Maaskofu Katoliki acheni kuunga mkono bomba la mafuta. Nchi za zilizoendelea zinaondokana na matumizi ya mafuta sisi ndio tunataka kuanza kuyachimba!

Ninaandika kwa mara nyingine kuhusu jambo hili ambalo wengi wenu hamtapenda kulisikia. Naandika kama mzalendo kwa nchi yangu Tanzania na sina interest nyingine yoyote kibiashara katika jambo hili. Naandika kwa kifupi tu hapa.

Ukweli ni kwamba dunia inakwenda kwa kasi sana. Mambo ya climate change sasa ni dhahiri na nchi zilizoendelea zimeonesha nia thabiti ya kuachana na mafuta ya miambani (fossil fuels) ambayo huchafua hewa na mazingira na kusababisha kuongezeka kwa joto na madhara ambatanishi.

Baadhi ya nchi za Ulaya kama Norway magari ya umeme yanazidi yale ya petrol/dizel na lengo ni kuondoa magari yatumiayo mafuta ifikapo 2030. Lengo hili limewekwa na nchi nyingi za Ulaya. China inaongoza kwa wingi wa magari ya umeme duniani ikiwa na magari milioni 7, ikifuatiwa na USA 2 milion na Germany 1.3 milioni.

Ukiangalia tunakokwenda utagundua kuwa future ya magari na mafuta ni fupi sana na sio zaidi ya miaka kumi kutoka sasa magari ya mafuta yatakuwa machache kuliko ya umeme duniani kote na hivyo soko la mafuta litaanguka.

Ndio kusema uwekezaji mkubwa ambao Tanzania na Uganda wanauweka kwenye bomba la mafuta ni upotevu wa fedha za maskini wa nchi hizi. Nani anawashauri viongozi wa nchi hizi?! Maaskofu katoliki acheni kuunga mkono msilolijua! Fuatilieni mambo yanayoendelea katika ulimwengu wa technologia ya engine za umeme na hydrogen, la sivyo mnachangia kuwafukarisha watanzania!

Nina uhakika bomba la mafuta la Hoima-Tanga litakuja kutumia kusafirisha maji ya kumwagilia kutoka ziwa Victoria na sio mafuta.
Kalale.
 
Hivi wewe upo sawasawa kweli? Matumizi ya mafuta hayataisha hata siku moja, Wewe unajifanya mwana mazingira wakati hujui unachofanya
Kwa watu mnaofuatilia Yanga na Simba tu hamwezi kuelewa jambo hili.
Hakika uongo ukirudiwa mara nyingi huonekana ukweli. Hivi umewahi kujiuliza hizo nchi zinazopigia kelele hilo Bomba la mafuta mbona wao ndiyo wanaoongoza kwa kusafirisha mafuta na gas kwa njia hiyo hiyo?
Yaani ni kama wao kutuambia viwanda vinaongeza joto Duniani lakini wao kila siku wanaongoza kutengeneza viwanda na haitoshi wanashindana kutengeza WMD's kwaajili ya kumwangamiza huyo huyo Binadamu ambaye wanajifanya wanamlinda dhidi ya uharibifu wa Mazingira.
Amka Mkuu hakuna anayependa Africa iinuke na kujitegemea kwakuwa ndiyo soko kuu la bidhaa zao na huduma
Hujui yanayoendelea duniani na sio rahisi kwa mtu anayebeti tu kila siku.
 
Battery yeyote inahitaji replacement iwe ya simu ,ya gari nk

Battery ya gari ya umeme ku replace inategemea aina ya gari bei.ya chini kabisa kwa vigari vidogo ni dollar 5000 sawa na milioni kumi na moja za Tanzania na juu ni dola elfu ishirini sawa na kama milioni 45 za Tanzania

Maana yake nini huko mbeleni tukiruhusu hayo magari ya umeme yawe ndio pekee pesa zetu za kigeni zote zaweza.ishia kununua betri tu za magari

Kwa taarifa hiyo ni moja ya factor watu Tanzania hata matajiri wakubwa hawaagizi hayo magari ya umeme

Sababu kitu kingine yanakula sana umeme na muda wa kuchaji ni mrefu sana iwe nyumbani au kituo cha kujazia tofauti na mafuta
Mfano Kuchaji charger ya kawaida nyumbani kwako waweza hitaji kuchaji hadi masaa nane hadi 12 kujaza full kutegemeana na aina ya charger uliyonayo bei za chini ni laki 8 za juu nzuri ni milioni tano za Tanzania sababu hilo.betri ni rechargeable kama la simu tu na likiwa full utatembelea kilomita 250 unatakiwa uchaji tena

