Mabadiliko Baraza la Mawaziri: Doto Biteko ateuliwa kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati. Makamba Mambo ya Nje, Pindi Chana Katiba na Sheria

Exactly, Samia bonge la kiongozi
 
Kuna mda nakaa najiuliza ni Kwa Nini TEUZI hizi! Kama mtu kashindwa au kufanya kazi chini ya kiwango Kwa Nini TEUZI nyingine?

Waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi Ndugu Angelina Mabula alifanya kazi nzuri sana!!! Kwanini katolewa?

Kwanini Mchengerwa Kila mara?

Huyu si ndiye kaoa Kule?

Mimi namhitaji Ndugu Angelina Mabula kwenye ardhi maana ni mtendaji Kwa vitendo.

Nampongeza Rais Kwa kumtoa Ndugu January Makamba kwenye Nishati maana hayawahi Fanya project yoyote ikawa 100% efficiency.

Nakumbuka kama mtadi wa Solar ambao aliutangaza
 
Kwahio Makamba baada ya kuharibu huku.., Na ile miradi lukuki iliyoanzishwa ipo mbioni kuanzishwa imepewa pesa za kuanzishwa inakuwaje au ni kupita kuharibu na lawama azikute mwingine...
 
Gabon tayari leo wanajeshi wamefuta uchaguzi wa kitapeli na kuchukuwa nchi.

Hizi utawala za kijanjajanja Dawa yao ni Jeshi tu, sema kwetu tatizo la Jeshi wanakula nao pamoja kwahiyo hilo haliwezi kutokea.
 
Angellah beautiful lady kalamba mali asili na utalii. Mungu amtangulie amlinde na ampe weledi na afya njema. Wish i was Mbelwa the luckiest man on planet earth.
 
Anàfuata nyayo za mzanzibar mwenzake mwinyi àlimteua mrema rip kuwa NWM.
Lakini hapo kulikuwa na hitaji la dharula!! Wizara nyingi zilianza kujishughulisha sana na ufisadi enzi za mzee ruksa!! Mrema kama waziri wa mambo ya ndani akaona ni wajibu wake kuingilia wizara hizo ili kufuatilia tuhuma za ufisadi kwa nguvu zote!! Mawaziri wengine wakawa hawamruhusu kwa madai kuwa anaingilia utendaji wa wizara nyingine!! Mwinyi kuona hivyo akaamua kumpa Mrema rungu litakalomwezesha kuingia kila wizara kihalali kwa nafasi yake! Kwa hiyo akamfanya pia naibu waziri mkuu!! hapo mawaziri wote waliufyata!! Mrema alitisha sana!!! Ukiona Mrema ametembelea mahali tegemea watu watakamatwa!! Ila kwa sasa kuna hitaji lipi la kulazimisha nafasi ambayo haipo kwenye muundo wa serikali?
 
Naibu Waziri Mkuu...mh! Tunarudi enzi za Mwuyi na Mrema.
Biteko ndiye JPM alikua anamuandaa kuja kuwa mrithi wake.
 
Hata mkapa nae alikua waziri wa nje
 
Ni kweli kabisa,inaonekana kuna mtu hatakiwi ila anaonewa aibu kufukuzwa waziwazi,kama na yeye anafikria mbali anatakiwa aondoke kiutu uzima,asisubiri kukimbizwa na mpini kama kibaka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…