Maajabu ya mwanamke mjamzito kuomba police wamwambie mume asimpige tena sababu anampenda sana, hii ni baada ya kupewa kipigo kizito!

Maajabu ya mwanamke mjamzito kuomba police wamwambie mume asimpige tena sababu anampenda sana, hii ni baada ya kupewa kipigo kizito!

Kwa hiyo mtu akiwa na mimba ndo apigwe hivyo na aone ni Sawa tu?

Huyu mama anakaa na mtu ambae ameshamiathiri kiakili sasa amehamia rasmi kwenye mwili

Wakienda enda anamnalizia kabisa
Wanawake tunapitia changamoto sana.imagine huyu ameonekana katika vyombo vya habari…

Vipi wale ambao hawaonekani?na wanapitia mateso?

Ninauhakika huyu dada anataka kumsamehe ili akamnase tukio la uzima huyo mwanaume
 
Dah!! Yaani mkeo unapiga Kama unaua nyoka🤔
Mke mwenyewe ndio kaishazimika mazima😂😂
Ipo siku watagawana majengo ya serikali.
 
Mbona hizi nyuzi sioni wahusika🤣🤣🤣🤣wanasubiri wapuuzi wenzao wanapoanzisha nyuzi za kutukana wanawake na kuwaita mafeminist na viumbe wa ajabu yanaenda kujazana kama nzige. Wanawake tafteni kazi za kufanya ona huyu dada anaonekana zamwamwa kwasababu anakomaa na vipigo hana pakwenda.

💯✔
 
Mama mwenye ujauzito wa miezi minne Jamila Hamisi (34) mkazi wa mtaa wa Remtula kata ya Elerai Jijini Arusha, amedai amejeruhiwa macho yake kwa kupigwa ngumi za uso na mume wake baada ya kutokea mzozano kati yao desemba 27, 2022.

Jamila ameliomba Jeshi la polisi mkoa wa Arusha limkanye mwanaume huyo ili aweze kuendelea kuishi naye kwakua bado ana upendo naye.

View attachment 2467685


Hawa ndio wanaishiaga kugawana majengo ya serikali - warudiane kisha mmoja aishie mortuary mwingine jela
Hawa ndio wanaishiaga kugawana majengo ya serikali - warudiane kisha mmoja aishie mortuary mwingine jela
 
Marriage imekuwa Suffering....Kuogopa tu kuitwa "Single Mother".
Hii wala haina uhusiano na hilo eneo unalozungumzia. Huyu kabaki hapa kwa matatizo yake ya kiakili na wala haina uhusiano na kulinda Ndoa au heshima.
 
Mwanaume wa kupiga kiasi hiki hapana kwakweli.

Mapenzi matamu mkinuniana kiaina lakini si kwa ulingo huu.huu uwanja ni wakina mandonga mtu kazi

Akili itakuwa imetingishika kidogo.wasubirie akili ipoe,itulie na kukaa mahali pake ndipo waje maswali kama hayo
Ni hatareee tupuuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sijawahi kupiga mwanamke ila natamani siku nitandike mtoto wamama mkwe mpaka alazwe
 
Wewe nawe ni walewale wauaji. Yaani shida yako ni kuhalalisha huu unyama alofanyiwa Huyu mwanamke tuu

Mfyuuuu
We unadhan kumwambia mwanaume kuwa mtt c wake ni jambo dogo eeh?jichanganye ung'olewe taya
 
Mama mwenye ujauzito wa miezi minne Jamila Hamisi (34) mkazi wa mtaa wa Remtula kata ya Elerai Jijini Arusha, amedai amejeruhiwa macho yake kwa kupigwa ngumi za uso na mume wake baada ya kutokea mzozano kati yao desemba 27, 2022.

Jamila ameliomba Jeshi la polisi mkoa wa Arusha limkanye mwanaume huyo ili aweze kuendelea kuishi naye kwakua bado ana upendo naye.

View attachment 2467685


Hawa ndio wanaishiaga kugawana majengo ya serikali - warudiane kisha mmoja aishie mortuary mwingine jela
Sasa hata kama ni hasira sio kwa kipigo hiki!!
Unampigaje binadamu mwenzio,Tena mke kama unapiga mwizi!!!
Yaani nikiona matukio kama haya,huwa nahisi nywele za shingo zinasimama!!!
 
Changamoto iliyopo kwa sasa katika mahusiano kwenye jamii ya mtu mweusi ni uwepo wa vijana na mabinti wenye traumatic experiences tofauti tofauti ambazo wamezipitia katika malezi na makuzi yao.

Tunashuhudia huku mtaani ndoa changa za wanawake na wanaume wenye umri mdogo wakipigana, kuchaniana nguo, kutukanana, kufokeana, kudhalilishana na matendo mbali mbali ya kukosa hekima na heshima mbele za watoto wadogo sana ambao hawajafikia hata miaka 10.

Haya matendo huacha impact mbaya sana katika akili ya mtoto katika makuzi yake. Maana anachokiona ndicho kitakwenda kuhifadhiwa katika kumbukumbu za kudumu za akili yake.

Imagine mtoto wa miaka 5 au 7 wa kike,anamuona mama yake wa umri wa miaka 23 au 24 akipigana na baba yake wa miaka 25,28 au 30,wakitukanana matusi mazito huku wamezungukwa na majirani wakiwacheka na kuwashangaa kwa matukio yao haya ya kuaibisha.

