Maadhimisho ya miaka 60 ya muungano na idadi ndogo ya mahudhurio uwanjani, nini tatizo?

Maadhimisho ya miaka 60 ya muungano na idadi ndogo ya mahudhurio uwanjani, nini tatizo?

Nao katika majukwaa wamejaa watu katika uniforms na track suits kuliko wananchi raia wa kawaida.
• Hao wa track suits na uniforms wameenda kwa kumlazimishwa tu, ili kuulindda ugali wao...

• Hii Niliona toka mda hasa pale account ya msemaji wa serikali kufanya promotion ya viongozi wa kuu wa nchi tofauti kuwa watafika kwenye hiyo kasheshe iliyopooza.
 
Wakuu natizama maadhimisho ya muungano, idadi ya watu mpaka Sasa ni ndogo mno kulingana tukio lenyewe. Je, ni uwepo wa mvua ama ni watanganyika kutokuona umuhimu wa tukio lenyewe na kukatishwa tamaa na jinsi mambo yanavyoendeshwa nchini?

Maoni yenu wakuu.
Kwa Leo nimewakubali Watanganyika. Kama hawatageuka tunaelekea pazuri. Muungano wa viongozi ubaki Kwa viongozi.
 
Wakuu natizama maadhimisho ya muungano, idadi ya watu mpaka Sasa ni ndogo mno kulingana tukio lenyewe. Je, ni uwepo wa mvua ama ni watanganyika kutokuona umuhimu wa tukio lenyewe na kukatishwa tamaa na jinsi mambo yanavyoendeshwa nchini?

Maoni yenu wakuu.
Ukiona hivyo ujue hela ya kuhonga makundi mbalimbali kuhudhuria ilikuwa ndogo.
 
Unadhani Diamond Platinum angekuwepo Uhuru Leo wamachinga wangeogopa mvua kuja uwanjani?

Wasanii ni hamasa tuwatumie inapobidi

Ahsanteni Sana 🐼
Kwahiyo wananchi wanamuelewa diamond zaidi kuliko muungano?
 
Wakuu natizama maadhimisho ya muungano, idadi ya watu mpaka Sasa ni ndogo mno kulingana tukio lenyewe. Je, ni uwepo wa mvua ama ni watanganyika kutokuona umuhimu wa tukio lenyewe na kukatishwa tamaa na jinsi mambo yanavyoendeshwa nchini?

Maoni yenu wakuu.

Mpaka aibu. Ingekuwa ni Mkutano wa CCM wangepeleka Maroli kusomba watu ...... ila kwenye hili hawana shida.

Ila ni aibu sana. Wamealika Viongozi kibao halafu wameshindwa kuwahamasisha wananchi kwenda kwenye sherehe.
 
Mama.hana mvuto kwa raia.
Maisha yamekuwa magumu sana.
Mvua sio kisingizio, watu wa temeke tu wangeweza kujaza huo uwanja na hakuna hiyo mvua huku zaidi ya vinyunyu.
Angalia kesho Yanga anacheza chamazi uwanja utakavyojaa.
Mama machawa wanamdanganya kuwa añapendwa ila sio kweli.
Amechokwa haraka sana, km atataka kugombea 2025 ajitafakari kwanza.
Kuna uwezekano wananchi wakagomea uchaguzi, watajitokeza wachache sana kushiriki zoezi la uchaguzi.
Mbaya zaidi upinzani nao unapumulia mashine.
IMG-20240426-WA0006.jpg
 
Wakuu natizama maadhimisho ya muungano, idadi ya watu mpaka Sasa ni ndogo mno kulingana tukio lenyewe. Je, ni uwepo wa mvua ama ni watanganyika kutokuona umuhimu wa tukio lenyewe na kukatishwa tamaa na jinsi mambo yanavyoendeshwa nchini?

Maoni yenu wakuu.
Watu wamechoka. Hizo fedha za sherehe zinafujwa nchi ina mahitaji kibao zingepekwa kuboresha reli ya ruvu, Moshi, Arusha
 
Habari bila picha Dunia ya sasa au video clip sw na takataka TU
 
Maisha yamebadilika sana
Zamani ilikuwa lazima kwenda uwanjani kila sehemu tz, tena na biashara zote zinafungwa kabisa

Ngoma na makelele ya kutosha
 
Watu kwenda huko tu ni maumivu
Kunyeshewa na mvua,usafiri mmbovu...tabu yote ya nini
Wawape hao hao wasanii na machawa hela

