Maarifa Hatari: Embu tujifunze na kumjadili huyu Shetani vizuri

Maarifa Hatari: Embu tujifunze na kumjadili huyu Shetani vizuri

Kwanza naomba mods msihamishe uzi huu kwa kuupeleka kwenye jukwaa la dini maana nataka tumjadili huyu Shetani katika misingi ya maisha yetu ya kila siku na si katika misingi ya dini.

Naileta mada hii kwa tahadhari kubwa sana. Sina nia ya kumpromote huyu jamaa ila nadhani imefika wakati tumuangalie katika uhalisia. Siwezi kuimagine dunia bila kuwa na miongozo ya maisha yenye kusisitiza upendo, amani, mshikamano na umoja kati ya wanadamu. Miongozo yote hii tumeambiwa ndiyo njia ambayo Mwenyezi Mungu anataka tupite. Shetani kwa upande mwingine tumefundishwa, mambo yake na njia zake ni potofu, ovu na zitakazopelekea uangamie katika moto wa milele. Maandiko yameenda mbali zaidi na kutuambia tajiri atapata wakati mgumu sana kuuona ufalme wa Mungu. Hili jambo ukilifirkia vizuri, linafikirisha sana.

Kutokuwa na maarifa kumeelezewa katika maandiko kuwa ni kitu hatari na kibaya, lakini pia kuwa na maarifa na kwenyewe kumehusishwa na shetani kwa sababu kunaweza kumfanya mtu kuwa na majivuno na kwamba majivuno yanakuja kabla ya maangamizi. Kwa hiyo kiufupi maandiko yame discourage sana kuwa na maarifa kutokana na sababu nyingi ambazo ukiziangalia kweli zina mashiko.

Mimi nimeanza kufikiri kuna jinsi ambayo maandiko yamepotoshwa sehemu. Upotofu unaweza kuwa kwa njia ya kuficha taarifa muhimu kuhusu mtu au kitu fulani, taarifa ambazo kama ukiwa nazo zinaweza kubadili ufahamu wako kuhusu jambo hilo. Nayasema maneno haya kwa tahadhari kubwa naomba nieleweke vizuri. Nahisi kuna watu wamehodhi maarifa haya na wanayatumia kwa ajili ya ku control watu na dunia.

Tunaishi maisha ambayo hatujijui sisi ni nani, asili yetu, nguvu zetu na hata madhaifu yetu. Wakati huo huo ufahamu wa shetani ni mdogo saaana. Ukikaa ukafikiria jinsi gani hatumjui shetani utashangaa sana. Sun Tzu aliwahi kusema ili kumshinda adui yako inabidi kwanza ujijue wewe vizuri na umjue adui yako vizuri, hapo unajiweka katika nafasi ya kushinda vita. Kama Shetani ni adui yetu namba moja kama tunavyofundishwa, nadhani tuanze kwanza kufundishana ili mimi na wewe kila mmoja wetu ajijue YEYE NI NANI na pia kuwe na mafundisho ya kutosha na deep sana kuhusu Shetani.

Uzi huu ni wa maarifa hatari. Naomba tujadili mada hii kwa staha ili wote tutoke na kitu cha kutujenga katika maisha yetu hapa duniani.
Shetani umemuumba wewe mwenyewe kwa ajili ya kutafuta mtu/kitu Cha kumpa lawama pindi unapofanya kitu kisichowapendeza wengine. Shetani kwa maana nyingine ni wewe mwenyewe
 
Okay nafikiri kuna watu wana shuhuda za kweli za matukio ya kweli ya kujichanganya na kufanya kazi na shetani ni kweli shuhuda hizi zinasisimua na kufungua macho sana. Kama unapenda story hizo nitakuelekeza wapi utazipata.
Tupia hizo shuhuda tuweze kuzichambua
 
Shetani yupo na kwa kweli kwa asili yake ni kiumbe mwenye nguvu nyingi mno kulinganisha na viumbe wengine wema na wabaya. Hata kati ya malaika shetani ni malaika wa daraja ya juu sana! Yapo madaraja 9 ya malaika (angelic hierarchies) or angelic choirs kama ifuatavyo:

Seraphims
Cherubim
Thrones
Dominions
Virtues
Powers
Principalities
Archangels
Angels

Shetani yupo katika kundi la pili la malaika yaani Cherubims (Makerubi)!!!

