Pamoja na kuwa hizo gharama za BBT zipo juu
Ila kuna vitu muhimu hujaeleza kuhusu huo mradi. Kwanza kikubwa ni kutayarisha shamba na kuweka miundombinu, ya kulifikia na muhimu zaidi kuweka mfumo wa UMWAGILIAJI. Sina hakika kama wanatumia maji ya mto au wamechimba visima ambapo ni ghali sana kununua miundombinu ya Solar kwa ajili ya kuvuta maji au pengine kupeleka umeme huko mashambani.
Mradi kama huu, hauhitaji kubahatisha Mvua kama wakulima wetu wengi wanavyolima lakini pia; gharama hizo ni kama mtaji; inamaana, wakilima tena gharama nyingi hazitakuwepo
Muhimu pia: kwa kuwa na miundo mbinu sahihi, kuna uwezekano wa kulima mara mbilli kwa mwaka na hata mara tatu kutegemea na aina ya mazao
Mwisho; Kuna wale vijana (Wengi) waliopelekwa huko, ujue kuna gharama za kuwatengenezea mazingira ya kukaa huko shambani (Nyumba/Mahema Chakula, Bima ya Afya nk)
Binafsi najua huu mradi unaweza kuwa na changamoto kadhaa kwa sababu bado tunajifunza ila kutoka rohoni kwangu naamini ni moja ya miradi bora kabisa ya majaribio na inayoweza kutusaidia kama Nchi.
Angalizo: Mimi sihusiki huko kwa mradi, napambana kivyangu huku nje/Private