Ova
 
wewe ndio mjuaji na mshamba. Hapa maeneo ya selassie kukavu na hiyo mvua si mvua ya kusema watu washindwe kutoka . Sema hakuna msukumo wa watu kwanini aende huko . Unafikiri simba na yanga mvua ingekuwa inanyesh uwanja ungeacha kujaa? Uwe unaacha ujuaji wa kijinga. Achana tu na mtaa wa makaburini hao wanaoishi huo mtaa unaotazamana na uwanja wa taifa watu wamelala ndani na geti la uwanja analiona.
Wacha kusema watu wameshindwa kwenda sababu ya mvua sema Hakuna anayeleewa hicho kitu ni nini. Hata wengi walioingia mule mbali na wanafunzi kubebwa t hata watu wazima hawawezi kukuelezea huo muungano
Watu wajue, hicho siyo kipaombele tena! Mbona watu wametoka kuingia kazini kama kawa?

Daladala zilikuwa zinapiga kazi kama kawaida
 
Ubaguzi siyo mzuri, tukianza kuwekeana ubaguzi huyu siyo hatutaishia hapo tukimaliza kundi moja tutaona haitoshi tutaanza kuwabagua makundi mengine.

Marekani kuna kila aina ya wamarekani wenye nasaba tofauti na wote wanahesabika ni waMarekani.

Dola madhubuti kama USA, China, Russia n.k haziangalii rangi ya mtu wote ni raia na kwa pamoja wanasonga mbele kwa kadri ya kipawa walichopewa kila raia.
Acha ujinga wako hii ni Ya waafrika weusi hao wahindi, waarabu na wazungu ndio waliua Babu zetu na kuwafanya mateka miaka na miaka Leo watutungie jina la nchi yetu huo si ukichaa!

Kuongea uhalisia sio ubaguzi. Uhalisia ni kuwa Babu zetu waliteswa na hao watu.
 
Hold on.! unaonekana unauelewa hafifu sana.
Hapa tunazungumzia upungufu wa watu uwanjani. Hoja yangu ni sababu ya mvua.
Watanzania wameanza lini kutoelewa Muungano mpaka ije ghafla leo wasiende? Tangia miaka mingi watu hawaelewi huu Muungano lakini haiwazuii kwenda uwanjani.

Sababu ya mvua hata mtoto mdogo anaweza kujua kwakua ni week sasa mvua inanyesha kubwa na kuzua taharuki mtaani.

Wewe kama unaishi mtaa wa uwanja wa Taifa inahusika vipi? acha ujinga kijana leta hoja.
Huu muungano ni muda mrefu watu hawauelewi si Bara sio visiwani ila haijawahi zuia watu kwenda uwanjani labda ulete sababu nyingine naweza kukuelewa.
Mbona shindano la kusoma Quran mwezi Jana limejaza Uwanja Hadi pomoni


Mbona mechi ya mamelody na yanga ilijaa licha ya mvua


Mbona mechi ya Simba 1 yanga 5 ilijaa licha ya mvua kuwa kubwa
 
Wakuu natizama maadhimisho ya muungano, idadi ya watu mpaka Sasa ni ndogo mno kulingana tukio lenyewe. Je, ni uwepo wa mvua ama ni watanganyika kutokuona umuhimu wa tukio lenyewe na kukatishwa tamaa na jinsi mambo yanavyoendeshwa nchini?

Maoni yenu wakuu.
Hapo kuna watu wanalipwa Sitiing allowance, huku Raia wakienda kuuza tu sura pale.
 
Babu zetu waliteswa

Kuna wengine makabila ya waafrika hawakuteswa wala kupelekwa utumwani. Na waliishii na wanaendelea kuishi Afrika.

Acha kukariri mfano Wahaya wa dola ya Baganda- Bunyoro, Wachaga chini ya Mangi Meli , Wanyakyusa, Machinga chini ya Mfalme Alei(Ali)waLunga.. wa Lindi. n.k ni baadhi ya makabila ambayo hayakuchukuliwa utumwani ni wale wanyonge walikamatwa na makabila mengine kisha kuuzwa utumwani na wenzao kwa waarabu na wazungu pia waafrika wa makabila mengine walijipeleka utumwani Wazigua wa Tanga walienda Somalia na miaka hii waafrika wanavuka wenyewe bahari ya Mediterranean na pori la Darién Gap kule Marekani ya Kati kwenda Marekani na Canada :


Toka maktaba:

Simulizi za Mjukuu wa Mfalme Mlinganaweka AleiwaLunga wa maeneo ya Wamachinga Pwani aliyekuwa na watumwa
Tanzania

