Maadhimisho ya Uhuru wa Tanganyika, na nafasi ya Kanisa Katoliki

Maadhimisho ya Uhuru wa Tanganyika, na nafasi ya Kanisa Katoliki

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2010
Posts
17,005
Reaction score
20,425
Maadhimisho ya Uhuru wa Tanganyika yanaweza kutupa sura mpya tusiokuwa tukiifahamu sote, Pengine ni kwa mara ya kwanza Kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi ndio kinaeleza uhusika kikamilifu wa Kanisa katoliki duniani katika uhuru wa Bara la Afrika na hasa Tanganyika chini ya shirika nguli la Ujasusi la Kanisa hilo . Utafiti wa kinyaraka na machipuzi ya nera kwa mambo anuawai, ndio yaliyonihakikishia kuhitimisha katika kitabu hiki, Tunapoadhimisha kumbukumbu ya Uhuru wa Tanganyika tunayo sababu na ni haki yetu kutambua mchango wa kila mtu alivyoshiriki katika uhuru huo, haijalishi mapokeo, Tusipoandika historia yetu, tusilaumu tukiandikiwa.

Hebu turejee kwenye Kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi, Kwa mfano, hali ya Tanganyika kuwa eneo ka kudhaminiwa, ilisababisha Uingereza kutokubali walowezi wengi kuja hapa. Vivyo hivyo, hali ya Afrika ya Kusini Magharibi kuwa eneo la kudhaminiwa, ilizuia sehemu hii kuwa jimbo la Afrika Kusini kuwa msingi kwa uhuru wake kama nchi ya Namibia.

Jukumu la kuandaa nchi hizo kupata uhuru liliratibiwa na shirika hilo la kijasusi (Jeisuiti) kwa ustadi mkubwa bila baadhi ya makoloni kujua. Lakini, lilikumbana na kiunzi/ukinzani hasa kufuatia mnyumbuliko wa kiimani ndani ya Ukristu, kufuatia nguvu ya Cambrige (Anglikana).

Mgogoro huo ulikuzwa kwa kuwa Anglikana nao tayari walikuwa wameaandaa shirika lao la kijasusi la Fabian Society, maalumu kwa minajili ya kuwaandaa Vijana katika makoloni Uingereza hususani barani Afrika, kukabidhiwa nchi zao na kwa Tanganyika Fabian Society wao walikuwa wamemuandaa Chifu David Kidaha Makwaia huku Jeisuti ya Katoliki wakiwa wamemuandaa Julius Nyerere. Rejea kitabu cha Vatican Assassins cha Eric Jon Phelps akieleza nguvu ya Vatican katika kudhibiti ulimwengu, anakazia katika harakati za ukombozi duniani hasa Afrika na nafasi ya kanisa chini ya Jeisuti.

Barani Afrika, Jesuiti ilibadili mbinu kwa kuwa dola la Kiingereza, lilikuwa kikwazo kwa sehemu fulani. Haikujikita kwenye dola, bali ilisimama katika muundo wa shirika likifanya shughuli zake ndani ya Kanisa. Dhamiri shahiri, ilikuwa lazima itimie, kama ilivyoelezwa mwanzoni kuwa hawa ndio wabobevu wa elimu ya juu kwa kila nyanja na ndio wanaotawala ulimwengu. Kwa hiyo, hivyo vikwazo havikukwamisha wao kufikia malengo.

Katika Tanganyika, chini ya Udhamini wa Shirikisho la Kimataifa, kulikuwa na harakati za hapa na pale za kudai haki za kiraia kwa wenyeji. Ifahamike kuwa vyama vya harakati Tanganyika vilikuwa vingi sana, na vipo vilivyokuwa vikipingana vyenyewe kwa vyenyewe. Mwaka 1927 hadi 1929, kanisa Katoliki nchini, chini Joseph Gabriel Zelger, lilibainika kuingiza siasa katika utendaji kazi wake Tanganyika, kitendo hiki kiliwakwaza wakuu wa mamlaka ya kikoloni na kupelekea majasusi wakikoloni wapendekeze aachishwe uongozi wa kanisa nchini. Ni kweli. Tar. 12 Februari, mwaka 1929, Zelger alistaafu wadhifa wake kwa lazima.

