Nadhani kuna watu wamekumbwa na uwendawazimu wa itikadi za kivyama.
Tatizo la watu kupigwa lisitazamwe kwa fikra duni za uhayawani wa ushabiki wa kivyama, bali litazamwe kwa hekima iliyo ya kweli.
Umtazame Halima Mdee na Bulaya na wengine, kama Watanzania. Kisha tujiulize:
1) Hawa walioumizwa walitenda kosa gani?
2) Kama kuna kosa walilolitenda, kosa hilo linastahili adhabu?
3) Kama walitenda kosa linalostahili adhabu, ni nani mwenye haki za kisheria kutoa adhabu? Ni Polisi, ni mahakama au ni magereza?
4) Kama walitenda kosa, ni hatua gani zilistahili kuchukuliwa? Ni kuvunjwa mikono na askari magereza, kufikishwa mahakamani au kuuawa na hao Askari magereza?
Maana haiingii akili, kwa mtu mwenye akili timamu, kuamini kuwa hao akina Dada wawili wasio hata na toothpick mkononi, walikuwa na nguvu za kuhatarisha usalama wa gereza zima na kundi la askari wote magereza waliopo Segerea, kiasi kwamba kulikuwa hakuna njia yoyote ya kistaarabu ya kuwadhibiti zaidi ya kuvunjwa mikono, kuwakanyaga matumboni na vifuani.
Taifa letu linapelekwa kwenye primitivity ambayo hata babu zetu hawakuwahi kuwa nayo. Hawa askari magereza walichokifanya, ustaarabu wao unazidiwa hata na fisi. Maana pamoja na kwamba fisi hana akili na ana tamaa ya kuoindukia lakini huwezi kuona fisi akimvunja au kumwua fisi mwenzie. Hawa askari hayawani hawana hata chembe ya ufahamu kuwa wale ni binadamu wenzao.
Tusishabikie matukio ya kijinga. Mambo yale yaliyofanywa na askari magereza yanaweza kuganyika kwenye jamii iliyokosa ustaarabu hata ule tu wa kufikia kiwango cha wanyama pori. Tusikubali usalama wa raia kuwekwa mikononi mwa majambazi.
Hawa askari magereza waliofanya upumb.avu ule wameliaibisha Taifa. Ule ni upumbavu ambao haustahili kufanywa kwa mtu yeyote, hata kwa mfungwa. Kama wametenda upumb.avu ule kwa raia wa kawaida, wafungwa huko magerezani wanafanywa nini?