Maadhimisho na Kilele cha Usomaji Quran kufanyika Siku ya Pasaka ni Dharau na Uchokozi kwa Wakristo au ni Utaratibu tu?

Kwani wewe unafikiri utawahitaji Waislamu siku hiyo ya pasaka uwakose?? Au wao wakifanya shughuli zao siku hiyo ya pasaka inaathiri vipi sherehe yako wewe ya pasaka?!
Bado sijawelewa malalamiko yako na ya Genta katika hili, dadavua zaidi.
 
Tutakuwa taifa la hovyo sana kama tutakuwa tunapeleka mambo hivi kwa kupetiana petiana, huku ni kuwa "snowflake"
 
Kwani Rais ni Mkristo mpaka aende kwenye misa ya pasaka?? Kwa hiyo kukiwa na sikukuu ya ibada ya Ng'ombe ya Wahindi aende huko pia??
Yaani siku ya Pasaka msome Qur'an kwa nini siku hiyo Rais asiende kwenye Misa ya Pasaka
 
Hii ni secular country na Wakatoliki pombe sio dhambi kwao.
 
Usomaji Quran sio kwa ajili ya watu wote na pia Pasaka sio kwa ajili ya watu wote.
 
Siku Kuu yetu Muhimu na Kubwa ya Pasaka ( Kufufuka kwa Mkombozi Wetu ) Yesu Kristo.
Waisrael wanasema hawamtambui Yesu Kristu na walitaka kupitisha sheria yeyote anaezingumzia kuhusu Yesu apigwe kifungo gerezani, hii imekaaje ?
 
Mkuu usiwe na wasiwasi! Tutasherehekea Pasaka kama kawaida.
 
Kuna ni waongo hata shetani anakaa pembeni, Yaani haya ulivyoandika utadhani unajua hizo siku za Waislamu vizur kuliko wao. Yaani kila Sikukuu yenu wao nao wana Sikukuu? Je nyinyi mlikatazwa kupita huko mitaani au mlinyimwa haki kabisa ya kufunga mitaa? Hivi siku ya Eid ikiangukia Jpili au Ijumaa kuu mtaacha kwenda kufanya Ibada zenu ili muwapishe Waislamu washerehekee?
Waislamu kila siku ni Ibada na ujue kwa siku Waislamu wana swala 5 za lazima na sio uchaguzi wa kuamua kupisha mambo mengine.
Kwa kifupi wewe ndio ulikuwa unataka mashindano wakati wenzako wapo busy na Ibada zao.
 
kwa andiko lipi kuwa pasaka ni ya wakristo mkuu
Mathayo 26
1 Ikawa Yesu alipomaliza maneno hayo yote, aliwaambia wanafunzi wake,

2 Mnajua ya kuwa baada ya siku mbili itakuwa Pasaka, na Mwana wa Adamu atasalitiwa asulibiwe.

3 Wakati ule wakuu wa makuhani, na wazee wa watu, wakakusanyika katika behewa ya Kuhani Mkuu, jina lake Kayafa;

4 wakafanya shauri pamoja, ili wamkamate Yesu kwa hila na kumwua.

5 Lakini wakasema, Isiwe wakati wa sikukuu, isije ikatokea ghasia katika watu.

6 Naye Yesu alipokuwapo Bethania katika nyumba ya Simoni mkoma,

7 mwanamke mwenye kibweta cha marhamu ya thamani kubwa alimkaribia akaimimina kichwani pake alipoketi chakulani.

8 Wanafunzi wake walipoona, wakachukiwa, wakasema, Ni wa nini upotevu huu?

9 Maana marhamu hii ingaliweza kuuzwa kwa fedha nyingi wakapewa maskini.

10 Yesu akatambua akawaambia, Mbona mnamtaabisha mwanamke? Maana ni kazi njema aliyonitendea mimi.

11 Kwa maana siku zote mnao maskini pamoja nanyi; lakini mimi hamnami siku zote.

12 Maana kwa kunimwagia mwili wangu marhamu hiyo, ametenda hivyo ili kuniweka tayari kwa maziko yangu.

13 Amin, nawaambieni, Kila patakapohubiriwa Injili hii katika ulimwengu wote, tendo hilo alilolitenda huyu litatajwa pia kwa kumbukumbu lake.

