Mabadiliko kutoka Building Better Tomorrow - BBT mpaka kuwa Building Bashe Tomorrow - BBT

Ukiangalia hao vijan ni uvccm na ccm waliota hadi mvi. Watu wameshapiga pesa na hakuna maneno tunafanya hapo.

Serikali kuna namna ya kuwezesha kilimo ila kwa ili alilochagua bashe ni baya sana limejaa wizi na ujanja. Fikiri pia wanamilikishwa vitalu kwa miaka zaidi ya 40.

Serikali ingewekeza kutoa mbegu bure, pembejeo za kilimo tukaamua huu mwaka tunakomboa kilimo cha dengu, wao watafute na soko wauziwe kwa malipo ya cash, wao wauze nje wanakoona inafaa. Iyo ndio namna ya kukuomboa nguvu.

Ccm ata wapewe miaka mingine 50 hawawezi kutuvusha. Tuishi tusubiri kufa tuu.
 
Pamoja na kuwa hizo gharama za BBT zipo juu
Ila kuna vitu muhimu hujaeleza kuhusu huo mradi. Kwanza kikubwa ni kutayarisha shamba na kuweka miundombinu, ya kulifikia na muhimu zaidi kuweka mfumo wa UMWAGILIAJI. Sina hakika kama wanatumia maji ya mto au wamechimba visima ambapo ni ghali sana kununua miundombinu ya Solar kwa ajili ya kuvuta maji au pengine kupeleka umeme huko mashambani.
Mradi kama huu, hauhitaji kubahatisha Mvua kama wakulima wetu wengi wanavyolima lakini pia; gharama hizo ni kama mtaji; inamaana, wakilima tena gharama nyingi hazitakuwepo
Muhimu pia: kwa kuwa na miundo mbinu sahihi, kuna uwezekano wa kulima mara mbilli kwa mwaka na hata mara tatu kutegemea na aina ya mazao

Mwisho; Kuna wale vijana (Wengi) waliopelekwa huko, ujue kuna gharama za kuwatengenezea mazingira ya kukaa huko shambani (Nyumba/Mahema Chakula, Bima ya Afya nk)
Binafsi najua huu mradi unaweza kuwa na changamoto kadhaa kwa sababu bado tunajifunza ila kutoka rohoni kwangu naamini ni moja ya miradi bora kabisa ya majaribio na inayoweza kutusaidia kama Nchi.
Angalizo: Mimi sihusiki huko kwa mradi, napambana kivyangu huku nje/Private
 
Soma mchanganuo umeandikwa hapo na siyo kujifanya mjuaji wakati kichwa kimejaa kamasi!
 
Bashe aondoshwe!
 
Soma mchanganuo umeandikwa hapo na siyo kujifanya mjuaji wakati kichwa kimejaa kamasi!
Kwa mtu mwenye akili akisoma huo mchanganuo uliowekwa hapo anaona kabisa ni wa uongo (Fake!)
Mfano:
1. Hao vijana 800 wanalala wapi (Nyumba & Chakula) kwa gharama zipi
2. Gharama za matibabu ya hao vijana (Bima) zinatoka wapi?
3. Hayo maji ya kunywesha kwa matone yanatoka wapi hadi yafike huko shambani
4. Miundombinu ya kufika huko shambani (barabara) inatengenezwa kwa gharama zipi?
5. Gharama za kununua matractor zinatoka wapi?
Nafikiri tutafute Mchanganuo wa huo mradi badala ya kukaa hapa na kulishwa matango pori.....
 
Hivi ngoja, wizara ya kilimo si ilitengewa Bilioni 210+ hivi za bajeti na ilipitishwa?
 
Nakuunga mkono. Watanzania hii laana ya uzembe hebu tuivue. Tujivike ujasiri wa muda tufumue mfumo wa uongozi watu wahovyo waondoke serikalini.
 
Mdude_Nyagali
Hoja zako ni nzuri lakini Mungu alikunyima;
1..Hekima
2...Busara
Uwashilishaji wako siku zote umejaa dharau na kejeli.
Ni vigumu watu wenye akili kukusikiliza na kuheshimu mchango wako.

Jifunze kwa mwenyekiti wako Mbowe na Mnyika.
Kejeli sio unana harakati bali kukosa hekima...badilika muda bado unao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…