Maadhimisho ya miaka 60 ya muungano na idadi ndogo ya mahudhurio uwanjani, nini tatizo?

wewe ndio mjuaji na mshamba. Hapa maeneo ya selassie kukavu na hiyo mvua si mvua ya kusema watu washindwe kutoka . Sema hakuna msukumo wa watu kwanini aende huko . Unafikiri simba na yanga mvua ingekuwa inanyesh uwanja ungeacha kujaa? Uwe unaacha ujuaji wa kijinga. Achana tu na mtaa wa makaburini hao wanaoishi huo mtaa unaotazamana na uwanja wa taifa watu wamelala ndani na geti la uwanja analiona.
Wacha kusema watu wameshindwa kwenda sababu ya mvua sema Hakuna anayeleewa hicho kitu ni nini. Hata wengi walioingia mule mbali na wanafunzi kubebwa t hata watu wazima hawawezi kukuelezea huo muungano
Huo mtaa wenu wa Selassie labda ni wachawi watupu, haiwezekani mji mzima maji yamejaa kwenu nyie kukavu.

Mechi ya Yanga juzi wamecheza JKT kule uliona watu walio hudhuria? Matawi ya Yanga tu hata ma 5 sidhani yalifika na mechi ni Dar hapa hapa sababu nini unadhani?
Mitaani maji yamejaa bado unataka watu wajazane ili iweje?
 
1.Muungano hauna faida kwa yeyote kwa mwananchi wa kawaida,so why attend,binafsi sioni faida.
2.Nchi imekuwa ya watu wachache, wananchi wa kaida wametengwa,so wanaofaidi nchi waende.
3.Nchi kwa sasa ni captured na dark forces na viongozi ni collaborators,so why support them.
4.Viongozi hawajali maslahi ya mwananchi wa kawaida,kwa hiyo waendelee wenyewe.
5.Kila eneo ambalo lingekuwa la manufaa kwa mwananchi wa kawaida viongozi wanalihujumu kwa kuiba fedha za miradi.Kwa mfano miradi ya upatikanaji wa umeme,maji,kilimo, elimu,miundo mbinu etc.Watu wanaiba pesa za miradi,CAG anatoa ripoti,kwa hiyo wezi wanafahamika,no action is taken.It would be stupid to support such a corrupt government.

Umenena kiongozi,nchi ipoipo tu kina madelu na wenzake wanakula Kwa urefu wa kamba huku wakimsifu mama hadharani na kumng'ong'a mafichoni...
 
Malori ya kuwabeba wanaccm na halaiki toka mikoani yamekwama na mvua.
 
Huo mtaa wenu wa Selassie labda ni wachawi watupu, haiwezekani mji mzima maji yamejaa kwenu nyie kukavu.

Mechi ya Yanga juzi wamecheza JKT kule uliona watu walio hudhuria? Matawi ya Yanga tu hata ma 5 sidhani yalifika na mechi ni Dar hapa hapa sababu nini unadhani?
Mitaani maji yamejaa bado unataka watu wajazane ili iweje?
habari ya sidhani ni habari za kipumbavu! Mechi ya yanga juzi nadhani yalifika matawi 12.
Wewe unaongea kuhusu uchawi au tunazungumzia umuhimu wa tukio kwann watu hawajaenda? Mimi ninakueleza mtaa unaotazamana na uwanja watu wamelala ndani na geti ameliona mitaa ya karibu na hapa hakuna mvua ya kuzuia watu kufika uwanjani. HAKUNA MTU ANAYEELEWA NINI MAANA YA HUO MUUNGANO HATA WEWE PIA VILE VILE HUELEWI . Sio mimi tu peke yangu wengi vile vile hawaelewi. Sasa unaendaje kwenye sehemu kitu hukielewi?
 
Wakuu natizama maadhimisho ya muungano, idadi ya watu mpaka Sasa ni ndogo mno kulingana tukio lenyewe. Je, ni uwepo wa mvua ama ni watanganyika kutokuona umuhimu wa tukio lenyewe na kukatishwa tamaa na jinsi mambo yanavyoendeshwa nchini?

Maoni yenu wakuu.
Uwepo wa mvua mkuu mvua imepiga sana nina iman kungekua hakuna mbua watu wangejaa sehem zingine watu hawawez kutoka kabisa usafir hakuna kutokana na njia
 
Hilo ni wazo lako na hakukua na hakika kwamba kutakuwa na mvua za muendelezo. kumbuka hili suala linapangwa kwa siku kadhaa kabla ya tukio.
Utabiri wa hali ya hewa, wameweka wazi uwepo wa mvua nyingi ukanda huu hadi mwezi ujao!!... 😳
 
Wakuu natizama maadhimisho ya muungano, idadi ya watu mpaka Sasa ni ndogo mno kulingana tukio lenyewe. Je, ni uwepo wa mvua ama ni watanganyika kutokuona umuhimu wa tukio lenyewe na kukatishwa tamaa na jinsi mambo yanavyoendeshwa nchini?

Maoni yenu wakuu.
Hiyo sentensi ya mwisho ndo sahihi!!

Pengine baada ya mawaziri kuhusika kumtusi na kutokuwachukulia hatua, sasa hujuma imehamishiwa eneo hilo. Ikiendelea hivi CCM tunakwenda kupoteza uchaguzi.
 