Ni mwaka huohuo wa 1927, ndio Chama cha African Assosiotion (AA) kilianzishwa na Gavana Sir David Cameron, maalumu kwa minajili ya kuratibu mambo ya sherehe za watu weusi pembeni ya mji, huko mtaa wa Stanley (leo Lumumba) na akawapa jengo la ofisi mahali leo wanapojiita TANU ilizaliwa. Lakini, historia ya Tanganyika haiwataji kinagaubaga waasisi wa AA: Rais wa kwanza, Mwalimu, Cesil Matola (msomi wa mwanzo kabisa enzi za Mjerumani kutoka kabila la Wayao), Katibu Mkuu wa kwanza, Klest Sykes (Mzulu, Baba yake alikuwa mateka wa kikoloni kutoka Afrika Kusini), Mwekahazina, Ali Ramadhan (Mzaramo na mvuvi maarufu wa pwani la Azania leo bahari ya Hindi).

Hawa ndio mwaka 1927, waliounda Chama cha kwanza kabisa cha kutetea maslahi ya weusi Tanganyika na shughuli zake zilikuwa ni kuratibu sherehe za waafrika tu. (Chama cha walevi kwa lugha nyingine). Mwaka 1933, Mwalimu Cesil Matola alifariki na nafasi yake ikakaimiwa na katibu mkuu wa chama hicho, Bw. Klest, mpaka ilipofika mwaka 1948, yakatokea mapinduzi yaliyoongozwa na mtoto wa Klest, aliyeitwa Abdulwahid Sykes.
Abdulwahid Sykes alitoka kupigana Vita Kuu ya Pili ya Dunia, huko Burma. Aliporudi, alikuwa na mawazo ya ujana kutoka vitani, akampindua baba yake kwa vurugu na ngumi. Mapinduzi yaliyoitwa ‘ondoa wazee’. Kisha chama cha AA kikabadilishwa jina na kuitwa TAA ambapo Rais wake wa Kwanza, akawa Daktari wa binadamu Vedasto Kyaruzi (Mhaya), aliyekuwa anafanya kazi Kingorwila Mkoani Morogoro.

Huyu ndie daktari wa binadamu wa kwanza kabisa wa Kiafrika, Tanganyika. Katibu Mkuu, akawa Abdulwahid Sykes mwenyewe na Mweka Hazina akawa Dosa Azizi. Miaka miwili tu ya chama kipya, yaani 1950, Daktari Vedasto Kyaruzi, kwa ghiriba za wakoloni, alihamishiwa Sengerema Mwanza, kama sehemu ya kumuondoa jijini Mzizima leo Dar es Salaam awe mbali na harakati. Nafasi ya rais wa TAA ikakaimiwa na Bw. Adbulwahid, mpaka mwaka 1953, uchaguzi ulipofanyika na Julius Nyerere akashinda pale kwenye ukumbi wa Anautoglo (Mnazimoja ya leo).

Mnamo tar. 7 Julai, mwaka 1954, Vijana (wazee wa Kariakoo) wakiongozwa na Mwl. Nyerere, walikubaliana wazo la kuhuisha chama kutoka TAA kwenda TANU, chini ya uratibu wa karibu wa Wajesuiti (Askofu Maranta) na Waislamu (Sheikh Issa bin Amir) ijapokuwa alikuwa amefariki mwaka mmoja nyuma, hekima za Sheikh huyu ziliendelea kusaidia. Na zaidi ni kuwa safari ya kwanza ya Mwl. Nyerere ya kwenda UNO tar. 5 Machi, mwaka 1955, kanisa Katoliki lilitoa msaada kwa chama cha TANU wa tikiti ya ndege ya kwenda na kurudi. Lilifanya hivyo kupitia shirika lake la Maryknoll Sisters la New York Marekani.

Si hivyo tu, bali katika moja ya utani wa Mwl. Nyerere wenye ukweli ndani yake, aliwahi kusema kuwa makasisi Walsh na Art Wille wa Shirika la Maryknoll ni mabosi wake, akikumbuka malipo ya Shilingi mia sita (600/=) angali ameacha kazi ya ualimu, akiwa kijijini Butiama. Kuna ushahidi wa kihistoria pia unaochagiza habari hizi kwamba majasusi wa Kanisa walimuandaa Mwalimu Nyerere kuja kuiongoza Tanganyika mpya. Barua ya lugha ya Kilatini, ya kitume, Tot Tangaeque, ya Papa wa Roma, ya tar. 8 Novemba, mwaka 1984, kwenda kwa Kanisa Katoliki Tanzania, inautangazia ulimwengu kwamba Tanzania itakuwa chini ya himaya ya kanisa kwa mwavuli wa Bikira Maria Imakulata.

