Ma brother wa miaka 35+ hebu tupeni wadogo zenu, ushauri wowote wa kuhusu maisha

Wewe tlatla ushauri wako naomba vijana waupuuze tu bwashee.
 
Dah ona Sasa ume kuja kujibu ujinga wako, we mwenyewe chawa
 
Umri wa miaka 18 mpaka ukomae kimapenzi ni wakati ngumu sana ; kati umri utashuhudia mtu unayempenda anaolewa na mwingine mpaka anapewa mimba 🤣, utashangaa binti unamfukuzia ofisini anakuja na mimba unaumia mpaka anakifungua...Yote ya yote mapenzi hayana furaha kwa dunia ya sasa .

Uchumi ,utakuja kushangaa kijana umri wako anatoboa ila wewe hauna kitu, kwenu pagumu hujafanya kitu ila wenzio wanapost wamewajengea wazazi wao.

Kiufupi, dunia ni ngumu sana nyakati hzi na inaendelea kuwa ngumu zaidi.
 
1. Suala la uchumi, aisee chagua Nuru au Giza. Mimi nilichagua Nuru hivyo nimeona mambo yakienda kupitia maombi japo kuna muda utaona ka Mungu amekusahau lkn itakua sauti ya chini moyoni ikisema endelea kuvumilia mi ndimi Mungu wako nitakusaidia.
2. Ishu ya mahusiano, hapa bwana uwe makini ngoma ipo na inaua na wengi wameukwaa. Nina mengi ya kuzungumza hapa ila niseme tu tundu utakaloingiza hakikisha mahali hapo umepima h.i.v au umevaa salama.
 
Unafikiri vina umri basi. Kikubwa pumzi.

Kina Mwijaku na Baba Levo wote ni 40 lakini mpaka leo wanatembea vitambi nje na kubusu makalio ya wanaume wenzao ili wale.

Usisubiri ufike umri fulani ndio uanze. Wewe ukipata fursa hata ukiwa na 18 tusua tu ila haimaanishi ukifika 35 huna muelekeo ndio umefeli.

Unaweza kuja kutusua na 50+.

Colonel Sanders katusia akiwa na miaka 65, leo hii mnaenjoy KFC wakati muanzilishi alisulubika na maisha mpaka kutoka kimaisha akiwa na 65 yrs.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…