Alafu unawasikia wajinga siku za ibada wakiomba eti wanamkemea shetani na kumkanyaga
Nachelea kusema andiko lako hili limejaa upotoshaji mwingi sana ambao haupaswi kupuuzwa. Kwa bahati mbaya hujataja chanzo cha taarifa zako ni kipi.
Maana ni wazi umedai haumo kwenye Uislamu wala katika Ukristo. Je, umeoteshwa labda?
Kerubi sio malaika, maserafi sio malaika
Maserafi (Isaya 6:1-7) na makerubi (Mwanzo 3:24; Zaburi 80:1), hawa wote ni malaika. Malaika wema ni watumishi wa Mungu; wao wanaitwa pia watakatifu, wahudumu, nyota, wana wa Mungu, wajumbe wa mbinguni, nk.
Pia Biblia humtaja Mikaeli, malaika mkuu (Yuda 1:9) na Gabrieli, ^nisimamaye mbele za Mungu^ (Luka 1:19). ^Je, hao wote si roho watumikao, wakitumwa kuwahudumu wale watakaourithi wokovu?^ Ebrania 1:14.
Malaika waovu, malaika wabaya, mapepo, pepo wachafu, majini, majeshi wa kiroho waovu, mashetani, malaika wa Shetani (Marko 1:21-27; Luka 10:17-18).
Baada ya kuja dunian, Shetan alishawishi baadhi ya wafuasi wake (malaika) kufanya unajisi wa Uzao wa viumbe vya dunian kwa kushiriki uzazi baina ya viumbe wa kimbingu (malaika) na viumbe wa dunia wakiwepo binadamu, wanyama, wadudu ndipo likaibuka kundi la uzao chotara ambao bible zenu zinawaita Nephilims/giants, chotara hawa ndio chanzo cha uzao wa viumbe wapya wa kiroho waitwao Mapepo/majini maana hawa ndio kundi la mwisho la uzao wa viumbe wa kiroho.
Uongo mkubwa, malaika hawazaliani. Mathayo 22:30
maana roho haifi bali mwili
^Msiwaogope wauuao mwili, wasiweze kuiua na roho; afadhali mwogopeni Yule awezaye kuangamiza
mwili na roho pia katika jehanamu.^ ~Mathayo 10:28
Na kwa level zetu wanadamu viumbe tunaoshindana nao ni mapepo yaan jeshi la shetan la cheo kidogo
^Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya
falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.^ ~Waefeso 6:12
^Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani,
naye atawakimbia.^ ~Yakobo 4:7
mambo ya kiroho yanakwenda kwa utaratibu, huwezi kumpambanisha kiumbe mwenye nguvu kubwa zaidi kuliko mpinzani wake
Kwa hiyo unavyofikiri, wadhani vita vya kiroho ni kama mechi au mashindano fulani ya kirafiki, ambapo adui anaonewa huruma?
^Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu
Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze.^ ~1 Petro 5:8
ndio maana mpaka sasa Shetan hawezi kuja duniani kushindana na viumbe dhaifu wanadamu
^Ole wa nchi na bahari! Kwa maana yule Ibilisi ameshuka kwenu mwenye ghadhabu nyingi, akijua ya kuwa ana wakati mchache tu.^ ~Ufunuo wa Yohana 12:12
Baada ya kuja dunian, Shetan alishawishi baadhi ya wafuasi wake (malaika) kufanya unajisi
ndipo uje ushindane na kundi la malaika ambao shetani alishuka nao
Umedai hapo juu kwamba ^Shetani hawezi kuja duniani.^
Lakini hapa umeandika kinyume chake, kwamba Shetani alikuja duniani, alishuka pamoja na malaika wake.
Tushike lipi???