Miaka thelethini na mbili (32) baadae, Kanisa Katoliki Tanzania chini ya Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu Tanzania, Askofu Tarcisius J.M. Ngalalekumtwa, linaijibu barua hiyo kwa barua yenye kumbukumbu nambari TEC/PR/1 ya tar. 10 Novemba, mwaka 2016, likikubaliana na kuitangazia dunia kuwa siku ya Uhuru wa Tanganyika, tar. 9, mwezi 12 ya kila mwaka itakuwa pia siku ya kuadhimisha Sikukuu ya Bikira Maria Imakulata. MSIMAMIZI wa JAMHURI ya MUUNGANO wa TANZANIA......

Kupata ufahamu zaidi, Soma kitabu cha Ujasusi kwa bei ndogo kabisa na halisi ya 80,000 tu popote ulipo

Lipia 80,000 kwa Mpesa au Tigopesa 0715865544/0755865544 (Yericko Nyerere). Kisha tuma majina yako na mahali ulipo.

Utaletewa kitabu popote ulipo. Nje ya dar utalipia nauli 8,000/
 
Uzi mrefu kumbe point ni kuuza kitabu

Yericko huaminiki hata vitabu vyako hakuna wa kuviamini , ulintukana sana mzee lowassa ,alipokuja chadema ukamsafisha ,

Huaminiki hata kidogo, hivo vitabu vyako baki navyo mwenyewe
Strategic ya Romani Catholic ni kubwa sana. Leo wameweka makanisa meengi katika dola ya kiislamu pia hata Zanzibar wao ndio wauzao kitimoto na kukifuga.

Waislam wanaishi bila strategies kabisa kazi kukurupuka.

Leo wanawakaribisha waislamu wengi huko nje yaani marekani na UK na kuwaachia makanisa ili iwe misikiti na waislamu wameingia mkenge wanaitumia na vyombo vya habari vinatangaza dunia ione alafu waislamu wao wanacheka na kufurahia hawaelewi mambo ya strategic kabisa.
 
Mkuu Yericko, Asante kwa hii, kumbe ni kanisa letu, Takatifu, Katoliki la Mitume, ndilo limetupatia uhuru na sio wale wazee wa naniliu?. Kila siku, nimekuwa nikijiuliza, kwani akiwa Mkristu, ni lazima awe Mkatoliki?!. Nyerere alikuwa Mkatoliki, Mkapa, Mkatoliki na mwaka mmoja kabla Magufuli hajaingia, kuna kitu nilikisikia hapa, japo sikukisema kumhusu Magufuli
Na kweli ikatokea kweli kuwa ni Magufuli, na Magufuli ni Mkatoliki...
This is a very amazing coincidence, kila akiwa Mkristu, inatokea tuu, lazima anakuwa ni Mkatoliki!.
P
 
Tangazo hili lilipiwe , kitabu cha ujasusi kinauzwa ubungo bukubuku hii ni laana sasa

USSR
 
GENTAMYCINE njoo umshangae na Yericko Nyerere anayezungumzia Uhuru wa Tanganyika!!!
 
Katoliki ukiishakuwa padri muasi, ndio basi tena. Angekuwa Membe.
Kama ulinote EL alijitoa sana kwenye harambee za kanisa Katoliki, hata Regina akaandika kitabu ili kumnasibu EL na Ukatoliki!.
P
Kweli mkuu nadhani ni kheri muislam awe raisi kuliko protestant

Akiwaga raisi mwislamu kunaibukaga NGO's nyingine za kutetea haki za binadamu, haki za kiraia, jukwaa LA katiba, nyaraka za kitume

Raisi akiwa katoliki zinapotea
 
Yeriko kwenye mada za haya mambo kuna moja aliandika bibi Cecil Matola wakati ni mwanaume mpaka Pascal alivyomkosoa ndiyo akaedit
Nyingine kuna picha kina bibi titi wamevaa mabaibui ya kitambo hata bibi yangu Mwajuma bint Bakari RIP nilimuona nalo yeye akasema wale ni masister wa kikatoliki.
Toka hapo sijisumbui kusoma hii migazeti yake
 
Back
Top Bottom