Hata ukiwa na fast charger uwe mtulivu hadi ifikie full usubiri walau saa moja na umeme linaokula mwingi lazima uamkie shikamoo bill ya umeme

Umeme wa Tanzania na nchi nyingi Afrika bado mdogo hautoshelezi mahitaji sembuse wa kutosha magari ya umeme wakati viwandani tu bado hautoshi

Mafuta yataendelea kuwepo muda mrefu

Huwezi endesha kiwanda kwa kutumia umeme wa betri ya gari

Mafuta yanaendelea kuwepo tu
Ndio technology inashika kasi. Wakati simu zinaaingia mwishoni mwa 90s wengi tulifikiri zitakuwa kwa matajiri tu na tena wakati smart phone zinaingia tulifikiri matajiri tu watamiliki smart phones. Unaonaje sasa?
 
Kweli adui wa mtu mweusi ni mtu mweusi aisee yani unalipwa kuja kuandika pointless kiasi hiki na wewe unakubali tuu
 
Kwa watu mnaofuatilia Yanga na Simba tu hamwezi kuelewa jambo hili.

Hujui yanayoendelea duniani na sio rahisi kwa mtu anayebeti tu kila siku.
Mkuu wewe unayejua yanayoendelea Duniani hujui Race ya utengenezaji wa WMD's unaofanywa na mataifa ya Ulaya na Marekani?
Unadhani silahi hizo zinatengenezwa ili kumuangamiza nani kama sio Binadamu huyu huyu ambaye wanatulaghai kuwa Wanamlinda dhidi ya athari za Mazingira? Au unadhani hizo silaha zinatengenezwa ili zikatumike kuwaangamiza viumbe wa sayari ya Mars?
Hapo bado sijaongelea biological weapons wanazoziunda na wewe ukaaminishwa kweli haya majamaa yanajali ustawi wa Binadamu.
 
Ndio technology inashika kasi. Wakati simu zinaaingia mwishoni mwa 90s wengi tulifikiri zitakuwa kwa matajiri tu na tena wakati smart phone zinaingia tulifikiri matajiri tu watamiliki smart phones. Unaonaje sasa?
Unachoongea kwa magari ni hallucinations
Betri za hizo gari za umeme ni issue kubwa na hawajapata ufumbuzi
 
Mkuu wewe unayejua yanayoendelea Duniani hujui Race ya utengenezaji wa WMD's unaofanywa na mataifa ya Ulaya na Marekani?
Unadhani silahi hizo zinatengenezwa ili kumuangamiza nani kama sio Binadamu huyu huyu ambaye wanatulaghai kuwa Wanamlinda dhidi ya athari za Mazingira? Au unadhani hizo silaha zinatengenezwa ili zikatumike kuwaangamiza viumbe wa sayari ya Mars?
Hapo bado sijaongelea biological weapons wanazoziunda na wewe ukaaminishwa kweli haya majamaa yanajali ustawi wa Binadamu.
Wazungu wangekuwa na ajenda ya kitaifa ya kuwaangamiza waafrika wangeshawamaliza enzi za utumwa au ukoloni, walikuwa nauwezo wote tena bila kulauniwa na mataifa mengine. Tatizo lenu mnadanganywa sana mambo mengi.
 
Ninaandika kwa mara nyingine kuhusu jambo hili ambalo wengi wenu hamtapenda kulisikia. Naandika kama mzalendo kwa nchi yangu Tanzania na sina interest nyingine yoyote kibiashara katika jambo hili. Naandika kwa kifupi tu hapa.

Ukweli ni kwamba dunia inakwenda kwa kasi sana. Mambo ya climate change sasa ni dhahiri na nchi zilizoendelea zimeonesha nia thabiti ya kuachana na mafuta ya miambani (fossil fuels) ambayo huchafua hewa na mazingira na kusababisha kuongezeka kwa joto na madhara ambatanishi.

Baadhi ya nchi za Ulaya kama Norway magari ya umeme yanazidi yale ya petrol/dizel na lengo ni kuondoa magari yatumiayo mafuta ifikapo 2030. Lengo hili limewekwa na nchi nyingi za Ulaya. China inaongoza kwa wingi wa magari ya umeme duniani ikiwa na magari milioni 7, ikifuatiwa na USA 2 milion na Germany 1.3 milioni.