14 Wakati huo mmoja wa wale Thenashara, jina lake Yuda Iskariote, aliwaendea wakuu wa makuhani,

15 akasema, Ni nini mtakachonipa, nami nitamsaliti kwenu? Wakampimia vipande thelathini vya fedha.

16 Tokea wakati huo akawa akitafuta nafasi apate kumsaliti.

17 Hata siku ya kwanza ya mikate isiyotiwa chachu, wanafunzi wake wakamwendea Yesu, wakamwambia, Ni wapi utakapo tukuandalie uile Pasaka?

18 Akasema, Enendeni mjini kwa mtu fulani, mkamwambie, Mwalimu asema, Majira yangu ni karibu; kwako nitafanya Pasaka pamoja na wanafunzi wangu.

19 Wanafunzi wakafanya kama Yesu alivyowaagiza, wakaiandaa Pasaka.

20 Basi kulipokuwa jioni aliketi chakulani pamoja na wale Thenashara.

21 Nao walipokuwa wakila, alisema, Amin, nawaambia, Mmoja wenu atanisaliti.

22 Wakahuzunika sana, wakaanza kumwuliza mmoja mmoja, Ni mimi, Bwana?

23 Akajibu akasema, Yeye aliyetia mkono wake pamoja nami katika kombe, ndiye atakayenisaliti.

24 Mwana wa Adamu aenda zake, kama alivyoandikiwa; lakini ole wake mtu yule ambaye amsaliti Mwana wa Adamu! Ingekuwa heri kwake mtu yule kama asingalizaliwa.

25 Yuda, yule mwenye kumsaliti, akajibu, akasema, Ni mimi, Rabi? Akamwambia, Wewe umesema.

26 Nao walipokuwa wakila Yesu alitwaa mkate, akabariki, akaumega, akawapa wanafunzi wake, akasema, Twaeni, mle; huu ndio mwili wangu

27 Akakitwaa kikombe, akashukuru, akawapa, akisema, Nyweni nyote katika hiki;

28 kwa maana hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi.

29 Lakini nawaambieni, Sitakunywa kabisa tangu sasa uzao huu wa mzabibu, hata siku ile nitakapokunywa mpya pamoja nanyi katika ufalme wa Baba yangu.

30 Nao walipokwisha kuimba, wakatoka nje kwenda mlima wa Mizeituni.

31 Ndipo Yesu akawaambia, Ninyi nyote mtachukizwa kwa ajili yangu usiku huu kwa kuwa imeandikwa, Nitampiga mchungaji, na kondoo wa kundi watatawanyika.

32 Lakini baada ya kufufuka kwangu, nitawatangulia kwenda Galilaya.

33 Petro akajibu, akamwambia, Wajapochukizwa wote kwa ajili yako, mimi sitachukizwa kamwe.

34 Yesu akamwambia, Amin, nakuambia wewe, usiku huu kabla ya kuwika jogoo, utanikana mara tatu.

35 Petro akamwambia, Ijaponipasa kufa nawe, sitakukana kamwe. Na wanafunzi wote wakasema vivyo hivyo.

36 Kisha Yesu akaenda pamoja nao mpaka bustani iitwayo Gethsemane, akawaambia wanafunzi wake, Ketini hapa, hata niende kule nikaombe.

37 Akamchukua Petro na wale wana wawili wa Zebedayo, akaanza kuhuzunika na kusononeka.

38 Ndipo akawaambia, Roho yangu ina huzuni nyingi kiasi cha kufa; kaeni hapa, mkeshe pamoja nami.

39 Akaendelea mbele kidogo, akaanguka kifulifuli, akaomba, akisema, Baba yangu, ikiwezekana, kikombe hiki kiniepuke; walakini si kama nitakavyo mimi, bali kama utakavyo wewe.

