Ma brother wa miaka 35+ hebu tupeni wadogo zenu, ushauri wowote wa kuhusu maisha

Duh hapa mbona ume hamasisha uzinzi tu mkuu?
 
Sidhani kama jinsi na umri vina uhusiano sana na swali lako. Naweza nisifit kwenye category mojawapo hapo ila naweza kukushauri hivi;

1. Acha kuamini bata za kwenye social media. Ukiona mtu amefanikiwa tambua anajituma na anatumia muda wake mwingi kutafuta or else hana chochote ni show-off tu au anauza ngada ambazo ni biashara ambayo si salama.
2. Uwe na uthubutu. Jaribu mara kadhaa na njia kadhaa. Katika hilo take calculated risks, siyo kila jambo ujaribu
3. Punguza matumizi, ishi kwa uwezo wako lakini usiridhike ulipofikia
4. Ukiwa umri wa kusoma, wewe soma, ukiachana na ajira, elimu inakuahidi kukufungua upeo na fursa
5. Hakuna kitu cha bure, usiamini matangazo ya kujiunga freemasonry au ibada za kukesha church day in day out. Mungu anasikia maombi hata katikati ya suughuli zako
6. Jenga uaminifu na watu, uhuni na udanganyifu utakutenga na fursa
7. Punguza ngono na starehe nyingine, zitakupotezea mwelekeo
8. Jali usafi wa mwili na chunga kauli zako, vyote hivyo huweza kuvuta au kufukuza fursa kupitia watu. Lakini pia uchafu hukaribisha maradhi na kuvuruga salio na muda wako wa kutafuta. Katika hilo pia lala muda wa kutosha kwa ajili ya afya ya mwili wako na akili
9. Usitegemee cha mtu. Acha kuwarubuni majimama au kutegemea sponsors kufikia malengo yako. Nao wana malengo yao kwako, so don't believe watabadilisha maisha yako kama unavyotarajia
10. Usisubiri, fanya sasa, ukiangua inuka uanze upya. Hakuna perfect timing na hakuna alarm katika hilo. The time is now!
11. Katika safari ya mafanikio yako, usiwe sababu mtu fulani analia au anajutia kufahamiana na wewe. Huzuni za wengine huondoa baraka na kukaribisha laana.
 
Ila sio. Siri Ata ukiachana na Instagram kila siku sisi tunaenda kwenye maduka yao kariakoo, uniambie eti wanafeki mkuu
 
Mabinti unaowazungumzia hapa ni pamoja na sisters wako, and your daughters. I am pretty sure si wanawake wote katika familia yako walioolewa, au wataolewa wakiwa mabikra.
 
Nimesoma post zote #174

Ni porojo tu mara achaeni pombe,bangi,kataa ndoa,usihonge.

halafu wenye 35+ ni wachache sana wengi ni manyoka wanacoment upuuzi tu.
 
Nimesoma post zote #174

Ni porojo tu mara achaeni pombe,bangi,kataa ndoa,usihonge.

halafu wenye 35+ ni wachache sana wengi ni manyoka wanacoment upuuzi tu.
Ebu tuambie harifu, wewe una points gani! Leta ukosoaji plus muono wako chief 🥶wtf are you talking about?
 
Duh hapa mbona ume hamasisha uzinzi tu mkuu?
kwasababu ndipo anguko kuu lilipo.Unataka nikwambie usifanye🤗🤗🤗🤗fanya ila fanya kama mtu mwenye kujitambua.

Ukishindwa jizuie of which wengi hawawezi kuhimili.So what next fanya ila kwa tahadhari na tahadhari nimekupa🤝

Gari ni irizi ya mjapani kunasia mademu.Kama hutaki kuwa unaongea sana miliki gari kama unauwezo, kama huna endelea kujitafuta.

Gari ni basic need ukishindwa kabisa miliki hata TERIOS KID.Kijigari kidogo na hakina gharama. Kwa kibongo bongo SOCIAL VALUE inaongezeka ukimiliki gari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…