M23 waliamsha tena DRC, Wauteka mji wa Nyabibwe, Jimbo la Kivu Kusini

M23 waliamsha tena DRC, Wauteka mji wa Nyabibwe, Jimbo la Kivu Kusini

Siku mbili baada ya waasi wa M23 kutangaza kusitisha mapigano dhidi ya vikosi vya serikali ya DRC kwa sababu za kibinadamu, kundi hilo limeuteka Mji wa Nyabibwe, Jimbo la Kivu Kusini.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, waasi hao wameudhibiti mji huo uliopo kando ya Ziwa Kivu, takriban kilometa 70 kutoka Bukavu—eneo ambalo awali walisema hawana mpango wa kuliteka.

Taarifa kutoka kwa vyanzo mbalimbali, ikiwemo wafanyakazi wa mashirika ya misaada, zimethibitisha kuwa M23 sasa wanashikilia udhibiti wa Nyabibwe.
Niliwaambia hapa wanafanya-retreat watakuja kivingine maana paulo bado hajaridhika
 
Why are they being celebrated like this?

Are we being fed/misinformed (wrong information) about this guys? What for? Rebels are never celebrated like this?

View: https://youtu.be/ABkMQ8C-n7A?si=206_5odDdZCnnazv

Waaafrika wengi wakiona wanajeshi tu wanashangilia.

Wanajeshi wengi wanashangiliwa hivyo, hata Idi Amin.

Kipi kipya hapo?

Watanzania wengi wanapinga kuibiwa kura, wanasisitiza uhuru na utawala wa shwria, wakati huo huo wanamshobokea Captain Ibrahim Traore wa Burkina Faso!

Wakati Ibrahim Traore kaahirisha uchaguzi kwa miaka mitano tangu 2024!
 
Waaafrika wengi wakiona wanajeshi tu wanashangilia.

Wanajeshi wengi waneshangiliwa hivyo, hata Idi Amin.

Kipi kipya hapo?

Watanzania wengi wanapinga kuibiwa kura, wanasisitiza uhuru na utawala wa shwria, wakati huo huo wanamshobokea Captain Ibrahim Traore wa Burkina Faso!

Wakati Ibrahim Traore kaahirisha uchaguzi kwa miaka mitano tangu 2024!
Ni kiu ya msaada.

Kama mtoto anayenyanyaswa akimwona baba au mama yake.

Ila hawa ni waasi tunaoambiwa wengi wanyarwanda. Jamii ya Congo haiwataki....Wazalendo wamepigana pamoja na majeshi ya serikali.

Huu mgogoro haueleweki.....
 
Kuna jamaa mmoja alikuwa anahadithia mgogoro wa vita ya wenyewe kwa wenyewe ya kidini huko Lebanon.

Mgogoro ule ulihusisha mapigano kati ya wanajeshi wa Kikristo na wa Kiislamu.

Wananchi wa kijiji kimoja huko Lebanon walikuwa wanaangalia tu wanajeshi gani wamewafikia kijijini kwao.

Wakiona wanajeshi wa Kiislamu wanakuja, wanawalaki Kiislamu na kuwashangilia.

Wakiona wanajeshi wa Kikristo wameshinda na wanakuja kijijini kwao, wanawalaki Kikristo na kuwashangilia.

Kwa mtindo huo, wale wanajeshi wote waliwaona hao watu kuwa ni wafuasi wao, na hao wanakijiji wakasalimika hawakupigwa na jeshi lolote.

Hii ndiyo style sehemu nyingi Africa pia. Mwenye bunduki habishiwi.
 
Kuna sehemu nimesoma kuwa maelfu ya wanajeshi wa kulinda amani UN wameenda.
Ila nimesikitika sana, japo vita haina macho, kitendo cha kuwabaka na kuwachoma moto wakiwa hai, wafungwa wanawake zaidi ya 141 na watoto wao si sawa. Kila aliyeshiriki ghadhabu ya Mungu ikamshukie.
 
Siku mbili baada ya waasi wa M23 kutangaza kusitisha mapigano dhidi ya vikosi vya serikali ya DRC kwa sababu za kibinadamu, kundi hilo limeuteka Mji wa Nyabibwe, Jimbo la Kivu Kusini.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, waasi hao wameudhibiti mji huo uliopo kando ya Ziwa Kivu, takriban kilometa 70 kutoka Bukavu—eneo ambalo awali walisema hawana mpango wa kuliteka.

Taarifa kutoka kwa vyanzo mbalimbali, ikiwemo wafanyakazi wa mashirika ya misaada, zimethibitisha kuwa M23 sasa wanashikilia udhibiti wa Nyabibwe.
Linazidi kuisogelea Bukavu hili jeshi la Rwanda.
 
Kuna sehemu nimesoma kuwa maelfu ya wanajeshi wa kulinda amani UN wameenda.
Ila nimesikitika sana, japo vita haina macho, kitendo cha kuwabaka na kuwachoma moto wakowa hai, wafungwa wanawake zaidi ya 141 na watoto wao si sawa. Kila aliyeshiriki ghadhabu ya Mungu ikamshukie.
ICC imetangaza inafuatilia kwa karibu haya matukio, huenda kigogo mmoja wa nchi za maziwa makuu akatolewa hati ya kukamatwa kama kina Putin na Netanyau.
 
Back
Top Bottom