Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Siku mbili baada ya waasi wa M23 kutangaza kusitisha mapigano dhidi ya vikosi vya serikali ya DRC kwa sababu za kibinadamu, kundi hilo limeuteka Mji wa Nyabibwe, Jimbo la Kivu Kusini.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, waasi hao wameudhibiti mji huo uliopo kando ya Ziwa Kivu, takriban kilometa 70 kutoka Bukavu—eneo ambalo awali walisema hawana mpango wa kuliteka.
Taarifa kutoka kwa vyanzo mbalimbali, ikiwemo wafanyakazi wa mashirika ya misaada, zimethibitisha kuwa M23 sasa wanashikilia udhibiti wa Nyabibwe.
Taarifa kutoka kwa vyanzo mbalimbali, ikiwemo wafanyakazi wa mashirika ya misaada, zimethibitisha kuwa M23 sasa wanashikilia udhibiti wa Nyabibwe.