Kundi la pili kutoka mwisho ni malaika wakuu (archangels) mfano wao ni Michael, Gabriel na Rafael. Hawa tu wanatisha na wana nguvu za ajabu mno na hutawala juu ya makundi na makundi ya malaika!!

LAKINI USIOGOPE! Thanks to God! Shetani amefungwa sana hapo alipo yeye pamoja na malaika wenzake walioasi ambapo wengine nao ni mi-viumbe ya hatari iliyopo kwenye rank za juu sana na yenye uwezo wa kutisha!

Kwa kifupi jua kwamba Shetani na malaika zake hawajaachwa wafanye watakavyo ulimwenguni, God is in control. Pia jua kwamba pamoja na nguvu za ajabu walizopewa viumbe hawa, bado Mungu ni mkuu mno na hawezi kamwe kufananishwa hata kidogo na Maserafi (Seraphims)!!!

Sitazungumzia: Utukufu wa Mwanadamu na nafasi yake kati ya malaika. Ila Mungu asifiwe sana kwa jinsi alivyotuumba!!!

Mwisho: Jua pia kuna viumbe wengine walio pale Patakatifu pa Patakatifu juu ya majeshi ya malaika kama wale Wazee Wanne n..k. na kuna hatua zisizopimika kabla ya kumfikia boss mwenyewe; M.U.N.G.U.!!!
Mizimu iko kundi gani la malaika?
 
Katika kutimiza azma hiyo, silaha yake kubwa ni ushawishi wa hila, uongo, udanganyifu. Hupandikiza chuki baina ya mtu na mtu, taifa na taifa. Huzalisha na kueneza magonjwa.

Hutumia umaskini kuwateka na kuwatumikisha na kuwapotosha wanadamu. Husababisha ajali, majanga, na mateso kwa mwanadamu na viumbe duniani. Shetani hutenda kazi kupitia watu waovu walio mawakala wake.

Shetani huweza kukupa mafanikio kwa lengo la kukushawishi umwache Mungu na kujiweka chini ya mamlaka yake.

Ndiyo maana akamwambia Yesu angempa utajiri wote wa dunia iwapo Kristu angekubali kumsujudia.

Mwanadamu kuusalimisha utashi wake kwa Shetani, siyo lazima mpaka amsujudie kihalisia. Kile kitendo tu cha kukubali na kufanyia kazi pendekezo la Shetani, huko ni kumsujudia Shetani.

Kwa maneno mengine, mtu anapokubali kutekeleza nia na mawazo ya Shetani, hapo anakuwa mtumishi wa Shetani – anamsujudia Shetani.
Kwa hiyo kwa lugha nyingine unataka kusema shetani ni "mjinga mjinga" kiasi kwamba hawezi kufikiri kuwa njia nzuri ya kuwashawishi watu wamfuate ni kuwafanyia mazuri kwanza halafu kuwaambia wasipomsujudia atawanyang'anya mazuri hayo? Inawezekana Shetani amenyimwa uwezo huo wa kufikiri? Kuna mifano yoyote katika maandiko ya hali kama hii ya Shetani kumpa mtu mafanikio na tukaambiwa hatma yake?

Kwamba kwa kutumia mauaji, ajali, magonjwa, majanga na mateso mengine yanamfaidije katika mipango yake?
 
Ni mahadithi marefu ukitaka usikiluze mwenyewe utamjua shetani vizuri
Sawa shukrani. Nadhani watu walio "open-minded" ndiyo wana nafasi nzuri zaidi ya kumuelewa Mungu kwa kuwa hawaogopi kuutafuta ukweli. Mimi nipo hapa kuutafuta ukweli na ukweli ulio kamili kwa jinsi inavyowezekana.
 
