M23 waliamsha tena DRC, Wauteka mji wa Nyabibwe, Jimbo la Kivu Kusini

M23 waliamsha tena DRC, Wauteka mji wa Nyabibwe, Jimbo la Kivu Kusini

hakuna jw kule, waliopo huko ni vijana wachache sana wanalinda amani kwa muavuli wa sadc. Ushushe jw kule si watapiga mpaka kigali?
Amani gani wanalinda wakati wanauwawa na kuiacha M23 ikizidi kujitanua na kuteka maeneo.
 
M23 ni JANGA la kimataifa
Siku mbili baada ya waasi wa M23 kutangaza kusitisha mapigano dhidi ya vikosi vya serikali ya DRC kwa sababu za kibinadamu, kundi hilo limeuteka Mji wa Nyabibwe, Jimbo la Kivu Kusini.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, waasi hao wameudhibiti mji huo uliopo kando ya Ziwa Kivu, takriban kilometa 70 kutoka Bukavu—eneo ambalo awali walisema hawana mpango wa kuliteka.

Taarifa kutoka kwa vyanzo mbalimbali, ikiwemo wafanyakazi wa mashirika ya misaada, zimethibitisha kuwa M23 sasa wanashikilia udhibiti wa Nyabibwe.
 
CCM ni janga wametuharibia nchi na jeshi pia. Cku hizi usalama wa TAIFA na JWTZ wanajazana UVCCM, unatarajia nini mkuu
Uhakika ni kuwa tusiponunua silaha Kali, na za kisiasa, na kurecruit vijana wazalendo na wenye ari na Akili kubwa jeshini siku moja haya manya Rwanda matutsi wapenda damu za watu na mali za bure watatutawala. Wameanza kupenyeza viongozi, na ni wepesi na werevu kutunga uongo kuhalalisha vita. Tatizo hatusomi vitabu au machapisho yanayotoa Siri zao. Serikali yetu iko busy na siasa na watawala kujilimbikizia mali ambazo siku hao mashetani wakiingia wanabomoa au kujitwalia. Mtikila alisema, japo inasemekana Kagame alimuua.
 
Nilisoma comment moja humu kuwa wamenyang'anywa simu zote ili wasifanye mawasiliano yoyote na wamepewa silaha zao kama heshima tu.
Unamnyang'anya vipi mali mwanajeshi anayelinda amani kwa mwamvuli wa UN maana yk utakuwa umetangaza vita na nchi wanachama wote wa UN na huwezi toboa hata wiki..

Mambo mengine fanyeni utafiti kwanza kwa namna mnavyoandika kimihemko hivyo mtu wa nje akisoma anajua ni jamii ya aina gani tunayo.
 
kuna rebels hata marekani, wao wanaitwa jina ingine.
48082767-0-image-a-35_1631994038199.jpg

Photo daily mail.

Wanaitwa militias

wazungu wa Marekani nao wamesheherekea kuachiwa kwa rebels wao kwa msamaha wa Raisi wao, wanaomuita dictator and tyrrant Donald Trump.

US President Donald Trump issued pardons or commutations for more than 1,500 people convicted or charged in connection with the US Capitol riot four years ago.

Fourteen members of the Proud Boys and Oath Keepers, two far-right groups, are among those whose sentences were commuted by the new Republican president as he took office on Monday.

BBC
 
Mgogoro huu ni mgumu! Afadhari hata Rais wa Malawi aliyeamua kuliondoa Jeshi lake DRC.
 
Siku mbili baada ya waasi wa M23 kutangaza kusitisha mapigano dhidi ya vikosi vya serikali ya DRC kwa sababu za kibinadamu, kundi hilo limeuteka Mji wa Nyabibwe, Jimbo la Kivu Kusini.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, waasi hao wameudhibiti mji huo uliopo kando ya Ziwa Kivu, takriban kilometa 70 kutoka Bukavu—eneo ambalo awali walisema hawana mpango wa kuliteka.

Taarifa kutoka kwa vyanzo mbalimbali, ikiwemo wafanyakazi wa mashirika ya misaada, zimethibitisha kuwa M23 sasa wanashikilia udhibiti wa Nyabibwe.

View: https://www.instagram.com/reel/DFvbBtHJuXG/?igsh=MW9zMmtsNnMycngxOA==
 
Unamnyang'anya vipi mali mwanajeshi anayelinda amani kwa mwamvuli wa UN maana yk utakuwa umetangaza vita na nchi wanachama wote wa UN na huwezi toboa hata wiki..

Mambo mengine fanyeni utafiti kwanza kwa namna mnavyoandika kimihemko hivyo mtu wa nje akisoma anajua ni jamii ya aina gani tunayo.
Taarifa ya kunyang'anywa simu iliandikwa na mmoja wa members humu. Usinilaumu mkuu. Kama ni kweli au sio, majibu yanatakiwa kutolewa kuhusu usalama wa askari wetu wanaolinda amani DRC.
 
Ni kiu ya msaada.

Kama mtoto anayenyanyaswa akimwona baba au mama yake.

Ila hawa ni waasi tunaoambiwa wengi wanyarwanda. Jamii ya Congo haiwataki....Wazalendo wamepigana pamoja na majeshi ya serikali.

Huu mgogoro haueleweki.....
Ina maana wanapigana kuikomboa Drc dhidi ya Tshekedi aliye mtawala katili?...hii kali
 
Back
Top Bottom