40 Akawajia wale wanafunzi, akawakuta wamelala, akamwambia Petro, Je! Hamkuweza kukesha pamoja nami hata saa moja?

41 Kesheni, mwombe, msije mkaingia majaribuni; roho i radhi, lakini mwili ni dhaifu.

42 Akaenda tena mara ya pili, akaomba, akisema, Baba yangu, ikiwa haiwezekani kikombe hiki kiniepuke nisipokunywa, mapenzi yako yatimizwe.

43 Akaja tena, akawakuta wamelala; maana macho yao yamekuwa mazito.

44 Akawaacha tena, akaenda, akaomba mara ya tatu, akisema maneno yale yale.

45 Kisha akawajia wanafunzi wake, akawaambia, Laleni sasa, mpumzike tazama, saa imekaribia, na Mwana wa Adamu anatiwa katika mikono ya wenye dhambi.

46 Ondokeni, twende zetuni! Tazama, yule anayenisaliti amekaribia.

47 Basi alipokuwa katika kusema, tazama, Yuda, mmoja wa wale Thenashara akaja, na pamoja naye kundi kubwa wenye panga na marungu, wametoka kwa wakuu wa makuhani na wazee wa watu.

48 Na yule mwenye kumsaliti alikuwa amewapa ishara, akisema, Nitakayembusu, huyo ndiye; mkamateni.

49 Mara akamwendea Yesu, akasema, Salamu, Rabi, akambusu.

50 Yesu akamwambia, Rafiki, fanya ulilolijia. Wakaenda, wakanyosha mikono yao wakamkamata Yesu.

51 Na tazama, mmoja wao waliokuwa pamoja na Yesu akanyosha mkono wake, akaufuta upanga wake, akampiga mtumwa wa Kuhani Mkuu, akamkata sikio.

52 Ndipo Yesu akamwambia, Rudisha upanga wako mahali pake, maana wote waushikao upanga, wataangamia kwa upanga.

53 Ama wadhani ya kuwa mimi siwezi kumsihi Baba yangu, naye ataniletea sasa hivi zaidi ya majeshi kumi na mawili ya malaika?

54 Yatatimizwaje basi maandiko, ya kwamba hivyo ndivyo vilivyopasa kujiri?

55 Saa ile Yesu akawaambia makutano, Je, mmetoka kama kumkamata mnyang'anyi, wenye panga na marungu, ili kunishika? Kila siku naliketi hekaluni nikifundisha, msinikamate.

56 Lakini haya yote yamekuwa, ili maandiko ya manabii yatimizwe. Ndipo wanafunzi wote wakamwacha, wakakimbia.

57 Nao waliomkamata Yesu wakampeleka kwa Kayafa, Kuhani Mkuu, walikokuwa wamekutanika waandishi na wazee.

58 Na Petro akamfuata kwa mbali mpaka behewa ya Kuhani Mkuu, akaingia ndani, akaketi pamoja na watumishi, auone mwisho.

59 Basi wakuu wa makuhani na baraza yote wakatafuta ushuhuda wa uongo juu ya Yesu, wapate kumwua;

60 wasiuone wangawa walitokea mashahidi wa uongo wengi.

61 Hata baadaye wawili wakatokea, wakasema, Huyu alisema, Naweza kulivunja hekalu la Mungu, na kulijenga kwa siku tatu.

62 Kisha Kuhani Mkuu akasimama akamwambia, Hujibu neno? Hawa wanakushuhudia nini?

63 Lakini, Yesu akanyamaza. Kuhani Mkuu akamwambia, Nakuapisha kwa Mungu aliye hai, utuambie kama wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu.

64 Yesu akamwambia, Wewe umesema; lakini nawaambieni, Tangu sasa mtamwona Mwana wa Adamu ameketi mkono wa kuume wa nguvu, akija juu ya mawingu ya mbinguni.

65 Ndipo Kuhani Mkuu akararua mavazi yake, akisema, Amekufuru; mna haja gani tena ya mashahidi? Tazameni, sasa mmesikia hiyo kufuru yake;

66 mwaonaje ninyi? Wakajibu, wakasema, Imempasa kuuawa.

67 Ndipo wakamtemea mate ya uso, wakampiga makonde; wengine wakampiga makofi,

68 wakisema, Ewe Kristo, tufumbulie; ni nani aliyekupiga?

