Habari Wakuu!
Huu ndio ukweli mchungu, utake usitake. Kama hukumkuta mkeo akiwa na bikra basi tambua wazi kuwa wewe ndio mchepuko wa huyo unayemuona na kumuita mkeo.
Baadhi ya wanaume hulalamika na kuona uchungu wakisikia wake zao wanachepuka kwingine, wanachoshindwa kuelewa ni kuwa ukishaoa mwanamke asiye na bikra wewe ni mchepuko wake kwani shina kuu ni yule aliyembikiri. Na huyo mwanamke ataendelea kutoa matawi/michepuko kadiri ya siku zinavyozidi kwenda.
Kwani nini uwe mchepuko wakati wanawake wenye bikra wamejaa tele?
Kijana nakushauri kama hutaki kuwa miongoni mwa wanaoteseka ndani ya ndoa hakikisha unaoa mwanamke bikra ambaye wewe ndiye utakuwa shina kuu na sio mchepuko/tawi. Hii itakusaidia kuwa na amani ndani ya ndoa.
Kwa waliooa waendelee na ndoa zao, wapambane na hali zao.
Usioe mwanamke asiye na bikra kisha njoo unishukuru
Jokajeusi