Yule naniliu wa Arusha angeujaza Uwanja bila kujali mvua wala nini [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Hata ukitangaza jambazi maarufu lililoua watu wengi litaletwa uwanjani, watu watajaa kuja kushuhudia hilo ni jitu la namna gani. Majambazi yataenda na watu wema wataenda ila kila kundi likiwa na sababu tofauti.
 
Hao wachache wanatosha. Hata hivyo waliokomaa kutuunganisha ni jamaa wawili tu.
 
Kuna mambo mawili;
Mvua
Hisia za watu juu ya Muungano

Mvua: Watu hawana uhakika wa kula yao ya leo sababu ya hizo mvua zenu, bado unawataka wahudhurie maadhimisho hayo? Wapite kwenye barabara gani wakati miundombinu imeharibika, mitaa imejaa maji, ajali zimeongezeka, nyumba zinaelea kwenye maji na mvua zinaendelea kunyesha?
Nani aende uwankani kunyeshewa na mvua mwanzo mwisho. Timu za mpira zenyewe pia zina struggle kujaza viwanja sasa hivi.
Lile fungu ambalo CCM hupewa ili kukusanya watu na kuwasafirisha kwenda kwenye matukio kama hayo, safari hii limeliwa

Hisia za watu
Linaweza likawa ni jibu la watu juu ya Muungano. Wameamua kuukataa na kutoutambua kwa vitendo. Muungano hauna tija kwa wananchi zaidi ya kuwasababishia waishi na wenzao kwa kusimangwa kwa kila kitu utadhani labda wao ni wakinbizi au wakoloni tu.
Pia imejidhihirisha hapendwi!!! Kumbe kundi la CHAWA ni dogo sana
 
Hata ukitangaza jambazi maarufu lililoua watu wengi litaletwa uwanjani, watu watajaa kuja kushuhudia hilo ni jitu la namna gani. Majambazi yataenda na watu wema wataenda ila kila kundi likiwa na sababu tofauti.
Cha muhimu ni Uwanja kujaa mbele ya USO wa Wageni Wetu 😂😂
 
Uwepo wa mvua mkuu mvua imepiga sana nina iman kungekua hakuna mbua watu wangejaa sehem zingine watu hawawez kutoka kabisa usafir hakuna kutokana na njia
Hao wachache waliofika uwanjani wamepelekwa na Chopa?
 
Kwa jinsi zanzibar walivyotupiga viboko wakati tunakula mchana wa mwezi wa ramadhan kwakweli hatuna hamu na muungano
 
Wakuu natizama maadhimisho ya muungano, idadi ya watu mpaka Sasa ni ndogo mno kulingana tukio lenyewe. Je, ni uwepo wa mvua ama ni watanganyika kutokuona umuhimu wa tukio lenyewe na kukatishwa tamaa na jinsi mambo yanavyoendeshwa nchini?

Maoni yenu wakuu.
Mambo yanayozungumzwa ni yaleyale miaka yote na hayatekelezwi yakakamilika hali inayopelekea watu kususia pia Kuna namna inabidi viongozi wetu wabadilike wamepewa dhamana ya kuwatumikia wa Tanzania na sio vinginevyo!
 
Wakuu natizama maadhimisho ya muungano, idadi ya watu mpaka Sasa ni ndogo mno kulingana tukio lenyewe. Je, ni uwepo wa mvua ama ni watanganyika kutokuona umuhimu wa tukio lenyewe na kukatishwa tamaa na jinsi mambo yanavyoendeshwa nchini?

Maoni yenu wakuu.
Umemaliza hapo mwisho maana hata hotuba ya jana hakuna aliyeifuatilia,Tunategemea kiongozi atupe hotuba ya kuelezea Taifa tunaelekea na tuko wapi kiuchumi na huduma za jamii kazi ipo.
 
Muungano ambao upande mmoja unatoa viongozi wa kutawala upande mwingine.Huu ni muungano au ukoloni ?.
 
habari ya sidhani ni habari za kipumbavu! Mechi ya yanga juzi nadhani yalifika matawi 12.
Wewe unaongea kuhusu uchawi au tunazungumzia umuhimu wa tukio kwann watu hawajaenda? Mimi ninakueleza mtaa unaotazamana na uwanja watu wamelala ndani na geti ameliona mitaa ya karibu na hapa hakuna mvua ya kuzuia watu kufika uwanjani. HAKUNA MTU ANAYEELEWA NINI MAANA YA HUO MUUNGANO HATA WEWE PIA VILE VILE HUELEWI . Sio mimi tu peke yangu wengi vile vile hawaelewi. Sasa unaendaje kwenye sehemu kitu hukielewi?
Hold on.! unaonekana unauelewa hafifu sana.
Hapa tunazungumzia upungufu wa watu uwanjani. Hoja yangu ni sababu ya mvua.
Watanzania wameanza lini kutoelewa Muungano mpaka ije ghafla leo wasiende? Tangia miaka mingi watu hawaelewi huu Muungano lakini haiwazuii kwenda uwanjani.

Sababu ya mvua hata mtoto mdogo anaweza kujua kwakua ni week sasa mvua inanyesha kubwa na kuzua taharuki mtaani.

Wewe kama unaishi mtaa wa uwanja wa Taifa inahusika vipi? acha ujinga kijana leta hoja.
Huu muungano ni muda mrefu watu hawauelewi si Bara sio visiwani ila haijawahi zuia watu kwenda uwanjani labda ulete sababu nyingine naweza kukuelewa.
 
Back
Top Bottom