Simulizi za wazee wetu : Waasisi wa madhehebu ya Ma- Shia nchini Tanzania na kwanini dhehebu la Shia lina kanuni la kukubali vijana wao kuuliza maswali (tabligh) wakati Sunni hukataza vijana wao kuuliza maswali na kulazimishwa kuwa mkubwa ktk imani yaani sheikh / Imamu / Maalim akisema basi yeye ndiye anafahamu ilm yote ya dini

(NZIMA)-SIMULIZI YA MAREHEMU SHEIKH ABDALLAH SEIF (1939 -2020) - HISTORIA YETU part 1



KIU YA ILMU, SHEIKH ABDALLAH SEIF ILIMPELEKEA KUSOMA KWA MIAKA 11 MFULILIZO KATIKA NCHI ZA IRAQ, LEBANON NA IRAN (1968-1979)

Sheikh Abdallah Seif Linganaweka anatujuza kuwa Wenyeji wa Lindi jina Lao la asili ni Wakudewe kwa sasa almaaruf wanafahamika kama waMachinga wa pwani ya Lindi.

Babu yake Babu Abdallah Seif alikuwa mfalme Mlinganaweka AleiwaLunga mwenye watumwa baada ya kuwazidi wanyonge majirani kuja kuwatumikisha kujaza vyakula. Mfalme Alei(Ali)waLunga.. wa Lindi.

Baada ya kuja mkoloni Muingereza nchini Tanganyika, aliua ufalme na kubakiza uchifu. Sehemu za pwani ziliathirika kwanza kwa kupoteza ufalme mapema kabla ya watu wa bara.. Pwani wakabakia na usheikh na uchifu... usiokuwa na nguvu kama falme za asili za maeneo yao Lindi / Kilwa kabla ya kuja ukoloni...

Sheikh MbogaBure mjuzi wa lugha ya Kiarabu, dini pia mmoja wa waanzilishi wa madhehebu ya Shia Tanzania amuunganisha Mzee Abdallah Seif kupata scholarship kwenda Baghdad, Iraq mwaka 1968 kusoma zaidi dini...

Kijana Abdallah Seif mwaka 1968 alipokwenda Kijijini ashutumiwa kupotea kwa kuukumbatia u-Shia mojawapo ya madhehebu ya dini ya KiIslamu, wakati wengine wote ni Sunni. Lakini babu yake msomi wa dini madhehebu wa Sunni anayetambulika Lindi na Kilwa hakuwa anatoa shutma zozote alikuwa msikivu na kumtia moyo Abdallah Seif asome zaidi na ili kuifahamu dini vizuri zaidi.

Kilichomsukuma Sheikh Abdallah Seif kuvutiwa na u-Shia ni namna masheikh wa ki-Shia walivyokuwa wazi (tabligh) kukaribisha maswali tofauti na madhehebu mengine ya KiIslam ambapo kijana hakuruhusiwa kuhoji na pia kuuliza maswali ilikuwa inachukuliwa ni utovu wa nidhamu kwa waalimu au masheikh wake.

Safari ya Sheikh Abdallah Seif wenzie vijana wakiwemo kina Sheikh Isihaka Pingili kwenda Iraq kwa meli iliwachukua mwezi mzima kupitia bandari mbalimbali za Zanzibar, Tanga, Mogadishu, Bahrain na kuishia Basra nchini Iraq na kutua katika chuo cha Hawza mji wa Najaf Iraq

Ujio wao Basra, Iraq ulileta tafrani kwa mwenyeji wao Mpakistani mfanyabiashara mkubwa nchini Iraq enzi hizo na kupelekea Saadam Hussein kumshutumu mfanyabiashara huyo tajwa kuleta majasusi wa kiAfrika ikumbukwe ndiyo kwanza Saddam Hussein na chama chake cha Baath walikuwa wanajaribu kushika hatamu za kuongoza nchi baada ya mapinduzi nchini Iraq. Mpakistani huyo alinyongwa mwaka 1969 pamoja na wafadhili wengine kama kuna Bakri Sadr waliowezesha ujio wa vijana wa kiAfrika kuingia Iraq kwa dhumuni la kusoma dini.

Kutokana na hilo ikabidi Sheikh Abdallah Seif, Sheikh Isihaka Pingili na vijana wengine wa kiAfrika waondoke Iraq mwaka 1970 kwenda Lebanon kwenda kuendelea na azma yao ya kusoma dini.