Ukiangalia tunakokwenda utagundua kuwa future ya magari na mafuta ni fupi sana na sio zaidi ya miaka kumi kutoka sasa magari ya mafuta yatakuwa machache kuliko ya umeme duniani kote na hivyo soko la mafuta litaanguka.

Ndio kusema uwekezaji mkubwa ambao Tanzania na Uganda wanauweka kwenye bomba la mafuta ni upotevu wa fedha za maskini wa nchi hizi. Nani anawashauri viongozi wa nchi hizi?! Maaskofu katoliki acheni kuunga mkono msilolijua! Fuatilieni mambo yanayoendelea katika ulimwengu wa technologia ya engine za umeme na hydrogen, la sivyo mnachangia kuwafukarisha watanzania!

Nina uhakika bomba la mafuta la Hoima-Tanga litakuja kutumia kusafirisha maji ya kumwagilia kutoka ziwa Victoria na sio mafuta.
NApata wakati mgumu kidogo kukuelewa na sia ajabu upo brainwashed kidogi na suala la mazingira.

Ninavyoandika nchi nyingi za ulaya ikiwa ni pamoja ufaransa Ujerumani wamerudi kwenye coal na bado wanatumia coal kwenye viwanda vikubwa pamoja na kwamba chanzo hiki cha nishati kinachafua zaidi mazingira. Dunia ina gas, ina umeme, ina solar lakini bado wapo kwenye makaa ya mawe.

Hii tafsi yake ni nini mafuta yataendelea kutumika kwa sana miaka 50 ijayo kama ilivyo kwenye makaa ya mawe.

Kuna kitu kinaitwa factor endowment, ulaya hakuna jua lililopo Africa, baridi iliyopo Ulaya haipo Africa, hivyo hivyo kwenye vyanzo vya nishati ambako kunapelekea kutegemeana hivyo. Hata yangetenezwa magari mengi kiasi gani bado kuna ambao watahitaji mafuta kwa ajili ya magari kwa sababu hawana jua la kutosha.

Pili bado kuna mitambo inahitaji kuendeshwa kwa nguvu kubwa na nishati pekee kwa sasa ni oil. Mfano meli zote.

Kwa ufupi mafuta bado yapo sana. Pili tambua hii ni propaganda ya kutaka nchi zinazoendelea kutokuendelea kwa kisingizio cha mazingira. Naishia hapo
 
Wazungu wangekuwa na ajenda ya kitaifa ya kuwaangamiza waafrika wangeshawamaliza enzi za utumwa au ukoloni, walikuwa nauwezo wote tena bila kulauniwa na mataifa mengine. Tatizo lenu mnadanganywa sana mambo mengi.
Ukiona mtu anaongea hivi ujue amefikia ukomo wa kufikiri. Unadhani hilo inalowaza ni rahisi kutokea kiasi hicho?
Hawawezi kutuangamiza kwakuwa sisi ndiyo soko lao wanalolitegemea wanachokifanya ni kutujaza ujinga kama walivyofanikiwa kwako mtoa mada ili kufanya urahisi wa kupora hizo rasilimali za Afrika na pia kutufanya tuwe wategemezi wa kila kitu ili kujihakikishia soko la bidhaa na huduma zao.
Ndiyo maana mapambano yao yote ni kuhakikisha tunaendelea kubaki gizani kuwarahisishia mahitaji yao.
Amka Mkuu usije ukakojoa kitandani, hawa jamaa usidhani watafanya kitu kwako kwakuwa wanakupenda.
 
U

ji ni mmbaya sana wewe unajua yanayoendelea kuhusu renewable energy na mataifa tajiri yamefika wapi na wamedhamiria nini kwenye timescale yao? Nafahamu ndio maana naandika haya, vinginevyo tusubiri miaka michache is ijayo wakati tulishapata hasara. Nilizungumza kuhusu biashara ya ndege miaka kadhaa iliyopita na watu walubeza ila jipangeni kusikia habari za hasara hadi mwisho.
 
Ninavyoandika nchi nyingi za ulaya ikiwa ni pamoja ufaransa Ujerumani wamerudi kwenye coal na bado wanatumia coal kwenye viwanda vikubwa pamoja na kwamba chanzo hiki cha nishati kinachafua zaidi mazingira. Dunia ina gas, ina umeme, ina solar lakini bado wapo kwenye makaa ya mawe.
Wanatumia coal wakati wa baridi kuzalisha umeme mwingi zaidi ila kwa mfano mwaka jana Scotland walitumia umeme wa upepo pekee wakati wa summer na wana mpango madhubuti wa kuondokana na fossil fuels very soon.
 