Shetani umemuumba wewe mwenyewe kwa ajili ya kutafuta mtu/kitu Cha kumpa lawama pindi unapofanya kitu kisichowapendeza wengine. Shetani kwa maana nyingine ni wewe mwenyewe
Tujikite kwenye mada na tuepuke kunyoosheana vidole. Kama mada ni nzito sana kwako, unaweza tu kusoma ukajifunza au pita hivi ⬅️⬅️⬅️
 
Binadam huwa tunachanganya sana, sifa ya ushetani na roho (spirits).

Binadam tuna "spirit" zaidi ya moja wakati wote lakini nafsi yetu ni moja.

Mwili wetu ni jumba tu la nafsi yetu.

Soma filosofia ya maisha, topic ya "weltanschauung" kuna uwezakano utanielewa.
Nitapitia hiyo "topic" ila nina maswali. Mwili na nafsi vina tofauti gani na kazi za mwili, nafsi pamoja na roho ni nini katika ishu nzima ya uumbaji na maisha ya mwanadamu hapa duniani na mipango ya baadae?
 
Sahihi.

Sahihi.

Siyo kweli.

Umesema ^siku hizi.^ Je, alianza lini kukosa hiyo access?
Alipoasi na kutupwa nje
^Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze.^ ~ 1 Petro 5:8
Hutumia ushawishi kupitia watu na uwezo wake upo limited sana hajaachwa aranderande atakavyo.
Sahihi

Kuzimu ni nini na wapi? Unapaelewaje?
Ni hali au “mahali “ pa kiroho ambapo shetani na malaika zake huweza kuwa karibu zaidi (lakini hawa hang amani) na wanadamu na kushirikiana. Kuzimu kwa maana hii zipo nyingi ila kuzimu pia kwa aina nyingine ni makao ya shetani na malaika zake. Ni tofauti na Jehanam.
Biblia ina mashairi, mithali na hekima, historia, unabii, vielelezo ama mifano, sheria, riwaya na visa, nk.

Humo zimetumika mbinu zote za ufundi ama sanaa ya lugha (isimu) -- tamathali za semi.

Sasa lugha ya picha ni kipande kimoja tu ambacho kimehusika, na wala siyo kote, Mwanzo hadi Ufunuo.

Kwa mfano, vielelezo vya Yesu ni sehemu mojawapo ambao Biblia imetumia lugha ya picha.

Lakini sehemu za Biblia kama vile matukio ya uponyaji na huduma ya Kristu, kwa sehemu kubwa hivyo ni visa vya moja kwa moja, ambavyo humhitaji mtu ajue tu lugha rahisi husika ili avielewe.

Ni upotoshaji kulazimisha kila andiko la Biblia lisomeke kama lugha picha inayowakilisha kitu fulani kisichojulikana wazi moja kwa moja kutokana na maneno yaliyotumika kukielezea.
Hakuna aliyesema kila andiko ni lugha ya picha, ila uelewe kuwa hata matukio kama kuzaliwa kwa Yesu, kifo na ufufuko na kazi alizofanya kama uponyaji vipofu nk ni metaphors zinazoashiria na kudai upana mkubwa zaidi wa uelewa ili kujua Yesu ni nani. Yesu aliponya vipofu ndio, lakini vipofu katika muktadha mpana wa kiroho ni wale wasioona mambo ya kiroho ya Mungu, viziwi ni wale wasiosikia sauti ya Mungu, wenye ukoma ni wale wachafu kiroho nk.
 
Sawa shukrani. Nadhani watu walio "open-minded" ndiyo wana nafasi nzuri zaidi ya kumuelewa Mungu kwa kuwa hawaogopi kuutafuta ukweli. Mimi nipo hapa kuutafuta ukweli.
Safi kabisa umesema vyema OPEN MIND, ndio mwanzo wa kuujua ukweli na utaujua sana! Kama una maswali specific niulize pia fuatilia shuhuda kujua ukweli wa shetani na Mungu kwa namna ambayo Maandiko hayajachambua japo yote katika shuhuda hizi hayapingani na Maandiko.
 
