Maadhimisho ya miaka 60 ya muungano na idadi ndogo ya mahudhurio uwanjani, nini tatizo?

Maadhimisho ya miaka 60 ya muungano na idadi ndogo ya mahudhurio uwanjani, nini tatizo?

Tatizo Kubwa Naona Ni Wananchi Kuuona Ukweli Wenyewe Upande Wa Maisha
Tanzania Watu Hawana Furahi, Hali Ngumu Sana Ya Maisha Leo Unawaita Walowe Na Mvua
Dar Es Salaam Imezingirwa Na Mafuriko Kote Kote

Halafu CCM Inadharau Wananchi Kwanini Wapeleke Tukio Dar Es Salaam Wakati Serikali Ipo Dodoma
 
Kinacho takiwa kufanyika kwenye sherehe hizo,ni kuonesha Taifa limepiga hatua gani kwenye Sayansi na teknolijia sio maonesho ya kupasua matofari kwa kichwa.
nashangaa sana hii maonesho imekuwa km ya kudaganya watu kila day, historia na maendeleo yanayojadiliwa ni yaleyale kila mwaka
 
sasa c wangesema watu wamfuatilie raisi kupitia runinga zao majumbani akihutubia kutoka ikulu kuliko kodi za watanzania zitapanywe tu
Hilo ni wazo lako na hakukua na hakika kwamba kutakuwa na mvua za muendelezo. kumbuka hili suala linapangwa kwa siku kadhaa kabla ya tukio.
 
Wakuuu naomba kuuliza hivi wanajeshi mbona siwaoni kwenye gwaride?
Hawakuwepo wale ni migambo,walipoanza kuigiza Kwa kurukaruka wakisema ni makomandoo nilizima runinga..Karne hii? Aibu hawaangaliagi Kwa wenzetu kama Kwa kiduku,china urusi na kwingineko?Kuna muda wanafanya kupandisha Mori kama morani wa kimasai,duh my kantre
 
Muda mwingine tusitumie mihemko kujadili kitu, kwa akili ya kawaida unaona mvua ipo.
 
ndio nakuuliza muda huu wewe upo temeke au kurasini? Na upo sehemu gani?
kuhusu kujua sehemu yangu hilo halihusiana na mada mkuu.
Suala ni kwamba wakati ule tangu asubuhi kumekucha kulikuwa na mvua kubwa at least muda huu imepungua.

Kuhusu Temeke na Kurasini pia mvua ilikuwepo na Ushahidi ni picha za moja kwa moja toka Uwanjani. Punguza ujuaji wa kishamba
 
Hawakuwepo wale ni migambo,walipoanza kuigiza Kwa kurukaruka wakisema ni makomandoo nilizima runinga..Karne hii? Aibu hawaangaliagi Kwa wenzetu kama Kwa kiduku,china urusi na kwingineko?Kuna muda wanafanya kupandisha Mori kama morani wa kimasai,duh my kantre
kwwni huko china, urusi na kwa kiduku huwa hawafanyi gwaride?
 
Wakuu natizama maadhimisho ya muungano, idadi ya watu mpaka Sasa ni ndogo mno kulingana tukio lenyewe. Je, ni uwepo wa mvua ama ni watanganyika kutokuona umuhimu wa tukio lenyewe na kukatishwa tamaa na jinsi mambo yanavyoendeshwa nchini?

Maoni yenu wakuu.
Bila picha?
 
Muungano si wawananchi,huu muungano ni wa viongozi kugawana vyeo.
 
kuhusu kujua sehemu yangu hilo halihusiana na mada mkuu.
Suala ni kwamba wakati ule tangu asubuhi kumekucha kulikuwa na mvua kubwa at least muda huu imepungua.

Kuhusu Temeke na Kurasini pia mvua ilikuwepo na Ushahidi ni picha za moja kwa moja toka Uwanjani. Punguza ujuaji wa kishamba
wewe ndio mjuaji na mshamba. Hapa maeneo ya selassie kukavu na hiyo mvua si mvua ya kusema watu washindwe kutoka . Sema hakuna msukumo wa watu kwanini aende huko . Unafikiri simba na yanga mvua ingekuwa inanyesh uwanja ungeacha kujaa? Uwe unaacha ujuaji wa kijinga. Achana tu na mtaa wa makaburini hao wanaoishi huo mtaa unaotazamana na uwanja wa taifa watu wamelala ndani na geti la uwanja analiona.
Wacha kusema watu wameshindwa kwenda sababu ya mvua sema Hakuna anayeleewa hicho kitu ni nini. Hata wengi walioingia mule mbali na wanafunzi kubebwa t hata watu wazima hawawezi kukuelezea huo muungano
 
Mvua ina nyesha mji mzima barabara zinazo elekea uko na mjini zime fungwa una tegemea watu wakajazane uwanjani wakati local channel zote ziko MBASHARA
Bora niangalie upendo tv na katuni za junior kuliko niangalie tbc,itv,clouds channel ten
 
Wakuu natizama maadhimisho ya muungano, idadi ya watu mpaka Sasa ni ndogo mno kulingana tukio lenyewe. Je, ni uwepo wa mvua ama ni watanganyika kutokuona umuhimu wa tukio lenyewe na kukatishwa tamaa na jinsi mambo yanavyoendeshwa nchini?

Maoni yenu wakuu.
1.Muungano hauna faida kwa mwananchi wa kawaida,so why attend,binafsi sioni faida.Ni a lunatic tu anayeweza kuhudhuria sherehe za nanna hiyo.
2.Nchi imekuwa ya watu wachache, wananchi wa kaida wametengwa, wanaofaidi nchi waende.
3.Nchi kwa sasa ni captured na dark forces na viongozi ni collaborators,so why support them.
4.Viongozi hawajali maslahi ya mwananchi wa kawaida,kwa hiyo waendelee wenyewe.
5.Kila eneo ambalo lingekuwa la manufaa kwa mwananchi wa kawaida viongozi wanalihujumu kwa kuiba fedha za miradi.Kwa mfano miradi ya upatikanaji wa umeme,maji,kilimo, elimu,miundo mbinu etc.Watu wanaiba pesa za miradi,CAG anatoa ripoti,kwa hiyo wezi wanafahamika,no action is taken.It would be stupid to support such a corrupt government.
 
Back
Top Bottom