Maajabu ya Mungu: Nimeiombea "graphics card" mbovu - imepona!

Maajabu ya Mungu: Nimeiombea "graphics card" mbovu - imepona!

Wewe umeshachanganyikiwa.... kwani ukiwa mlokole lazima uwe kichaa pia?
1 Kor 1:18-25
"Neno la msalaba kwao wanaopotea ni upuzi, bali kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu. Kwa kuwa imeandikwa, Nitaiharibu hekima yao wenye hekima, Na akili zao wenye akili nitazikataa."
 
Ni halali kugombea computer kama wewe ni fundi stadi na umeshindwa kuitengeneza.
Unaweza kugombea computer kwa sababu computer ina roho.
Hata binadamu. Kama daktari ameshindwa kumtibu unampeleka kwa Mwamposya.
 
Mungu anaweza. Ukiomba kwa moyo Mungu anasikia. Tunaomwamini Mungu haya tunayajua.
 
Ni halali kugombea computer kama wewe ni fundi stadi na umeshindwa kuitengeneza.
Unaweza kugombea computer kwa sababu computer ina roho.
Hata binadamu. Kama daktari ameshindwa kumtibu unampeleka kwa Mwamposya.
Sijakuelewa ndugu. Kugombea au kuombea computer?
 
Heshima zenu wakuu. Mada hii ni habari ya kweli kabisa. Kila mara huwa nasisitiza hapa kwamba uongo nauchukia kama ukoma. Hivyo unaposoma mada hii usifikiri ni chit chat au chai. Ni kweli kweli tupu.

Haya, twende kwenye mada sasa. Kwanza namshukuru Mungu mambo ya IT hayajanipita kando. I can build a custom PC from scratch.

Hivi majuzi, graphics card(GPU) ya PC yangu iliharibika. By the way, kabla hujaendelea kusoma, kama hujui umuhimu wa GPU, muulize chatGPT ili twende pamoja vizuri.

OK, tuendelee. Ilitokea ghafla tu, niliwasha computer ikawaka, lakini screen ikabaki nyeusi. Nika-reboot, screen ikatoa mistari au dots dots za rangi ya kijani kwenye desktop bila kuonesha picha. Kabla ya hapo, nilishindwa kabisa kufanya video rendering. Kila nikijaribu, PC ina-crash bila kutoa warning yoyote. Nili-update drivers, lakini haikusaidia.

Nilifanya display device replacement ku-verify monitor functionality. Monitor ya pili nayo pia ilibaki nyeusi. Nikafanya video cable replacement test ku-verify signal integrity, tatizo halikuondoka. Kisha nikafanya GPU hardware troubleshooting procedure, nikajiridhisha card imeharibika.

Kwa mtazamo wa imani ya Kikristo, Mungu anaweza kuponya chochote, hata vifaa vya kielektroniki, kama mtu ataomba kwa imani.

Marko 11:24 inathibitisha ukweli huo:
"Kwa sababu hiyo nawaambia, yoyote mtakayoyaomba mkisali, aminini kwamba mmeyapokea, nayo yatakuwa yenu."

Mungu anasema pia katika Yeremia 32:27
“Mimi ndimi Bwana , Mungu wa wote wenye mwili. Je, kuna jambo lolote lililo gumu nisiloliweza?"

Hiyo inatufundisha kwamba hakuna kitu ambacho ni kikubwa kwa Mungu, hata vifaa vibovu au matatizo yetu ya kila siku Mungu anaweza kuyatatua.

Yesu anasema tena katika Marko 11:23
"Amin, nawaambia, mtu yeyote atakayeuambia mlima huu, ‘Ngʼoka ukatupwe baharini,’ wala asione shaka moyoni mwake, bali aamini kwamba hayo asemayo yametukia, atatimiziwa."

Kuuambia mlima ung'oke ni jambo zito kibinadamu. Vivyo hivyo kwa mtu asiyeamini, anaweza kuona uzito sana kuiombea GPU.

Mimi nimemuona Mungu akinifanyia mambo mengi, makubwa sana katika maisha yangu, baada ya kumuomba. Hivyo niliiombea GPU nikaamini kuwa itapona kwa Jina la Yesu na itafanya kazi tena! Hivi ninavyoongea, GPU imepona na inafanya kazi bila tatizo. Screen inaonesha picha na apps zinazohitaji GPU zina-function properly. Mungu ni mwema kila wakati, haleluya!
MUNGU HASHINDWI JAMBO.NI TAJIRI MKUU.TAJIRI ASIYE MFANO.MFALME WA WAFALME,YAANI NI MKUU WA WAKUU.ATUKUZWE MUNGU,MILELE NA MILELE.
 
Haya mambo yapo mimi niliombewa na member mmoja humu Busu la Kenge kila kitu kineninyookea sasa hivi nimeagiza gari la saba
Uza kila kitu ulicho nacho, wagawie maskini fedha utakayopata, nawe utakuwa na hazina yako mbinguni; halafu njoo umfuate Yesu (Luka 18:18-43).
 
Uza kila kitu ulicho nacho, wagawie maskini fedha utakayopata, nawe utakuwa na hazina yako mbinguni; halafu njoo umfuate Yesu (Luka 18:18-43).
Nimeshauza kila kitu
Uza kila kitu ulicho nacho, wagawie maskini fedha utakayopata, nawe utakuwa na hazina yako mbinguni; halafu njoo umfuate Yesu (Luka 18:18-43).
 
To brand a testimony of divine intervention as 'nonsense' is to exhibit not only a deplorable deficiency of spiritual discernment but also an audacious contempt for the metaphysical verities that transcend empirical reductionism. Such cavalier repudiation exposes an intellect ensnared in the prison of materialistic dogma, impervious to the pneumatological realities by which God manifests His sovereignty even in the minutiae of creation. Beware, for to scoff at the operations of the Almighty is not merely an act of ignorance but an indictment of the heart’s obstinate rebellion against eternal truth.
 
Back
Top Bottom