Ng'wanangwa
Nikifa MkeWangu Asiolewe huyo mdogo wetu nadhani ana kaushamba fulani, kwa sababu kumdanganya kila msichana nitakuoa hapo anakuwa Anasema uongo. Na sijui status ya maisha ya mdogo wetu iko Vipi? Maana kama anajiweza kujihudumia kwa kila kitu basi akili ya Mwanamke na yeye akili yake huwa inawaza huyu Mwanaume ananifaa.
Zingatia ananifaa (Sio kwa ndoa lakini ila ananifaa kwa ajili ya mahusiano, showoff tu)
Lakini kiuhalisia Mwanamke wa sasa hajui ni nini anachokitaka kwa sababu asilimia kubwa ya wanawake huwa anapenda sana mahusiano ya kimapenzi kuliko ndoa.
Ushauri kwa mdogo wetu mwambie asiwe anapenda kujipendekeza kwa kutoa ahadi zisizotekelezeka. Maana ukiangalia mahusiano yake na hao mabinti naona hakuna hata mmoja wa kuoa hapo.
Lakini kama yeye anataka kuoa afanye maamuzi sio kuendelea kuwashikilia wasichana wote watatu hapo ni pagumu maana inakoelekea atajikuta anawapoteza wote hao hasa wakija kugundua wote wapo kwenye mahusiano na mtu mmoja.
Halafu la mwisho kumjua mwanamke kiundani zaidi ni lazima uwe umeshamuoa sio upo naye tu kwenye mahusiano ya kawaida. Atakuletea kila aina ya maigizo na wewe ukaamini anakufaa.
Mwambie mdogo wetu moyo wake unampenda na Unaridhika na nani kati ya hao Watatu. Baada ya hapo awe serious achukue maamuzi ya kuoa.
Awe serious tu kuwadanganya wote watatu huo ni uongo na anajipotezea muda wake na anajiingiza kwenye ma Lawama tu.