Maana ya Mwanamke Bikra, Kuwa na Mahusiano/Kuoa Mwanamke Bikra

Wakuu Kwema!

Mara kwa mara nimekuwa nikihamasisha vijana humu kuwa wasioe wanawake wasio na bikra kwani hao sio wake zao. Pia mwanamke usikubali kuolewa na mwanaume ambaye hajaitoa bikra yako, huyo sio mumeo.

Huyo sio mkeo kama hukukuta bikra na wala hukuitoa. Huyo ni mke wa uzinzi, na lazima upate matokeo ya uzinzi,

Mwanamke uliyemkuta bikra na ukaitoa ndiye mkeo, huyo ndio mliwekeana agano la kuwa mwili mmoja na roho moja na yeye na sio mwanamke ambaye hukuikuta bikra yake.
Mwanamke kama hukuitoa bikra yake ni lazima akumbuke wanaume wake wa zamani, ni lazima awe mzinzi na malaya. Usioe! Usikubali kujidharau wewe kama mwanaume kwa kuoa mtu ambaye sio mke wako, huko ni kufanya uzinzi.

Leo nitanukuu aya za mke wa ujana wako ambaye sharti awe na bikra, bikra ndio ujana au usichana wa mwanamke, bila bikra mwanamke ni mtu mzima, hawi tena msichana(kijana wa kike) yaani ni kusema umeoa mzee wakati wasichana wapo.

Katika nukuu hii nimekoleza sehemu muhimu
Malaki 2:14- 16
14Mnauliza, “Mbona sasa hazikubali?” Mwenyezi-Mungu hazikubali kwa sababu anajua wazi kuwa umeivunja ahadi yako kwa mke wa ujana wako. Umekosa uaminifu kwake ingawa uliahidi mbele ya Mungu kwamba ungekuwa mwaminifu kwake.
15Je, Mungu hakuwafanya nyote wawili muwe mwili mmoja na roho moja? Je, alikusudia nini alipofanya hayo? Yamkini alikusudia tuzae watoto ambao watamcha yeye. Kwa hiyo, hakikisheni kuwa hakuna hata mmoja wenu anayekosa uaminifu kwa mkewe.
16Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli asema: “Ninachukia talaka. Ninachukia mmoja wenu anapomtendea mkewe ukatili huo. Hakikisheni kwamba hakuna hata mmoja wenu anayekosa uaminifu kwa mkewe.”

Mambo ya msingi
1. Usipooa mwanamke asiye na bikra Mungu hasikii maombi yako, na ukitoa bikra usimuoe mwanamke uliyembikiri pia hasikii maombi yako.
2. Mwanaume ukimtoa bikra mwanamke mnakuwa mwili mmoja na roho moja. Lakini usipotoa bikra hamuwi wamoja na ndio maana ndoa za siku hizi zinaumiza pande zote mbili
3. Mungu anachukia talaka kwa mke uliyemtoa bikra.

Kiufupi ni kuwa Mungu hamtambui mkeo kama hukumkuta na bikra, anaona mnafanya zinaa.

Usioe mwanamke asiye na Bikra, usiolewe na mwanaume ambaye hakukutoa bikra.

Jokajeusi
 
Huu ni ukweli mchungu lakini ni ngumu sana ukweli huu kuishi ndani ya karne hii ambayo maadili na malezi yameporomoka mno. Me nadhani tatzo kubwa linalochangia hii hali kwasasa ni malezi mabovu na maadili tukilitatua hili kwa asilimia kubwa itapunguza hizi kasumba za kuanza mapenz katika umri mdogo.
 
Umenena vyema,,Siku zote unaongea kweli ingawa tunakuchukulia Kama mlopokaji,,Fikilia unamuoa mwanamke aliyetolewa bikira na mwanaume mwingine,,huwa haileti maana pia ni aibu na dharau .

Alafu watu wanasema wanawake wabaya wakati wewe ndiye mbaya kwa kuchagua mwanamke malaya. Vijana wa siku hizi wengi ni maamuma
 

Mkuu Lutu aliweza kuishi na familia yake Sodoma na Gomora.

Kwenye maisha hakuna sababu ya kushindwa isipokuwa wewe mwenyewe, hata Mungu akikuhukumu hataangalia maadili ya kizazi husika bali wewe mwenyewe ndio utatoa hesabu.

Matokeo ya maisha yawe hasi na chanya hayaangalii ujumla wa jamii bali mtu mmoja mmoja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…