Mabadiliko Baraza la Mawaziri: Doto Biteko ateuliwa kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati. Makamba Mambo ya Nje, Pindi Chana Katiba na Sheria

Mabadiliko Baraza la Mawaziri: Doto Biteko ateuliwa kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati. Makamba Mambo ya Nje, Pindi Chana Katiba na Sheria

Acha ujinga. Huyu ndo mkombozi wetu baada ya kuteswa na jiwe miaka mitano bila mishahara kuongezeka Wala ajira mpya zozote. Sasa hivi ajira ni kila pahala hasa sector binafsi ambayo ilikuwa imekufa kabisa kifo Cha Mende.

Sasa hivi utalii inaajiri kwa Kasi mno na waliosoma tourism wanasema mama has rescued them. Sector ya bank inaajiri kwa mamia kwa Sasa baada ya kupulia mashine k a miaka mitano ya jiwe.

Mpaka ameamua kuwarudishia pesa zilizoobwa kwenye akaunti za Hawa wamiliki wa bureau de change. Sasa hatusikii watu kuuawa ovyo ovyo na watu wasiojulikana.
Exactly, Samia bonge la kiongozi
 
Kuna mda nakaa najiuliza ni Kwa Nini TEUZI hizi! Kama mtu kashindwa au kufanya kazi chini ya kiwango Kwa Nini TEUZI nyingine?

Waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi Ndugu Angelina Mabula alifanya kazi nzuri sana!!! Kwanini katolewa?

Kwanini Mchengerwa Kila mara?

Huyu si ndiye kaoa Kule?

Mimi namhitaji Ndugu Angelina Mabula kwenye ardhi maana ni mtendaji Kwa vitendo.

Nampongeza Rais Kwa kumtoa Ndugu January Makamba kwenye Nishati maana hayawahi Fanya project yoyote ikawa 100% efficiency.

Nakumbuka kama mtadi wa Solar ambao aliutangaza
 
Kwahio Makamba baada ya kuharibu huku.., Na ile miradi lukuki iliyoanzishwa ipo mbioni kuanzishwa imepewa pesa za kuanzishwa inakuwaje au ni kupita kuharibu na lawama azikute mwingine...
 
Watanzania hawajaridhika na Mkataba. Hii teua tengua sio Suluhisho.....

"serikali Ina namna mbili tu..
1. Kiheshimu hofu na maoni ya wananchi kwamba hawajaridhika na suala hili, au
2. Kuwapuuza wananchi na kuendeleza na suala hili.

Lakini wapime madhara ya kila uamuzi watakaoifanya"

Mapinduzi yapo mlangoni mwako.
Gabon tayari leo wanajeshi wamefuta uchaguzi wa kitapeli na kuchukuwa nchi.

Hizi utawala za kijanjajanja Dawa yao ni Jeshi tu, sema kwetu tatizo la Jeshi wanakula nao pamoja kwahiyo hilo haliwezi kutokea.
 
Angellah beautiful lady kalamba mali asili na utalii. Mungu amtangulie amlinde na ampe weledi na afya njema. Wish i was Mbelwa the luckiest man on planet earth.
 
Anàfuata nyayo za mzanzibar mwenzake mwinyi àlimteua mrema rip kuwa NWM.
Lakini hapo kulikuwa na hitaji la dharula!! Wizara nyingi zilianza kujishughulisha sana na ufisadi enzi za mzee ruksa!! Mrema kama waziri wa mambo ya ndani akaona ni wajibu wake kuingilia wizara hizo ili kufuatilia tuhuma za ufisadi kwa nguvu zote!! Mawaziri wengine wakawa hawamruhusu kwa madai kuwa anaingilia utendaji wa wizara nyingine!! Mwinyi kuona hivyo akaamua kumpa Mrema rungu litakalomwezesha kuingia kila wizara kihalali kwa nafasi yake! Kwa hiyo akamfanya pia naibu waziri mkuu!! hapo mawaziri wote waliufyata!! Mrema alitisha sana!!! Ukiona Mrema ametembelea mahali tegemea watu watakamatwa!! Ila kwa sasa kuna hitaji lipi la kulazimisha nafasi ambayo haipo kwenye muundo wa serikali?
 
Naibu Waziri Mkuu...mh! Tunarudi enzi za Mwuyi na Mrema.
Biteko ndiye JPM alikua anamuandaa kuja kuwa mrithi wake.
 
Rais mstaafu wa awamu ya nne alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje. Akawa mwanadiplomasia mahiri sana. Pia kuwepo kwake kwenye wizara hiyo kulimuepusha na vurugu za siasa za ndani. Akaja kuwa Rais baadae.

Bernard Membe almanusura angekuwa Rais mara baada ya kuhudumu kwa muda mrefu Wizara ya Mambo ya Nje. Akakshindwa na John Magufuli mwaka 2015.

Na sasa January Makamba amepelekwa Wizara ya Mambo ya Nje. Je ndio maandalizi ya kumpika kama Rais ajaye?
Hata mkapa nae alikua waziri wa nje
 
Nakumbuka hata Kibaki aliwahi kutengeneza hicho cheo cha naibu PM na kumpa Uhuru Kenyatta, enzi hizo walipounda serikali ya mseto baada ya kutokea mgogoro wa uchaguzi na Odinga akawa PM. Utaona kwamba kuunda hiyo nafasi kunalenga kumkwepa PM na kumtumia naibu PM...........kwa maneno mengine Maja atabaki kuwa PM jina.​
Ni kweli kabisa,inaonekana kuna mtu hatakiwi ila anaonewa aibu kufukuzwa waziwazi,kama na yeye anafikria mbali anatakiwa aondoke kiutu uzima,asisubiri kukimbizwa na mpini kama kibaka.
 
Back
Top Bottom