Ninaandika kwa mara nyingine kuhusu jambo hili ambalo wengi wenu hamtapenda kulisikia. Naandika kama mzalendo kwa nchi yangu Tanzania na sina interest nyingine yoyote kibiashara katika jambo hili. Naandika kwa kifupi tu hapa.

Ukweli ni kwamba dunia inakwenda kwa kasi sana. Mambo ya climate change sasa ni dhahiri na nchi zilizoendelea zimeonesha nia thabiti ya kuachana na mafuta ya miambani (fossil fuels) ambayo huchafua hewa na mazingira na kusababisha kuongezeka kwa joto na madhara ambatanishi.

Baadhi ya nchi za Ulaya kama Norway magari ya umeme yanazidi yale ya petrol/dizel na lengo ni kuondoa magari yatumiayo mafuta ifikapo 2030. Lengo hili limewekwa na nchi nyingi za Ulaya. China inaongoza kwa wingi wa magari ya umeme duniani ikiwa na magari milioni 7, ikifuatiwa na USA 2 milion na Germany 1.3 milioni.

Ukiangalia tunakokwenda utagundua kuwa future ya magari na mafuta ni fupi sana na sio zaidi ya miaka kumi kutoka sasa magari ya mafuta yatakuwa machache kuliko ya umeme duniani kote na hivyo soko la mafuta litaanguka.

Ndio kusema uwekezaji mkubwa ambao Tanzania na Uganda wanauweka kwenye bomba la mafuta ni upotevu wa fedha za maskini wa nchi hizi. Nani anawashauri viongozi wa nchi hizi?! Maaskofu katoliki acheni kuunga mkono msilolijua! Fuatilieni mambo yanayoendelea katika ulimwengu wa technologia ya engine za umeme na hydrogen, la sivyo mnachangia kuwafukarisha watanzania!

Nina uhakika bomba la mafuta la Hoima-Tanga litakuja kutumia kusafirisha maji ya kumwagilia kutoka ziwa Victoria na sio mafuta.
1. Wewe ni muathirika wa propaganda mkuu si kweli kwamba magari ya umeme ni mazuri kwa mazingira, gari la umeme linakua Zuri kwa mazingira pale tu source ya umeme ikiwa ni upepo ama solar etc. Ila Nchi nyingi source za umeme ni Nuclear, mafuta, makaa ya mawe na Fossil nyengine, kuna Study mbalimbali zinaonesha Magari ya umeme yanaweza kuwa na madhara kuliko ya Mafuta.

2. Battery za Magari zinatoka mazingira mabovu na wanatumia Kemikali nyingi ambazo sio rafiki wa Dunia kuzitengeneza. Kila Tani moja ya lithium/Cobalt/nickel inayotengenezwa kuna Tani 75 za uchafu zinamwagwa za Acid na Tani moja ya radioactive materials

3. Kuna material ya batery sio renewable nayo ni uchafu wa kemikali unarudi ardhini

Material mengi yanatoka Africa na hali ya hao wanayoyachimba ni mbaya mno. Watoto wadogo wanachimba Congo, wengine wanakufa, wengine wanapata magonjwa ya ajabu ajabu.

Bottom line kutengeneza Gari la umeme linalotunza mazingira ni ngumu sana, Vi nchi vidogo visivyo na demand maybe ila ma Nchi makubwa kama Usa na China wanaharibu mazingira na magari ya umeme kuliko Mafuta.

Na sisi Kama Nchi vyema tuangalie Maslahi yetu hao wazungu ni wajanja sana waishatumia kitu fulani kupata maendeleo huwa wataanzisha chokochoko kisitumike ili wengine wasiendelee, tunahitaji source za umeme nyingi kadri iwezekanavyo, nchi bado changa sana hii
 
