Mabadiliko Baraza la Mawaziri: Doto Biteko ateuliwa kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati. Makamba Mambo ya Nje, Pindi Chana Katiba na Sheria

Mabadiliko Baraza la Mawaziri: Doto Biteko ateuliwa kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati. Makamba Mambo ya Nje, Pindi Chana Katiba na Sheria

Usifananishe China na Tz
Wametuzidi mbali sana
Unajua kusoma na kuandika?


20230731_234928.jpg
 
Majaliwa ajitafakari... aachie ngazi kwa busara na heshima yake iendelee kuwepo kwa wananchi... hii movie inavyoenda anaweza tolewa... kwa cheo cha waziri mkuu, rais akitumia utashi wake kukupa msaidizi ni wazi 'umeshindwa' kazi..
 
Rais Samia Suluhu amefanya mabadiliko na teuzi za sura mpya kwenye baraza la mawaziri. Uapisho utafanyika September 1, Ikulu ndogo Zanzibar saa tano kamili asubuhi...
1. Kuna ulazima gani wa kuwa na naibu waziri mkuu?
Zaidi ya miaka 20 hiki cheo hakipo kinaletwa tena, kwa miaka yote hii ambayo hakikuwepo kuna madhara yaliyojitokeza?

Wizara ya nishati ni wizara pasua kichwa je waziri wake kuwa na ofisi zaidi ya moja ataweza kusimamia kote kwa umakini?

2. Tanzania inaonekana ina fedha za kuchezea viongozi, majuzi kati kuna wizara mpya iliazishwa akawekwa Mkumbo je wanaongeza ufanisi, utendaji, ubunifu au wanaongeza mzigo wa bajeti ya nchi na kuwaelemea raia kwa kodi?

3. Je Mh Dotto Biteko yupo kwenye timing au ameaminiwa au kuna kundi linapunguzwa makali?

Dotto atakuwa na performance zuri kiasi kwamba kero ya umeme inyosumbua tangu JM awe nayo wizara au atakuwa kawekwa mtu kati?
 
Hiki cheo mara ya mwisho alikishika Mrema kama sikosei enzi za Mwinyi.

Kiuhalisia ni cheo cha utashi wa raisi, hakipo kikatiba.

Ila kinachotafakarisha hapa ni pale Biteko atakapokosea kama Naibu Waziri wa Nishati, je waziri akimuadhibu si itakuwa anamuadhibu Boss wake ambae ni Naibu Waziri Mkuu? Maelekezo ya Waziri wa Nishati yatakuwa na mashiko kwa Naibu wake ambae kiuhalisia ni Boss wake?
Kwenye nishati ni waziri kamaili.
 
Rais mstaafu wa awamu ya nne alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje. Akawa mwanadiplomasia mahiri sana. Pia kuwepo kwake kwenye wizara hiyo kulimuepusha na vurugu za siasa za ndani. Akaja kuwa Rais baadae...
Wacha apate uzoefu...tutamuangalia mbeleni...
 
Katika biblia takatifu kuna hadithi moja ya Washami. Hawa nchi yao ilikuwa imetekwa na chakula chote kilifungiwa kwenye lango la mji wao wakawa nje ya lango hawana chakula. Na ilikuwa ukisogea kwenye lile lango chakula kinauzwa bei mbaya na askari walikuua kama ulitaka kufanya ujanja ujanja. Hawa Washami Mungu alikuwa upande wao na walikuwa wamemlilia Mungu kwa muda mrefu.

Njaa ilipowazidi Washami wakajiambia moyoni mwao kuwa TUKIBAKI HAPA TUTAKUFA NA NJAA NA TUKIENDA KULE KWENYE LANGO ASKARI WATATUUA LAKINI PIA BWANA ANAWEZA KUTUFANYIA MUUJIZA. Wakaamua kwenda kule kwenye lango na Mungu akaleta kishindo cha farasi wengi wale askari kule kwenye lango lenye chakula wakakimbia wakijua kuwa kuna jeshi kubwa linakuja kuwapiga.

Kwako Kassim Majaliwa hadithi hii ikusaidie japo sio ya kitabu cha dini yako. Kwa ulipofikishwa leo ni kuwa unapaswa kumalizwa kisiasa kabisa. UKINYAMAZA WATAKUMALIZA NA UKIZUNGUMZA WATAKUMALIZA ila ukizungumza unaweza kupata kishindo cha jeshi la wananchi kikakusaidia. Uchaguzi ni wako.

Mimi nakushauri PAMBANA utakuwa umeisaidia nchi yako kidemokrasia. Otherwise utabaki kuwa Waziri Mkuu wa kusaini na kutia mihuri na mpaka Dec. Bunge lijalo atateuliwa Waziri Mkuu mwingine na utakuwa umejeruhiwa sana kisiasa au kuuawa kisiasa kabisa.
 
Back
Top Bottom