Maandamano ya 7/7 yaruhusiwe na Serikali na kupewa ulinzi

Hakuna anayestahili, unafikiri hao waandamanaji wangeingia barabarani na bunduki kama ambavyo ripoti ya Chande ilidanganya unafikiri askari wangapi wangeuwawa pia?
Kumbe wanafadhiliwa na CHADEMA?
 
Maria Sarungi, MangeKimambi, Heche, Gwajima, Boniface Jacob, Padre Kitima
Waliongozaje ?

Tarehe 29 October , Maria Sarungi alikua Kenya , Mange Marekani, Gwajima alikua mafichoni, Boniphace Jacob alikua kwake, Kitima alikua Kurasini pale TEC



Hebu tupe picha au video ya hao watu wakiongoza maandamano.

Msanii Davido alipokua anapinga mauaji ya polisi Nigeria kupitia kampeni ya #EndSARS mwaka 2020 alitoka Marekani alipokua anaishia kwa kipindi hicho akaingia barabarani kuongoza maandamano mitaa ya Abuja kuungana na wananchi.


View: https://youtu.be/EeuCQH0TQSY?si=wIkjaRGq6RM0fJk4
Nyie bado mnaishi kwenye propaganda mkiamini yale maandamano yalifadhiliwa na kuongozwa na CHADEMA wakati walioingia barabarani walikua na genuine concerns za kuandamana cha ajabu wakawa wanazuiwa ndio maana wakaamua kuingia kufanya maandamano na vurugu .

Barabarani walionekana vijana wasio na chama na wenye vyama kwa ufupi propaganda zenu kwenye yale maandamano zimefeli mwanzo mlisema ni wageni kutoka Kenya mara wamekodiwa kuandamana ila mkasahau hata bendera zilizokuwepo katika maandamano yale ni za Tanzania hakuna video wala picha ilionekana bendera ya CHADEMA.
 
Binafsi siamini kama kuna maandamano yoyote yatafanyika mana tofauti na kuongelewa na wanaharakati mitandaoni, hamna mahali pengine popote nimeskia mtu anaongea.

Mtu ataandamana vipi na alikua hajui chochote. Wakati huo huo kumbukumbu za oct29 bado mbichi kabisa. Sioni maandamano.
 
Ni kweli maandamno yapo kwenye mitandao ya Jamii; Twitter, Instagram, JF etc.

Kupotea njia wakati wa kwenda, siyo wakati wa kurudi.

Naamini Serikali na vyombo vyake viko kamili gado
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…