Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Maandamano yanayoambukizika ya vyuo vikuu maarufu nchini Marekani yameanza kuihofisha serikali kuu ya nchi hiyo.
Nguvu zimetumika kuwatawanya wanafunzi wa chuo kikuu cha Columbia baada ya spika wa bunge wa Marekani.bwana Johson kutembelea eneo hilo kuwataka watawanyike bila mafanikio.
Maandamano kama hayo yamekuwa yakiendelea kwenye vyuo vikoo kadhaa kikiwemo cha Yale. Kitu cha hatari zaidi maandamano na kugoma kuingia madarasani kumeanza kushuka chini mpaka kwenye vyuo vya kiufundi na vyenginevyo.
Vita vya Vietnam vilianza mwaka 1954 na kufikia mwisho mwaka 1973 kwa kushindwa kwa Marekani japo ilikuwa tayari imepeleka askari na wamarekani wengine zaidi ya milioni 3 kuikalia nchi hiyo ya Asia.
Kilichopelekea kushindwa kwa Marekani na kuondoka nchini humo ilikuwa ni upinzani mkubwa uliotokea ndani ya nchi hasa kwenye vyuo vya elimu.