Kila mahali Biblia imeonesha kwamba mwanadamu amepewa uhuru wa kuchagua, ama kumtii Mungu au kufuata utashi wa nafsi yake, kama alivyofanya Shetani.

Uamuzi wa kumtii Mungu na kuishi, au kumwasi na kuangamia, uko kwa mtu mwenyewe.

^Waambie, Kama Mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, sikufurahii kufa kwake mtu mwovu; bali aghairi mtu mwovu, na kuiacha njia yake mbaya, akaishi. Ghairini, ghairini, mkaache njia zenu mbaya.^ Ezekieli 33:11
Sawa ila kama binadamu amepewa uhuru wa kuchagua na atahukumiwa kwa maamuzi yake, je haudhani kuwa uhaba wa taarifa kuhusu adui yake unaweza kumfanya binadamu asiwe katika nafasi nzuri ya kufanya maamuzi mtambuka? Watu walioko North Korea, China au sehemu nyingi za Asia ambapo wameishi na wengine kufa wakiwa ndani ya mifumo tofauti ya kiimani, watahukumiwa vipi wakati hawakuwa na access tuliyonayo mimi na wewe ya maandiko haya?

Kama nilivyojibu kwenye swali lililopita, si kweli hata kidogo kwamba mwanadamu akiwa chini ya mamlaka ya Mungu hawezi kupata maendeleo na wala kufanikiwa.

Kinyume chake, msingi wa maendeleo na mafanikio ya mwanadamu hutegemea kujiweka kikamilifu katika usimamizi wa Muumba wake.

Maisha ya Ibrahimu, Daudi, Sulemani, na wengine wengi wacha-Mungu katika historia huthibitisha hilo pasi na shaka.

Ni kweli Shetani anaweza kumpa mtu utajiri na mafanikio (ya muda), lakini haina maana kwamba kuwa chini ya utawala wa Mungu ni kuchagua umaskini.

^Laiti wangekuwa na moyo kama huu ndani yao siku zote, wa kunicha, na kushika amri Zangu zote siku zote, wapate kufanikiwa wao na watoto wao milele!^ Kumbukumbu la Torati 5:29
Kuna mifano yoyote katika maandiko ya watu waliopata mafanikio kwa kupewa na Shetani?
 
Mizimu iko kundi gani la malaika?
Mizimu ni zile roho zilizoabudiwa kama Mungu katika jamii flani. Ni tawi la utendaji wa shetani kama ilivyo roho ya uchawi, uganga, nk Makundi yote ya malaika waovu wanahusika kupromote roho hizi kwa nafasi zao mbalimbali. Hata wanadamu maajenti wa shetani waweza kujibadilisha kwa msaada wa malaika waovu na kuoperate kama mizimu.
 
Safi kabisa umesema vyema OPEN MIND, ndio mwanzo wa kuujua ukweli na utaujua sana! Kama una maswali specific niulize pia fuatilia shuhuda kujua ukweli wa shetani na Mungu kwa namna ambayo Maandiko hayajachambua japo yote katika shuhuda hizi hayapingani na Maandiko.
Hapo juu kuna kamjadala nilifanya na Jasmoni Tegga alipotumia maandiko kusema tumeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu. Nadhani wote tunaamini maneno haya hayakumaanisha Mungu akiwa na sura na umbo la mwili wa mwanadamu, sasa kama ina maana ya mwanadamu kupewa "sifa na uwezo" wa Mungu, ni sifa zipi ambazo mwanadamu amepewa za ki-Mungu? Hili swali linaenda moja kwa moja kujibu swali mwanzoni mwa mada hii ya "MIMI NI NANI"?
 