Nafahamu yote hayo na source ya umeme zinazoendelezwa ili kupata umeme wa kutumia kwenye magari ni umeme wa upepo, solar, geothermal nk.
2. Battery za Magari zinatoka mazingira mabovu na wanatumia Kemikali nyingi ambazo sio rafiki wa Dunia kuzitengeneza. Kila Tani moja ya lithium/Cobalt/nickel inayotengenezwa kuna Tani 75 za uchafu zinamwagwa za Acid na Tani moja ya radioactive materials
Ndio ila kuna development kubwa kwenye kuingiza chemicals nyingine zilizo less polluting or cheaper na maendeleo ni mazuri.
3. Kuna material ya batery sio renewable nayo ni uchafu wa kemikali unarudi ardhini
Recyclable batteries zinaendelea kuvumbuliwa.
Material mengi yanatoka Africa na hali ya hao wanayoyachimba ni mbaya mno. Watoto wadogo wanachimba Congo, wengine wanakufa, wengine wanapata magonjwa ya ajabu ajabu.
Kuna deposits nyingi tu zinagunduliwa hata juzi tu waligundua potential kubwa in lower Kilimanjaro.
Bottom line kutengeneza Gari la umeme linalotunza mazingira ni ngumu sana, Vi nchi vidogo visivyo na demand maybe ila ma Nchi makubwa kama Usa na China wanaharibu mazingira na magari ya umeme kuliko Mafuta.
Technology ya battery ni commercially driven na kuna funding nyingi na projects nyingi tu zilizo promising within 5 years.
Na sisi Kama Nchi vyema tuangalie Maslahi yetu hao wazungu ni wajanja sana waishatumia kitu fulani kupata maendeleo huwa wataanzisha chokochoko kisitumike ili wengine wasiendelee, tunahitaji source za umeme nyingi kadri iwezekanavyo, nchi bado changa sana hii
Kweli nakuambia hatutatumia bomba la mafuta kwa muda mrefu kabla mafuta kupigwa marufuku au kukosa masoko ya kuuza mafuta. Dunia inakwenda mbio sana si umeona cell phone revolution just 15 years ago nikiangalia mimi kumiliki simu ya mkonge ilikuwa ndoto leo kila mtu anapangusa.
 
Ninaandika kwa mara nyingine kuhusu jambo hili ambalo wengi wenu hamtapenda kulisikia. Naandika kama mzalendo kwa nchi yangu Tanzania na sina interest nyingine yoyote kibiashara katika jambo hili. Naandika kwa kifupi tu hapa.

Ukweli ni kwamba dunia inakwenda kwa kasi sana. Mambo ya climate change sasa ni dhahiri na nchi zilizoendelea zimeonesha nia thabiti ya kuachana na mafuta ya miambani (fossil fuels) ambayo huchafua hewa na mazingira na kusababisha kuongezeka kwa joto na madhara ambatanishi.

Baadhi ya nchi za Ulaya kama Norway magari ya umeme yanazidi yale ya petrol/dizel na lengo ni kuondoa magari yatumiayo mafuta ifikapo 2030. Lengo hili limewekwa na nchi nyingi za Ulaya. China inaongoza kwa wingi wa magari ya umeme duniani ikiwa na magari milioni 7, ikifuatiwa na USA 2 milion na Germany 1.3 milioni.

Ukiangalia tunakokwenda utagundua kuwa future ya magari na mafuta ni fupi sana na sio zaidi ya miaka kumi kutoka sasa magari ya mafuta yatakuwa machache kuliko ya umeme duniani kote na hivyo soko la mafuta litaanguka.

Ndio kusema uwekezaji mkubwa ambao Tanzania na Uganda wanauweka kwenye bomba la mafuta ni upotevu wa fedha za maskini wa nchi hizi. Nani anawashauri viongozi wa nchi hizi?! Maaskofu katoliki acheni kuunga mkono msilolijua! Fuatilieni mambo yanayoendelea katika ulimwengu wa technologia ya engine za umeme na hydrogen, la sivyo mnachangia kuwafukarisha watanzania!

Nina uhakika bomba la mafuta la Hoima-Tanga litakuja kutumia kusafirisha maji ya kumwagilia kutoka ziwa Victoria na sio mafuta.
Za kuambiwa changanya na zako. Mafuta bado yatatumika kwa miaka mingi sana.
Idadi uliyoweka ingekuwa kwa % ingeeleweka zaidi. Mafuta bado ni utajiri duniani kwa kuwa yanahitajika sana.
Bomba la mafuta linawekwa na makampuni ya nje (TOTAL ikiwa mmiliki mkubwa ), Tanzania na Uganda zikiwa na umiliki mdogo (minor share holders).
Unapojadili hili bomba na teknolojia ya engine za umeme, uliangalie kwa uono mpana.
 
Technology inakwenda kasi kuliko estimations hata za wanasayansi wenyewe. Estimations nyingi zinaonesha by 2040 (about 15 years from now) magari ya petroleum yatakuwa bidhaa adimu. Soma andiko moja hapa:

What year will everyone be driving electric cars?
It is predicted that in 2025, 20% of all new global car sales will be electric, in 2030 this will jump to 40%. By 2040, mostly all cars sold across the world will be electric, according to forecasting by investment bank UBS.
 
Back
Top Bottom