kwenye mkutano.
Pia naomba ufafanuzi wa neno hili (kauli mbiu ya ..CCM Mwanga Ukimya sasa Basi..)
ina maana hizo picha haujaziona ama..??? tumia kichwa sio ukitumwa kuandika unakuja spidi na kuandika bila mpangilio..kwanza hapa haijatajwa chadema mbona mnajishuku..au mmehusika..??
Chadema hawakwepi hili suala hata wafanye vipi hii tabia ya kipumbavu sana.
Mmebakisha mkakati wa kumuuwa Zitto na kusingizia ChademaTaarifa iliyotufikia hivi punde inaeleza kuwa Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Mwanga Kilimanjaro Ndugu Japhar Mghamba na Katibu Msaidizi wa Mkoa Maalum wa Vyuo Vikuu wilaya ya Dar es salaam Ndugu Daniel Zenda wameshambuliwa kwa Risasi na watu wasiojulikana.
Viongozi hao ambao wapo wilayani Mwanga Mkoa wa Kilimanjaro kwenye operesheni maalum inayojulikana kama operesheni Kokoro ambayo inalenga kuhamasisha vijana wa upinzani na wasio na vyama kujiunga na CCM, kuhamasisha Vijana wa CCM kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi ujao wa Serikali za mitaa hapo baadae October mwaka huu, na kukagua, kuhamasisha na kuelezea katika matawi na kata juu ya Utekelezaji wa Ilani ya Chama kwa kauli mbiu ya ..CCM Mwanga Ukimya sasa Basi..
Viongozi hao wa Jumuiya na Chama cha Mapinduzi wamekumbwa na Mkasa huo wa kusikitisha wakiwa wamemaliza sehemu ya kwanza ya Ziara hiyo katika Kata ya Kisangara na wakirejea mwanga mjini, Kwa bahati Njema hakuna aliyepoteza maisha na tayari taarifa zimesharipotiwa kituo cha Polisi Mwanga ambapo taratibu za Uchunguzi zinaendelea.
Matukio ya vurugu na vitisho vimeanza kutawala kwa kasi kubwa katika ulingo wa Siasa za ndani hapa nchini kwetu, ni vyema sasa Serikali ikawa macho katika kuangazia upande wa Siasa kama eneo hatari (Danger Zone) ili kulinda Uhai wa Vijana na wananchi kwa Ujumla.
Pole Ma Comrade wetu, wanashindwa kwenye Masanduku ya kuru, sasa wanatafuta ushindi kupitia Risasi. Hasira zetu waliziona kwenye uchaguzi mdogo wa Serikal za mitaa 24-3, wataziona kwenye hili Bunge la Katiba, Uchaguzi wa Kalenga na wa Chalinze. Wakatafute Makontena ya Silaha kabisaaa!
Chadema hawakwepi hili suala hata wafanye vipi hii tabia ya kipumbavu sana.
Kwa akili za matope kama hizi wahalifu hawezi kupatikana.
yaani we chalii hamnazo aisee..,mtu anafikwa na tukio very serious like this then mijitu mingine inaleta hoja za kipumbavu.huenda tatizo ni mke wa mtu....maana hawa vijana..ni kama copy ya mwigulu.
Nadhani gongo imeshapanda kichwani, sio bure ni gongo tu.Mbinu chafu ya ccm kuendesha siasa kihuni wajipiga risasi wenyewe halafu wadai ni wapinzani.
Kwa hiyo matukio yote haya hapa chini wameyafanya CHADEMA na hawajachukuliwa hatua! TAFAKARI NDUGU KABLA YA KUPOST UJINGA HAPA JF.
1. Aliyemmwagia Tindikali Said Kubenea
2. Aliyemteka na kumtesa Dr. Ulimboka
3. Aliyemuua Mwangosi
4. Waliomuua kwa kumchinja Mwenyekiti wa CHADEMA kule Usariver
5. Wale vijana wa UVCCM waliowashambulia wabunge wa CHADEMA kule Mwanza
6. Waliomteka na kumtesa Kibanda
7. Waliomuwekea sumu Mwakyembe
8. Waliomgonga kwa makusudi Mwakyembe kwa lengo la Kumuua
9. Waliomuua yule Kada wa CHADEMA kule Igunga
10. waliolipua Bomu katika Mkutano wa CHADEMA pale Soweto
11. Waliolipua Kanisani Olasit, Yule kijana waliyemrundikia zile tuhuma sidhani kama ni mtuhumiwa halali.
12. Waliomuua Padri kule Zanzibar
13. Waliowamwagia Tindikali wale Mabinti wa UK
14. Waliomshambulia Dr. Mvungi hadi kusababisha kifo chake
15. waliomsababishi kifo Waziri wa fedha Mgimwa
16Waliowamwagia Tindikali yule Shehk na mtoto wake jana kule Arusha.
17. Waliowatuma akina Masogange kupeleka ile Sembe Kule South Africa na kuwasaidia kuififisha ile kesi na kugeuza madawa kutoka Heroin/Cocaine na kuwa PHENOBABITONE