Shetani ni dubwasha likubwa sana hata Mungu 'ameshindwa' kupambana nalo eti anaturushia sisi wanadamu tuhangaike nalo!
Ukisoma kisa cha Ayubu, tukio la anguko la Adamu na Hawa Edeni, kitabu cha Zekaria, kisha kisa cha jaribu la Yesu jangwani, pamoja na sura kadhaa za Isaya, Ezekieli na Ufunuo zenye maelezo mahususi kuhusu sababu na anguko la Shetani, ni rahisi kuona haraka kwamba kuna lengo maalumu kwa nini Ibilisi alitupwa duniani, na wala hakuangamizwa moja kwa moja baada ya kuasi mbinguni.

Tutaweza kweli? Sidhani
Shetani ni adui aliyeshindwa tayari. Kutupwa kwake kutoka mbinguni ni uthibitisho tosha juu ya hilo.

Biblia inatuambia tuzivae silaha zote za Mungu ili tumpinge Shetani. Waefeso 12:11-18.
mi sina time ya kupambana na shetani.
Haiwezekani vyovyote kumkwepa Ibilisi; ama uko upande wake au kinyume naye.

Mungu kama anatupenda atusaidie kuliangamiza tuishi vizuri.
8. Kumbukeni haya, mkajioneshe kuwa waume; jifahamisheni haya, ninyi mkosao;

9. kumbukeni mambo ya zamani za kale; maana Mimi ni Mungu, wala hapana mwingine; Mimi ni Mungu, wala hapana aliye kama Mimi;

10. nitangazaye mwisho tangu mwanzo, na tangu zamani za kale mambo yasiyotendeka bado; nikisema, Shauri Langu litasimama, Nami nitatenda mapenzi Yangu yote. ~Isaya 46
 
Hapo juu kuna kamjadala nilifanya na Jasmoni Tegga alipotumia maandiko kusema tumeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu. Nadhani wote tunaamini maneno haya hayakumaanisha Mungu akiwa na sura na umbo la mwili wa mwanadamu, sasa kama ina maana ya mwanadamu kupewa "sifa na uwezo" wa Mungu, ni sifa zipi ambazo mwanadamu amepewa za ki-Mungu? Hili swali linaenda moja kwa moja kujibu swali mwanzoni mwa mada hii ya "MIMI NI NANI"?
Tumeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu. Tunayo ile essence ya uungu ndani yetu:
Roho
Nafsi
Akili
Utashi
Mamlaka
Uhuru (free will)

Malaika wana vyote hivyo isipokuwa kimojawapo kati ya hivyo! Jambo hili humfanya binadamu kuwa fumbo sio kati ya binadamu wenzake tu bali kati ya malaika pia!
 
Nukta ya msingi ni kwamba pamoja na uwezo mkubwa alio nao Shetani, bado hajaachwa kufanya atakavvyo 100%.

Kwa hiyo nguvu zake zimewekewa mipaka, na anatenda kile tu ambacho Mungu ameruhusu, na wala si zaidi ya hapo.
Kuvamia nchi nyingine kupora ardhi na kuua raia wasio na hatia ni ushetani??
 
Ukisoma kisa cha Ayubu, tukio la anguko la Adamu na Hawa Edeni, kitabu cha Zekaria, kisha kisha cha jaribu la Yesu jangwani, pamoja na sura kadhaa za Isaya, Ezekieli na Ufunuo zenye maelezo mahususi kuhusu sababu na anguko la Shetani, ni rahisi kuona haraka kwamba kuna lengo maalumu kwa nini Ibilisi alitupwa duniani, na wala hakuangamizwa moja kwa moja baada ya kuasi mbinguni.


Shetani ni adui aliyeshindwa tayari. Kutupwa kwake kutoka mbinguni ni uthibitisho tosha juu ya hilo.

Biblia inatuambia tuzivae silaha zote za Mungu ili tumpinge Shetani. Waefeso 12:11-18.

Haiwezekani vyovyote kumkwepa Ibilisi; ama uko upande wake au kinyume naye.


