Tetesi: Mabadiliko Baraza la Mawaziri; J. Makamba, Mhagama, Ummy Mwalimu nje; Adadi Rajabu, Bashe watajwa

Tetesi: Mabadiliko Baraza la Mawaziri; J. Makamba, Mhagama, Ummy Mwalimu nje; Adadi Rajabu, Bashe watajwa

Kigwangala kamfunika ummy, JM hakustahili kuwepo kabisa kwenye serikali ya magufuli, Makamba na Nape ni watu ambao mara zote huwa nasema hawakustahili nafasi zao walitakiwa wabaki kwenye Chama Chao tu, Bashe sina shaka nae mbunge wangu wa nzega mjini namkubali sana tu,
Tatizo la hawa ccm bado wamekariri kuwa kazi yao ni kutetea Chama na kuteteana wao kwa wao, wanasahau huyu jamaa anaitazama Tanzania kama nchi bila kuangalia vyama,
Ummy is far better than your Kigwangallah.
 
Serukamba mda mwingi hutuma msg Kwa Magufuli kumchongea January Makamba na mawaziri wengine anajulikana Kwa Unafiki lakini habari za chini ya kapeti na Kwa mujibu wa Sangoma mkuu wa January Makamba ni kwamba Adad Rajab atakuwa naibu Waziri lakini Waziri kamili wa mambo ya ndani atapewa January au Mwakyembe Magufuli anataka kuweka watu wenye roho ngumu za kuwadhoofisha upinzani , hataki wanafiki Kama serukamba hao watapewa wizara zenye bajeti ndogo zisizo na heka heka kubwa .

Mkuu naona ujasamehe effect ya team Lowassa baada ya Serukamba kukacha boti
 
Muda wowote mabadiliko makubwa yanategemea kutokea katika baraza la mawaziri ambapo mawaziri kadhaa watatemwa kutokana na sababu kadhaa.

1. Jenister Muhagama - Anatuhumiwa kwa kuzunguka mamlaka za teuzi (Rais na Waziri Mkuu) katika sakata la kumteuwa kaimu mkurugenzi wa NSSF... Mhagama alitenda kosa hilo akishirikiana na Balozi Ombeni Sefue ambaye kwa sasa kashatumbuliwa.

2. January Makamba - Maranyingi amesikika na kurekodiwa akimsema vibaya Rais, akimsengenya Rais pamoja na kuratibu mipango mbalimbali ya kumdhoofisha Rais Magufuli. haya anayatenda katika Hotel ya Protea Dar es Salaa., na Dodoma ambapo amekuwa akifanya vikao vya siri usiku wa manane na baadhi ya wabunge wa upinzani, pamoja na wafanyabiashara wakubwa wakiwemo wa sukari

3. Ummy Mwalimu - Inasemekana kasi na uwezo wake mdogo haumrithishi Rais kwa sasa..

Katika mabadiliko hayo Adadi Rajabu, Mbunge wa Muheza inasemekana anaweza kuingia kuchukua nafasi ya Kitwanga, wengine wanaotajwa ni Bashe, mbunge wa Nzega ambaye anaweza kupewa docket ya Mazingira au Maliasili na pia Serukamba amekuwa akitajwa.

Mytake: wananchi kwa umoja wetu tumuunge mkono Rais Magufuli ana dhamira njema kabisa la kuwatumikia watanzania.

Mkuu, tuhuma nambaa 2 ni serious sana. Ni ya kweli hiyo?
 
Adadi Rajabu is Pathetic. Huyo jamaa nilishangaa sana hata alipoewa uenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama. Ila nikaacha kushangaa baada ya kukumbuka kwamba wanasiasa ni kikundi cha 'wahalifu'.
 
hawezi kubadilisha mawaziri wengi kiasi hicho kwa muda huu mfupi na akifanya hivyo Nchi itamshinda mara 3 ya sasa hivi.Magufuli ana bahati mbaya kweli ajamaliza hata mwaka 1 inaonekana amezidiwa kwa vingi tofauti na watangulizi wake.
Pili atamuweka january katika wizara za hovyo hovyo lakini kumfukuza hawezi kwa kuwa J.Makamba kachangia ushindi wa JPM kwa kiasi kikubwa kuzidi mwana CCM yoyote.
 
Hizi tetesi zaweza kuwa kweli

Wengine tulishasema toka mwanzo kuwa Rais Magufuli alichoanza nacho wala sio KASI bali ni MIZUKA tu ya kuwa Rais. Nchi haiongozwi kwa mizuka na watakaomuangusha wala sio wapinzani bali ni hao hao wenzake ndani ya serikali na chama chake wengi wakijifanya washauri wake!!

Na staili yake ya uongozi hii ya kuamua bila kufikiria....ndiyo anguko lake. Wakati mwingine huyu mtu si hata wa kumuombea bali apaswa atumie akili na busara zake mwenyewe huku akiomba yeye mwenyewe!!

Huyu anafuata nyayo zilezile za Mkwere, hana jipya. Yaani wanambadilisha mwelekeo kabisa, badala ya ku deal na matatizo ya nchi, anaanza ku deal na migogoro ndani ya serikali yake!!
 
Interesting..

Indeed for people to suggest even Serukamba to be considered for a cabinet post; it will be suicidal for JPM!!! Adadi hawezi kuwa effectictive kwenye docket ya mambo ya ndani kwani vita dhidi ya madawa ya kulevya ilimshinda wakati akiwa DCI; Kagasheki ana rekodi ya ujasiri aliyoionesha akiwa Maliasili, anaweza kupambana na hawa wauza madawa!!!
 
Back
Top Bottom