- Thread starter
- #61
Wanashindwa kuelewa kila mtu hapa duniani yupo kwaajili ya kutafutia tumbo, hata huyo Lissu Sasa anaonekana mpinzani halisi kwakua ana matumaini ya Urais, Ila ikitokea kaukosa, na asione masilahi yoyote ndani ya Chadema kwa Miaka 10 ijayo, si ajabu akaunga juhudi.
Pongezi kwako kutambua hili:
"Lissu Sasa anaonekana mpinzani halisi."
Na huo ndiyo ulio ukweli thabiti. Ndiyo maana hata pamoja na kuyachagiza manyumbu ya Lumumba na maafisa vipenyo wote kuwa ni mwenzao - yote kabisa maji ga nyanja. Bado yame 'mute' tu. Kimyaaa, utafikiri hayapo!
Yamechanganyikiwa yasijue la kufanya. Kuweweseka tayari imebakia kurokota makopo tu sasa.
Pia ungemalizia kwa kutambua kuwa "jiwe yuko after maslahi yake zaidi na ndiyo maana kukandamiza haki na uhuru wetu ki hivi." Ungekuwa umejitendea haki zaidi.