Huyu mtoto atakuwa na hizi kumbukumbu na zitamuandama maisha yake yote. Akiwa mkubwa ni hawezi kuamini mwanaume kuwa anaweza mpenda maana ameona mwanaume namba moja (baba yake) akimshambulia mkewe (mama yake) badala ya kumprotect.

Hii itamtisha kuamini wanaume maisha yake yote especially mama yake atakapokuwa akimjaza maneno kama sehemu ya kutoa stress na heal maumivu ya moyo wake (wanawake wanafanya sana hii tabia).

And trust me, mtoto yupo bound kutafuta mwanaume mkorofi na kukubali kukaa nae huyo badala ya mwanaume mpole. Hii ni kwasababu ya vitu vifuatavyo:

Binti mwenye traumatic experiences za malezi mabovu ya wazazi huwa haamini katika maisha bora na ya utulivu sababu yale yaliyotokea kwa wazazi wake hayakumjenga katika kuwa na maisha bora bali maisha ya vita na kukorofishana 24/7. So endapo atakutana na kijana mpole, mstaarabu, muelewa na mpenda utulivu yeye atamuona kama hamchangamshi atataka fujo so lazima atamtibua na kumfanya ashindwane nae, maana mtu wa utulivu huwa hapendi ukorofi.

Wataalamu wa psychology wanasema mtu mwenye psychological issues na trauma huwa akikaa kwenye utulivu yale masauti kichwani yanaanza kumletea makelele ya kutamka afanye kile alichokiona wakifanya mama na mama yake. Umeshawahi kaa na binti ukasikia anakuuliza hivi wewe huwa unakasirikaga, nataka nione huwa ukikasirika unakuwaje, jua huyo hayupo sawa kiakili hata kama anajifanya mtulivu.

Pili, binti mwenye traumatic experiences za malezi mabovu ya wazazi wake huwa hana elimu ya kuishi vema na mwanaume ila ana elimu ya kuishi hovyo na mwanaume therefore ni lazima atakubali kuishi na mwanaume wa hovyo badala ya mwanaume wa kueleweka. Hii huwa ni reflection ya malezi na makuzi amepitia utotoni. Na ndio maana kama muhusika hapo juu amekung'utwa nusu ya kuuliwa ila unasikia upuuzi anao ongea hapo kuwa jeshi la polisi lisimuadhibu huyu jamaa yake kwa uhalifu wake na ukiukwaji wa sheria na kutenda jinai, bali wamkanye tu na yupo tayari kurejea kuishi nae.

Kimsingi hapo ni yeye amechagua kukaa na huyu jamaa. Jamii itamuona huyu jamaa ndie mtu mbaya au mkorofi ila niwaulize, hivi ikatokea mtu amejipeleka katika banda la simba pale Dar Zoo akafungua mlango na kujifungia kisha Simba akamrukia na kuanza kumrarua then raia wakawahi kumuokoa na majeraha yake kabla hajauwawa, halafu wiki moja baadae akarejea tena na kufanya ujinga ule ule hivi mtasema huyu simba auwawe kwa kumuua na kumla binadamu au itakuwaje?! Hapo nani hayuko sawa, ni binadamu au simba?!

Rejesha logic ya huo mfano katika hii story ya huyu dada, kesho unakuja kuona kwenye tv kuwa baada ya kurejea huyu dada aliuwawa miezi kadhaa baadae na huyu jamaa wake. Hivi inakufikirishaje hii story, kuwa jamaa ndie mwenye matatizo au ni mwanamke?!

So kimsingi mwanamke ndie ana matatizo hapa. Na ni victim wa childhood trauma. Kuna mambo alipitia akiwa mtoto na haya yamemjenga hivyo kudhani mahusiano ni kupigana na kuumizana kisha kusameheana na kuendelea kuishi mkisubiria next outbreak ya ugomvi na kujeruhiana kuanze upya.
 
We unadhan kumwambia mwanaume kuwa mtt c wake ni jambo dogo eeh?jichanganye ung'olewe taya

Umesikia wapi kwamba huyu mwanamke amesema mtoto sio wa huyo mwanaume!???
Au umeamua kukaa kitako kutengeneza maneno umbea!???
 
Umesikia wapi kwamba huyu mwanamke amesema mtoto sio wa huyo mwanaume!???
Au umeamua kukaa kitako kutengeneza maneno umbea!???
Hawa ndio wagawa vipondo wenyewe. Angekua mwanaume ndio kafumuliwa jicho zingejaa kelele humu ila wame'mute mwanamke ndio anaonekana kakosea utadhani walikuwepo muda wa tukio.
 
Umesikia wapi kwamba huyu mwanamke amesema mtoto sio wa huyo mwanaume!???
Au umeamua kukaa kitako kutengeneza maneno umbea!???
Umepanda mtumbwi wa kibwengo...na kwa haya makasiriko yako yawezkana ushamchanganyia damu huyo mwamaume wako....omba Mungu asigundue maana usharisk maisha kama huyo mwenzako hapo
 
Ukatili!! kwa nn majitu hayastaarabiki..Unampigaje hivyo mwanamke?
 
Umepanda mtumbwi wa kibwengo...na kwa haya makasiriko yako yawezkana ushamchanganyia damu huyo mwamaume wako....omba Mungu asigundue maana usharisk maisha kama huyo mwenzako hapo

Umeathirika kisaikolojia wewe

Yaani unadhani vile wewe ulibambikizwa kwa babako ndio kila mwanamke anafanya🙄🙄

Pole ndugu maana hiyo ni laana, na ndio maana unaona hata watoto uliodhani ni wako umebambikwa pia. Yaani kwa kifupi umevurugwa🤣🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom