Tetesi: Mabadiliko Baraza la Mawaziri; J. Makamba, Mhagama, Ummy Mwalimu nje; Adadi Rajabu, Bashe watajwa

Tetesi: Mabadiliko Baraza la Mawaziri; J. Makamba, Mhagama, Ummy Mwalimu nje; Adadi Rajabu, Bashe watajwa

Mpaka sasa najiuliza kama kweli JPM anataka hapa kaz si achukue sample na upinzani kama alivyofanya Dk.sheni au vip jaman?maana upinzan Kuna watendaji wazuri tunataka kuinua tz yetu sote pamoja...wapi kabwe,lisu,nasary,na wengine wengi tu
 
Mm napendekeza Mambo ya ndani Dr. JMP ampe KANGI LUGOLA, ni mzr ila kwa sababu huwa anapambana na rushwa, mafisadi huwa wanajitahidi mchafua. Tuachane na mambo ya Kambi (Team EL), tuangalie uwezo wa mtu.

Bashe ni mzr kwa hoja na ushauri, hana kashifa za kijinga. Yuko Serikalini na Upinzani (Ana uma kote kwa kusema ukweli). Japo ni team EL, tuachane na mambo ya team tujenge nchi kwa pamoja.

Huwa nasema kuna watu Hawamuelewi Rais JMP na dhana yake ya kutumbua, ila muda unavyoenda either Hutaki kumuelewa au unataka, utamuelewa hata kwa lazima!!

Fumua hii nchi iunde upya! Kila la kheri Rais.

Bora apewe hata halima bulembo kuliko huyo kangi lugola
 
Kwani alipowateua hakujua kua walikua na uwezo mdogo?

The offece of the president of united republic is too big.
Yes its too big than his ego which is reasonable......I personally understand him
Kwakua ni raisi unataka akikosea amezee tu ili msimuone kachemka, yeye pia ni binadamu kukosea kupo, vizuri akitambua kosa kuinuka na kurekebisha
 
Ni mzr mkuu , ila kwa sababu huwa anawashughulikia mafisadi, juzi alipowekwa kwenye kamati sijui ya PAC mafisadi wanajitahidi kumchafua ili wote wafanane.
Kwamba ile kusimamishwa kisutu ni plot? Ok maana hata mimi nilikuwa nina mkubali sana dosari ikaja hapo tu,tusubiri tuone ni mapema bado kumkubali kama vile.
 
Muda wowote mabadiliko makubwa yanategemea kutokea katika baraza la mawaziri. ambapo mawaziri kadhaa watatemwa kutokana na sababu kadhaa...

1. Jenister Muhagama..... Anatuhumiwa kwa kuzunguka mamlaka za teuzi (Rais na Waziri Mkuu) katika sakata la kumteuwa kaimu mkurugenzi wa NSSF... Mhagama alitenda kosa hilo akishirikiana na Balozi Ombeni Sefue ambaye kwa sasa kashatumbuliwa....

2. January Makamba...... Maranyingi amesikika na kurekodiwa akimsema vibaya Rais, akimsengenya Rais pamoja na kuratibu mipango mbalimbali ya kumdhoofisha Rais Magufuli. haya anayatenda katika Hotel ya Protea Dar es Salaa., na Dodoma ambapo amekuwa akifanya vikao vya siri usiku wa manane na baadhi ya wabunge wa upinzani, pamoja na wafanyabiashara wakubwa wakiwemo wa sukari

3. Ummy Mwalimu...... Inasemekana kasi na uwezo wake mdogo haumrithishi Rais kwa sasa..

Katika mabadiliko hayo Adadi Rajabu, Mbunge wa Muheza inasemekana anaweza kuingia kuchukua nafasi ya Kitwanga.... wengine wanaotajwa ni Bashe, mbunge wa Nzega ambaye anaweza kupewa docket ya Mazingira au Maliasili... na pia Serukamba amekuwa akitajwa.....

mytake: wananchi kwa umoja wetu tumuunge mkono Rais Magufuli.... ana dhamira njema kabisa la kuwatumikia watanzania....
Serukamba mda mwingi hutuma msg Kwa Magufuli kumchongea January Makamba na mawaziri wengine anajulikana Kwa Unafiki lakini habari za chini ya kapeti na Kwa mujibu wa Sangoma mkuu wa January Makamba ni kwamba Adad Rajab atakuwa naibu Waziri lakini Waziri kamili wa mambo ya ndani atapewa January au Mwakyembe Magufuli anataka kuweka watu wenye roho ngumu za kuwadhoofisha upinzani , hataki wanafiki Kama serukamba hao watapewa wizara zenye bajeti ndogo zisizo na heka heka kubwa .
 
Kwa Bashe na Hadadi hapo naunga mkono kabisa, hawa jamaa ni wazuri sana.

Hapo kwa Ummy Mwalimu naona kama huyu mama watakuwa wanamuonea vile aisee.

Mbona yuko safi sana.
 
Back
Top Bottom