Ndoa hizi kuwa mbovumbofu hata wanaume wanachangia huo ujinga, wengi hawaeleweki kabisa, unakuta mzigo mwingi wakuangalia familia anaachiwa mama tu, yeye akinunua minyama, mchele, sijui samaki kamaliza, hajui malezi mengine yanaenda vipi, kazi yao ni kupiga umbeya na mama zao na dada zao, huku hajui mienendo ya watoto wake, siku ya siku lawama Kwa mama, wakati mtoto wa kike mlinzi wake wa kwanza ni baba, lakini utakuta na midevu yake anamsengenya mkewe Kwa ndugu zake badala yakuangalia watoto wao na mkewe.