Maana ya Mwanamke Bikra, Kuwa na Mahusiano/Kuoa Mwanamke Bikra

Na habari ni kwamba hakuna mwanamke asiyependa kuolewa
 
Hahhahhaaa!! Endelea kujipa Moyo. Lakini ukweli upo moyoni. Ku-type hakutaathiri ukweli wowote uliomo moyoni mwako

Mkuu ngoja mimi nikusahihishe katika hiyo sentensi yako ya "endelea kujipa moyo" Mimi ni mwanamke hivyo naongea from experience, ukiona kuna mwanamke umri umeenda hajaolewa usifikiri amekosa wakumuoa, mwanamke hakosagi wakumuoa anachokosa ni machaguo yake anayoyataka/ matamanio anayoyataka kuyaona kwa mwanaume.

Ndio mwisho wa siku anaamua kukaa single, ila kama ni mtu wakuoa tu, kama nia ni kuvaa shela na pete, niamini mimi hakuna mwanamke anayekosa wakumuoa! Kama wewe si muoaji usifikiri kila mtu si muoaji mkuu.
 
Hahhahhaaa!! Endelea kujipa Moyo. Lakini ukweli upo moyoni. Ku-type hakutaathiri ukweli wowote uliomo moyoni mwako
Tatizo ni kwamba unataka watu waamini kile unachoamini ww hiv unajua kuna watu hata awe na heka kujaza dunia nzima ila bila kuwa na phd anaona hajafanya kitu ila kuna mtu hata akiwa na darasa la 3 tu lakin kwake hela ndo kila kitu na mwingine yupo radhi alale njaa ili awe na nguo nzuri lakin kuna mwingine yeye akijisitiri na ni safi kwake powa na sio kwamba hana uwezo wakununua nguo nzuri na ya gharama kubwa ila haoni umuhimu wake sasa ndo kama hapo yaani we unathamini sana hicho ila mwenzio anaona jambo la kawaida sana yaani

kuna mwenye uwezo wakuua mama ili apate hela lakini kuna mwenye yupo radhi kutoa hela zote alizonazo mama apone, hiyo ni mifano tu kuwa watu hatufanani kila mtu anakipaumbele chake,
 

Cha kwanza, Kwanini unaona umesema ukweli? Unajua maana ya ukweli? Kwanini unadhani ukweli kwako John utakuwa ni ukweli kwa Hamisi? Nihakikishie pasina shaka kuwa huu ni ukweli ili nami nianze kuwahubiria wadogo zetu ukweli huo kurescue vizazi vijavyo wasipoteze bikra zao.


Pili, Huyo mwanamke ambae unataka akutunzie bikra yake hadi hapo mtakapokutana unafahamu kuwa na yeye ana mihemko, matamanio na hisia zake, naye hutamani kufanya mapenzi, iweje ukandamize haki yake ya kimsingi yakuenjoy maisha only to satisfy your ego?
 
Sio werevu ila wenye bahati yakuitwa werevu,binafsi bado sijaoa na sijui ni mtu wa namna gani ntaoa ila bikira haiwi sababu yakumuoa bali ni sifa moja wapo tu na zingine mia zitafuata lakin kwa sababu najua sisi binadamu hatujakamilika ndo maana kuna mbaya sana,wastani,vizuri na vizuri sana,anaweza akakosa bikira afu akawa na zingine tisini na tisa afu et nimuache si ujinga huo
 


Mkuu ukweli unatoka wapi kama si kwenye misingi ya imani. Kwa misingi ya kikristo, Bikra inanguvu sana na ni kigezo kikubwa cha kumpata mke. Je unajua kuwa mwanaume anayohaki ya kumpa mwanamke talaka kama hatakuta bikra?
 
Itakuwa punda kuzaa mbwa
 
Ndo maana nimesema unarahisisha mambo, siyo kwamba wanaamua ni kwamba wako wired hivyo kwenye ubongo wao, labda nikuulize kwa nini kuna watu hawawezi kuongea kabisa ni wakimya na wengine wanaongea sana? Unaweza kuniambia ni kwa nini?
kuna sababu kama vile ulisishaji unaweza mfanya mtu awe mkimya au muongeaji na pia mwingine unakuta anapenda zaidi kusikiliza kuliko kuongea na mwingine hupenda zaidi kuonge kuliko kusikiliza na pia kuna mwingine huwa mkimya au muongeaji ni kwa sababu ya uamuzi wake tu.

nikirudi kwenye mada naona kabisa umekubali kuwa mtu kuwa na mahusiano si uamuzi wake bali kuna sababu humfanya kuwa hivo.

thanks it is over
 
Tochi ni muhimu lakin ukianza kutembea mchana umewasha tochi unamulika lazima tutakuwa na wasiwasi na akili yako otherwise unafanya komedi


Matumizi ya tochi na umuhimu wake ndio yanayosemwa hapa
 
Ukiona hivyo ujue walishaingia na kutoka au vyovyote vle....lakin kuolewa ni ndoto ya kila mwanamke.


Siyo kweli, unarahisisha sana maisha, maisha ni zaidi ya unavyoyaelewa, na siyo kila binadamu anafikiria unavyofikiria, hivi unajua kuna aina ya watu Wanawake/ Wanaume hawapendi kuwa na watoto na wanatoa kizazi kwa makusudi ili wadizae?
 
Hata kichaa huona walio wazima nao ni vichaa so kila mtu acheki kwa upande wake na akae kivyake,6 inaweza kuwa9 kulingana na ulipo


Hata aliyeiweka hiyo bikra naye alikuwa kichaa. Mada zingine zitakuvua nguo hasa ukiwa kama mwanaume
 
Tatizo lako ni moja nikuona bikira ni pointi pekee yakuwa wife materials kitu ambacho sio kweli kabisa yaani ni moja ya point tu lakin kuna zingine nyingi na unataka wengine tuelewe hivyo na kashangaa zaidi kufika hatua yakutukana wenye mawazo tofauti yako
 
Kosa la amber ni kubwa Kwan kuwa limetokea mtandaoni but wanaofanya hayo ni wengi Sana Katika jamii,Tumsaidie mkuu wa mkoa kuwang'amua watu hao katika jamii
 


Unasema sio kweli kabisa alafu unasema ni moja ya pointi. Embu tulia mkuu uandike vizuri huenda unachakusema
 


Hata kuolewa/oa pia hivyo, kuna watu wanazaliwa hivyo kwamba hawawezi kuishi na mtu na kwao kuishi wenyewe ni kawaida, hawapungikiwi na kitu, wako wired hivyo kichwani, kama vile watu wanaozaliwa wakimya pia!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…