8. Kumbukeni haya, mkajioneshe kuwa waume; jifahamisheni haya, ninyi mkosao;

9. kumbukeni mambo ya zamani za kale; maana Mimi ni Mungu, wala hapana mwingine; Mimi ni Mungu, wala hapana aliye kama Mimi;

10. nitangazaye mwisho tangu mwanzo, na tangu zamani za kale mambo yasiyotendeka bado; nikisema, Shauri Langu litasimama, Nami nitatenda mapenzi Yangu yote. ~Isaya 46
Mungu amejua kututesa Kwa kweli. Ye aliangamize tu.
 
Alafu unawasikia wajinga siku za ibada wakiomba eti wanamkemea shetani na kumkanyaga
Nachelea kusema andiko lako hili limejaa upotoshaji mwingi sana ambao haupaswi kupuuzwa. Kwa bahati mbaya hujataja chanzo cha taarifa zako ni kipi.

Maana ni wazi umedai haumo kwenye Uislamu wala katika Ukristo. Je, umeoteshwa labda?
Kerubi sio malaika, maserafi sio malaika
Maserafi (Isaya 6:1-7) na makerubi (Mwanzo 3:24; Zaburi 80:1), hawa wote ni malaika. Malaika wema ni watumishi wa Mungu; wao wanaitwa pia watakatifu, wahudumu, nyota, wana wa Mungu, wajumbe wa mbinguni, nk.

Pia Biblia humtaja Mikaeli, malaika mkuu (Yuda 1:9) na Gabrieli, ^nisimamaye mbele za Mungu^ (Luka 1:19). ^Je, hao wote si roho watumikao, wakitumwa kuwahudumu wale watakaourithi wokovu?^ Ebrania 1:14.

Malaika waovu, malaika wabaya, mapepo, pepo wachafu, majini, majeshi wa kiroho waovu, mashetani, malaika wa Shetani (Marko 1:21-27; Luka 10:17-18).

Baada ya kuja dunian, Shetan alishawishi baadhi ya wafuasi wake (malaika) kufanya unajisi wa Uzao wa viumbe vya dunian kwa kushiriki uzazi baina ya viumbe wa kimbingu (malaika) na viumbe wa dunia wakiwepo binadamu, wanyama, wadudu ndipo likaibuka kundi la uzao chotara ambao bible zenu zinawaita Nephilims/giants, chotara hawa ndio chanzo cha uzao wa viumbe wapya wa kiroho waitwao Mapepo/majini maana hawa ndio kundi la mwisho la uzao wa viumbe wa kiroho.
Uongo mkubwa, malaika hawazaliani. Mathayo 22:30

maana roho haifi bali mwili
^Msiwaogope wauuao mwili, wasiweze kuiua na roho; afadhali mwogopeni Yule awezaye kuangamiza mwili na roho pia katika jehanamu.^ ~Mathayo 10:28

Na kwa level zetu wanadamu viumbe tunaoshindana nao ni mapepo yaan jeshi la shetan la cheo kidogo
^Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.^ ~Waefeso 6:12

^Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia.^ ~Yakobo 4:7

mambo ya kiroho yanakwenda kwa utaratibu, huwezi kumpambanisha kiumbe mwenye nguvu kubwa zaidi kuliko mpinzani wake
Kwa hiyo unavyofikiri, wadhani vita vya kiroho ni kama mechi au mashindano fulani ya kirafiki, ambapo adui anaonewa huruma?

^Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze.^ ~1 Petro 5:8

ndio maana mpaka sasa Shetan hawezi kuja duniani kushindana na viumbe dhaifu wanadamu
^Ole wa nchi na bahari! Kwa maana yule Ibilisi ameshuka kwenu mwenye ghadhabu nyingi, akijua ya kuwa ana wakati mchache tu.^ ~Ufunuo wa Yohana 12:12
Baada ya kuja dunian, Shetan alishawishi baadhi ya wafuasi wake (malaika) kufanya unajisi
ndipo uje ushindane na kundi la malaika ambao shetani alishuka nao
Umedai hapo juu kwamba ^Shetani hawezi kuja duniani.^

Lakini hapa umeandika kinyume chake, kwamba Shetani alikuja duniani, alishuka pamoja na malaika wake.

Tushike lipi???
 
Back
Top Bottom