Ninaandika kwa mara nyingine kuhusu jambo hili ambalo wengi wenu hamtapenda kulisikia. Naandika kama mzalendo kwa nchi yangu Tanzania na sina interest nyingine yoyote kibiashara katika jambo hili. Naandika kwa kifupi tu hapa.
Ukweli ni kwamba dunia inakwenda kwa kasi sana. Mambo ya climate change sasa ni dhahiri na nchi zilizoendelea zimeonesha nia thabiti ya kuachana na mafuta ya miambani (fossil fuels) ambayo huchafua hewa na mazingira na kusababisha kuongezeka kwa joto na madhara ambatanishi.
Baadhi ya nchi za Ulaya kama Norway magari ya umeme yanazidi yale ya petrol/dizel na lengo ni kuondoa magari yatumiayo mafuta ifikapo 2030. Lengo hili limewekwa na nchi nyingi za Ulaya. China inaongoza kwa wingi wa magari ya umeme duniani ikiwa na magari milioni 7, ikifuatiwa na USA 2 milion na Germany 1.3 milioni.
Ukiangalia tunakokwenda utagundua kuwa future ya magari na mafuta ni fupi sana na sio zaidi ya miaka kumi kutoka sasa magari ya mafuta yatakuwa machache kuliko ya umeme duniani kote na hivyo soko la mafuta litaanguka.
Ndio kusema uwekezaji mkubwa ambao Tanzania na Uganda wanauweka kwenye bomba la mafuta ni upotevu wa fedha za maskini wa nchi hizi. Nani anawashauri viongozi wa nchi hizi?! Maaskofu katoliki acheni kuunga mkono msilolijua! Fuatilieni mambo yanayoendelea katika ulimwengu wa technologia ya engine za umeme na hydrogen, la sivyo mnachangia kuwafukarisha watanzania!
Nina uhakika bomba la mafuta la Hoima-Tanga litakuja kutumia kusafirisha maji ya kumwagilia kutoka ziwa Victoria na sio mafuta.
1. Wewe ni muathirika wa propaganda mkuu si kweli kwamba magari ya umeme ni mazuri kwa mazingira, gari la umeme linakua Zuri kwa mazingira pale tu source ya umeme ikiwa ni upepo ama solar etc. Ila Nchi nyingi source za umeme ni Nuclear, mafuta, makaa ya mawe na Fossil nyengine, kuna Study mbalimbali zinaonesha Magari ya umeme yanaweza kuwa na madhara kuliko ya Mafuta.
2. Battery za Magari zinatoka mazingira mabovu na wanatumia Kemikali nyingi ambazo sio rafiki wa Dunia kuzitengeneza. Kila Tani moja ya lithium/Cobalt/nickel inayotengenezwa kuna Tani 75 za uchafu zinamwagwa za Acid na Tani moja ya radioactive materials
3. Kuna material ya batery sio renewable nayo ni uchafu wa kemikali unarudi ardhini
Material mengi yanatoka Africa na hali ya hao wanayoyachimba ni mbaya mno. Watoto wadogo wanachimba Congo, wengine wanakufa, wengine wanapata magonjwa ya ajabu ajabu.
Bottom line kutengeneza Gari la umeme linalotunza mazingira ni ngumu sana, Vi nchi vidogo visivyo na demand maybe ila ma Nchi makubwa kama Usa na China wanaharibu mazingira na magari ya umeme kuliko Mafuta.
Na sisi Kama Nchi vyema tuangalie Maslahi yetu hao wazungu ni wajanja sana waishatumia kitu fulani kupata maendeleo huwa wataanzisha chokochoko kisitumike ili wengine wasiendelee, tunahitaji source za umeme nyingi kadri iwezekanavyo, nchi bado changa sana hii