Precious Diamond
JF-Expert Member
- Jun 9, 2023
- 593
- 1,376
Mwanaume mmoja huko Kenya aandamana kwa aina yake leo kwa kujifunga kwenye nguzo na mnyororo na kuanza kuongea kero zake.
Polisi walifika eneo la tukio na kujaribu kumfungua ili wamkamte huku watu wengine wakiwa wanarekodi tukio hilo. Polisi walipomuomba ufunguo, akasema mimi sina funguo. Kwa jinsi jamaa alivyokuwa amejifunga ilichukua muda polisi kuweza kumfungua.
Kwenye video mwanaume huyo anasema amekuja kuiambia serikari isiwanyanyase, kuwapiga, kuwaua, na kufanya waishi kwa vitisho, badala yake serikali inatakiwa kuwahudumia wananchi. Ahoji nani ameturoga Afrika, akisema uoga na ukabila ndio unafanya Afrika kuwa watumwa. Akisema kwamba muda umefika kwa Afrika kupata ukombozi wake na haogopi kitu chochote kumtokea yeye. Na hata walipoweza kumfungua na kumkamata huku wakimkokota kwenye gari, aliwaambia polisi mnachofanya ni unyanyasaji na kuendelea kusema haogopi kitu na yuko tayari kufa kwaajili ya wengine.