Sheikh Abdallah Seif wakakaa Lebanon kuanzia mwaka 1970 mpaka 1978 ambapo mara nyingine masomo ya dini yakaingia changamoto baada ya vita baina ya Wapaletina waliokuwa kambi za ukimbizi Lebanon na waLebanon wenye nchi na kuzua vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Mwaka 1978 Ikabidi Sheikh Abdallah Seif na wenzie wahamie nchi ya jirani ya Iran kwenda katika mji wa Qom city kuendelea na masomo yao ya dini. Iran ilikuwa imetulia nchi ya amani chini ya utawala wa mfalme (Shah) Mohammed Reza Pahlavi Historic Personalities of Iran: Mohammad Reza Shah Pahlavi miaka 7 waliakaa Iran wakiendelea kusomeshwa.

Wakati wa likizo Iran wengine wenda Ufaransa kuchuma zabibu mashambani au kufanya kazi sehemu za utalii wa ndani wa Iran au kuchukua mabusati ya kushona ya Iran yanayosifika Uarabuni kote kwenda kuyauza ktk nchi mbalimbali za Arabuni ndivyo mwanafunzi kama Sheikh Abdallah Seif na wenzie vijana walivyojiongezea fedha za kujikimu na kupeleka kiasi cha pesa nyumbani Tanzania.

Hatimaye mwaka 1980 baada ya kusoma kwa miaka 11 nje ya Tanzania ,walitunikiwa shahada ya baccalauréat ya masomo ya dini na kurejea Tanzania. Kwa miaka hiyo 11 ughaibuni pia waliweza kusoma elimu ya secular kiwango cha sekondari kwa njia ya posta masomo ya nchi ya Uingereza kwa msaada mkubwa wa swahiba wa kiongozi wa kijeshi wa Nigeria Jenerali Yakubu Gowon. Swahiba huyo alikuwa mfanyabishara wa vituo vya mafuta na makazi yake Uingereza.

Mahojiano haya yanakuja kwa hisani kubwa ya Ammar Dachi aliyemshawishi Mzee Abdallah Seif kufunguka historia ya mapito yake, ukoo , ilmu na utafiti wa mafuta 1955 na pia ujio wa madhehebu ya Shia nchini Tanzania


HISTORIA YA ABDALLAH SEIF (1939 -2020) Part - 2



Sheikh Alhaj Sheikh Abdallah Seif Linganaweka mzaliwa na mwenyeji wa kijiji cha Mnan’gole sehemu za Dimba mkoa Lindi Tanzania anaendelea kusimulia kazi kubwa aliyofanya ya kujitolea ya kueneza dini.

Sheikh Abdallah Seif anasisitiza umuhimu wa ilmu na elimu kwa wanazuoni wote wa KiIslamu.

Anasema ili sheikh awe mwanazuoni aliyekamilika kufundisha chuoni lazima kusoma ilmu ya dini kwa angalau miaka 15.

Anakumbuka alivyokuwa mjini Qom Iran akisoma chuoni alionana na wazee wenye umri wa miaka 70 wakijiendeleza na kuwaambia wao vijana kuwa inahitajika jumla ya miaka 35 ili kuielewa dini nje ndani kwa ufasaha. Wazee hao walicheka waliposikia vijana Sheikh Abdallah Seif, Sheikh Isihaka Pingili na vijana wengine toka Afrika wakisema wanataka kusoma dini kwa miaka 5 mpaka 10 tu ilihali wametoka Afrika na kuwaambia bila kupepesa macho kuwa ili wawe wabobevu wafikirie miaka angalau 15 ya ilmu ya dini ngazi ya chuo.

Hivyo akiwa amepikika kwa elimu tosha ya kidini baada ya kufanya kazi kwa takriban miaka 11 nchini Tanzania, mwaka 1990 sheikh Abdallah Seifu alikwenda Nampula jimbo la Cabo Delgado nchini Mozambique kufanya kazi ya dini.

Kisha sheikh Abdallah Seif alishuka mpaka mji mkuu wa Maputo Mozambique na alisaidia kufungua taasisi rasmi inayotambulika na serikali na kupewa leseni iliyosajiliwa Maputo Mozambique kwa ajili ya taasisi ya Shia Ithna-Asheri Muzdalifah . Sheikh Abdallah Seif anazungumza lugha za Kiswahili, Kiarabu, Kiingereza na Kireno.

Source : Asadiqmedia

RAMBIRAMBI NA WASIFU - Marhum Sheikh Abdallah Seif



Source : Asadiqmedia
 
Back
Top Bottom