69 Na Petro alikuwa ameketi nje behewani; kijakazi mmoja akamwendea, akasema, Wewe nawe ulikuwapo pamoja na Yesu wa Galilaya.

70 Akakana mbele ya wote, akisema, Sijui usemalo.

71 Naye alipotoka nje hata ukumbini, mwanamke mwingine alimwona, akawaambia watu waliokuwako huko, Huyu alikuwapo pamoja na Yesu Mnazareti.

72 Akakana tena kwa kiapo, Simjui mtu huyu.

73 Punde kidogo, wale waliohudhuria wakamwendea, wakamwambia Petro, Hakika wewe nawe u mmoja wao; kwa sababu hata usemi wako wakutambulisha.

74 Ndipo akaanza kulaani na kuapa akisema, Simjui mtu huyu. Na mara akawika jogoo.

75 Petro akalikumbuka lile neno la Yesu alilolisema, Kabla ya kuwika jogoo, utanikana mara tatu. Akatoka nje, akalia kwa majonzi.
 
Kiongozi, ina maana hufaham simple logic inayotumika kupanga maadhimisho ya kitaifa? shame!
Labda nikuulize; Sherehe ya Wakristo na sherehe ya Waislam vina uhusiano gani?
Namaanisha hata ukitofautisha tarehe; Wakristo hawataenda kwa Waislam na Waislam hawataenda kwa wakristo. Hicho ndio kigezo muhimu kinacho angaliwa wakati wa kupitisha tarehe
 
Imani ni matendo na wala sio fikra na mtazamo. Pasaka ipo palepale na shughuli za waislamu zitaendaelea vyema.

Ubarikiwe GENTAMYCIME
 
Niujinga mkubwa, kumbagua, mtanzania kisa ya dini hizi. Zilizoletwa na wazungu kwa njia ya ukoloni, pia kama kunawatu wa namna hii, kunautumwa mkubwa sana unaendelea kwa wajinga.
 
Usomaji Quran sio kwa ajili ya watu wote na pia Pasaka sio kwa ajili ya watu wote.


Angalia gist ya ninachosema; Pasaka ni sikukuu ya kuadhimisha kufufuka kwa Yesu, Yesu kwa imani ya wakristo ni mkombozi wa ulimwengu WOTE hivyo pasaka inakuwa automatically ni siku inayohusikana na mkombozi wa watu wote yaani Yesu, kwa imani ya Wakristo, yeye yupo kwa ajili ya watu wote japokuwa mimi au wewe hatuamini jambo hilo.

Qur'an tukufu nacho ni Muongozo kwa watu WOTE, yaani inaposomwa Qur'an wanaotakiwa waisikilize ni watu WOTE na kwa kuisikiliza Qur'an mtu Yeyote anapata rehema japokuwa wapo watu wanaopinga jambo hilo.

Sasa kwa upande wa Wakristo na upande wa Waisilamu katika suala la Sherehe ya Pasaka na Usomaji wa Qur'an tunayo "Common ground" nayo ni kumkomboa Mwanadamu kiroho na kimwili sasa itakuwa ni ujinga kuanza kuvutana bila sababu katika kitu ambacho "we share the same common ground". Kwa kitu ambacho kinaweza kuleta mfarakano na mapambano yasiyo ya lazima katika jamii moja ya Wtz then why not compromise??

Huyo mleta mleta mada angejenga hoja katika msingi huo wa "the same common ground" hapo angeeleweka vinginevyo kila dini inao utaratibu wa kufanya mambo yake ndani ya sheria bila kuingiliwa na mtu yeyote.
 
Leo umeandika kwa hekima sana sio kama yule niliemzoea
 
Usijisumbue kishachakachuliwa hiki kitabu. Kwanza Yesu hakukabidhiwa bibilia. Nyinyi bibilia mmeitoa wapi?
 
Nikija kufhaulu kuwa, raisi wa nchi, hii, mimi nafuta dini zote, hapa tanzania, dini ni unafiki tu, wanabaki waganga wa kienyeji tu,!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…