Mabadiliko Baraza la Mawaziri: Doto Biteko ateuliwa kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati. Makamba Mambo ya Nje, Pindi Chana Katiba na Sheria

Mabadiliko Baraza la Mawaziri: Doto Biteko ateuliwa kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati. Makamba Mambo ya Nje, Pindi Chana Katiba na Sheria

Ukisikia "kutapatapa" hakuwezi kuzidi huku tunakokushuhudia sasa.

Huu uwadhifa wa cheo cha uwaziri, imekuwa ni sifa tu ya kushikiliwa na mtu yeyote hata bila ya kuwa na uwezo wa kufanya kazi ya nafasi hiyo.
 
Ila watu wajanja sana alianza Mkumbo Kitila kuwa msemaji wa Bandari baada ya muda akaula, akaja Jerry Silaa nae akamuiga Mkumbo hivi sasa nae kaula, kumbe hizi ndio mbinu mbadala ya kupata uwaziri, nyuma nilidhani ni uchapakazi kumbe ni kuwa mwimbaji mapambio mkuu.
Ukiwa mchapakazi Tanzania unatishia vyeo vya watu, wanakuundia zengwe unakwisha.
 
Naibu waziri Mkuu wa kwanza Tanzania alikuwa ni Salim A. Salim ambaye alihudumu kwa miaka minne akiwa na Joseph warioba kama waziri Mkuu wake katika awamu ya kwanza ya utawala wa Mzee Mwinyi kwahiyo Mrema hakuwa wakwanza.
Asante kwa masahihisho, ila PM ujumbe atakuwa ameupata kwamba he is no longer needed.

Mzigo mwingine kwa Jamhuri kuweza kumtumza.

Ndiyo maana wage bill ya Serikali imefikia bilioni 695 kutoka bilioni 550 miaka 4 iliyopita 🙌
 
Mwenye kujua mkwe kapelekwa wapi maana hadi tunaingia mitamboni nadhani alikuwa maliasili na utalii
 
KATIBA YA JAMHURI WA MUUNGANO WA TANZANIA IBARA YA 55

55.-(1) Mawaziri wote ambao ni wajumbe wa Baraza la Mawaziri kwa mujibu wa ibara ya 54 watateuliwa na Rais (SAMIA) baada ya kushauriana na Waziri Mkuu (MAJALIWA)
Angalau wewe umeandika katika hali ya mtu anayejielewa. Haujanasa kwenye mipasho.
 
Tangu lini mwenye mkono wa Sweta a.k.a G.OV.I akawa na akili? Kupaa na ungo Kila siku akili itatoka wapi? Ungenambia Kula ugali mkubwa sawa
Mimi siyo msukuma, ila kwa majibu yako haya naona wewe ndo huna akili.
 
Rais Samia Suluhu amefanya mabadiliko na teuzi za sura mpya kwenye baraza la mawaziri. Uapisho utafanyika September 1, Ikulu ndogo Zanzibar saa tano kamili asubuhi.
1. Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Doto Biteko kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati. Awali alikuwa Waziri wa Madini.

2. Amemteua January Makamba kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Awali alikuwa Waziri wa Nishati.

3. Amemhamisha Balozi Pindi Chana kuwa Waziri wa Katiba na Sheria. Awali alikuwa Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo.

4. Amemhamisha Steven Byabato kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Awali, Byabato alikuwa Naibu Waziri wa Nishati.

5. Amemteua Jerry Silaa kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Silaa ni Mbunge wa Ukonga, Dar es Salaam.

6. Rais amemteua Anthony Mavunde kuwa waziri wa madini, mwanzo alikuwa naibu waziri wa kilimo.

7. Prof Makame Mbarawa aliyekuwa waziri wa ujenzi na uchukuzi amekuwa waziri wa uchukuzi.

8. Innocent Bashungwa amekuwa waziri wa ujenzi, mwanzo alikuwa waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa.

9. Godfrey Kasekenya aliyekuwa Naibu waziri wa Ujenzi na uchukuzi ameteuliwa kuwa Naibu waziri wa Ujenzi

10. Alexander Mnyeti ameteuliwa kuwa Naibu waziri wa Kilimo

11. David Mwakiposa Kihenzile ameteuliwa kuwa Naibu waziri wa Uchukuzi. Ni mbunge wa Jimbo la Mufindi

12. Judith Kapinga ameteuliwa kuwa Naibu waziri wa nishati, ni mbunge wa viti maalum Ruvuma.

13. Dunstan Kitandula ameteuliwa Naibu Waziri wa maliasili na Utalii, ni mbunge wa Mkinga

14. Stergomena Tax amehamishwa wizara ya mambo ya Nje kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa

15. Angellah Kairuki amehamishwa kutoka TAMISEMI na kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii

16. Dkt. Damas Ndumbaro amehamishwa kutoka Wizara ya Katiba ba Sheria na kuwa Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo.




View: https://www.youtube.com/watch?v=7bLEuvgVGG4

======

View attachment 2733279
View attachment 2733280
View attachment 2733281
View attachment 2733282

Mama anafanya mabadiliko kimkakati; nafasi ya naibu waziri mkuu inaakisi kutokuwa na Imani na waziri mkuu. Kuna namna hesabu zimepigwa na kuona kutakuwa na gharama kubwa kisiasa kulivunja Baraza Zima....
 
Msijilishe pumba, hizo kura hata akizikosa hazizuii yeye kuwa rais!! Mark this Samia ni mpaka 2030!!
Bongo watu mnapenda ubishi kiasi mtu anatunga kitu halafu anabijibishia mwenyewe. Wewe nanga kwani nimekuambia hatapata? Ni hivi: Hata kama CCM wanaiba au kubadilisha washindi lakini hujitahidi sana kufanya kura zao ziwe nyingi kadiri iwezekanavyo. Kadiri zinavyokuwa nyingi ndivyo wizi unavyokuwa mrahisi kufanya na uwezekano wa kutokea fujo kupungua.
 
Naona hujaielewa dhanna ya Reform and Rebuilding.


Hapo kwa Kassim Majaliwa, kilichositisha asipigwe chini ni mfumo tu, lakini ana "underperform" sana, juzi aliambiwa, usingoje maagizo kutoka juu.
Nani ambaye anaperform hata kwa 30% kwenye BM!!??
Hakuna
Hakuna
Hakuna
 
Kwa jicho la tatu ni kuwa majaliwa kasimu kawekwa pembeni kimtindo! Na yawezekana hakubaliani na Dp World. Reference ni ukimya wa Majaliwa kwa sasa
Kwanini anaogopa kujiuzuru?
 
Ila watu wajanja sana alianza Mkumbo Kitila kuwa msemaji wa Bandari baada ya muda akaula, akaja Jerry Silaa nae akamuiga Mkumbo hivi sasa nae kaula, kumbe hizi ndio mbinu mbadala ya kupata uwaziri, nyuma nilidhani ni uchapakazi kumbe ni kuwa mwimbaji mapambio mkuu.
Ukisifia unapongezwa.
 
Katiba yetu haisemi chochote........
-Majukumu ya Naibu waziri mkuu?
-Anareport Kwa nani?
-Mafao yake na Mshahara wake utakuwaje?
Anyway ngoja tuone siku atakayo waapisha
 
Back
Top Bottom