Mabadiliko kutoka Building Better Tomorrow - BBT mpaka kuwa Building Bashe Tomorrow - BBT

Mabadiliko kutoka Building Better Tomorrow - BBT mpaka kuwa Building Bashe Tomorrow - BBT

NAOMBA NIKAE KIMYA MANA NAANDIKA NAFUTA NAANDIKA NAFUTA.

NILITAKA NITOE KOMENTI NZITO HAPA LKN NAKAA KIMYA.


Ila sijui wenzangu hawauumii na hili swala la ufisadi mimi linaniuumiza sana, Ila siku ambayo kutakuwa na tuandamano kidogo na nikabahatika kuwa maeneo ya karibu.

Arooo!!, Nitaitumia nafasi hyo bila kuoga kwa mawe, virungu na mabomu ya petroli.


HALAFU KINACHOUUMA HATA UPINZANI WENYEWE HAWAKO TYR KUSHIKA NCHI NI WALEWALE WALAMBA ASALI
 
Bashe na timu ya bbt ni wapuuzi kupita kiasi tena wasio na huruma kwa vijana Wala nchi
 
Huo ndiyo ukweli wenyewe.yaani unaandaa shamba gharama ya milioni16.5 faida utapata shilingi ngapi.?mfano kikawaida hekta moja ya mpunga unapata gunia 55-60(kwa mbegu nzuri kama TXD360(saro5)ukiwa umezingatia vigezo vyote.Bei ya mauzo ikiwa nzuri kiwango cha juu cha mwisho ni 120000.gunia 60×120000=7.200.000.kwa maana hiyo ni mradi wa hasara kwa serikali
 
Huo ndiyo ukweli wenyewe.yaani unaandaa shamba gharama ya milioni16.5 faida utapata shilingi ngapi.?mfano kikawaida hekta moja ya mpunga unapata gunia 55-60(kwa mbegu nzuri kama TXD360(saro5)ukiwa umezingatia vigezo vyote.Bei ya mauzo ikiwa nzuri kiwango cha juu cha mwisho ni 120000.gunia 60×120000=7.200.000.kwa maana hiyo ni mradi wa hasara kwa serikali
Mpunga unalimia wapi chief
 
Mabadiliko kutoka 𝘽𝙐𝙄𝙇𝘿𝙄𝙉𝙂 𝘽𝙀𝙏𝙏𝙀𝙍 𝙏𝙊𝙈𝙊𝙍𝙍𝙊𝙒 - 𝘽𝘽𝙏 mpaka kuwa 𝘽𝙐𝙄𝙇𝘿𝙄𝙉𝙂 𝘽𝘼𝙎𝙃𝙀 𝙏𝙊𝙈𝙊𝙍𝙍𝙊𝙒- 𝘽𝘽𝙏. TUMEPIGWA BILIONI 13.

Kwa mujibu wa wizara ya Kilimo chini ya waziri @HusseinBashe ni kwamba serikali inatumia milion 16.4 kufadhili shamba la hekta moja kwenye mradi wa Building a Better Tomorrow kwa kifupi BBT. Gharama hizi hazina uhalisia wowote kwa mtu anayejua kilimo au mkulima yoyote. Na kama zingekuwa na uhalisia kwamba mkulima anaweza kutumia milioni 16 kuandaa shamba la hekta moja ambayo ni sawa na ekari mbili basi nchi hii hakuna ambaye angemudu gharama hizo.

Fikiria unalima nini kwenye shamba la hekta moja ambalo maandalizi yake mpaka kupanda mbegu yanagharimu milioni 16? Unalima dhahabu kwenye hilo shamba? Au unalima almasi? Ama tanzanite? Maana haiwezekani shamba lililoandaliwa kwa milion 16 upande mahindi, Mpunga au ulezi halafu utegemee mtaji wako milioni 16 kurudi achilia mbali kupata faida.

Naomba kujitolea mfano mwenyewe maana ni mkulima. Msimu wa kilimo uliopita nimelima ekari 2 na kidogo ambazo sawa na hekta moja na nilivuna tani 3 au gunia 30 za kg 100. Nilikodi shamba kwa laki moja. Vibarua wakanilimia kwa ng'ombe kwa shilingi laki moja. Gharama za mbegu, madawa ya kuuwa wadudu na kukausha nyasi pamoja na mbolea nikatumia laki tano. Kuvuna na kupukuchua pamoja na mifuko ya kuwekea mahindi nimetumia laki tatu. Jumla ya gharama nilizotumia ni milion 1. Nimeuza mahindi hayo December 2022 kwa milion 2 na nusu baada ya kuuza kwa kg Tsh. 800 hukohuko shambani. Hivyo faida ukawa ni milioni 1.5.

Sasa tukirudi kwa Bwana Bashe na wizara yake ya kilimo kwa hekta 1 au ekari 2 na kidogo bajeti yao ni kama ifutavyo:
  • Kulima shamba Tsh. 4,250,000/
  • Kumwagilia Tsh. 7,500,000/
  • Kupima afya ya udongo Tsh. 2,500,000/
  • Mbolea Tsh. 1,750,000/
  • Viuatilifu Tsh. 375,000/
  • Mbegu Tsh. 112,000/-
JUMLA Tsh. 16, 487, 500/ kwa hekta moja. Sasa hiyo milioni 16 ukizidisha mara hekta 812 za vijana waliochukuliwa tayari awamu ya kwanza na wizara ya kilimo chini ya waziri Bashe unapata bilioni 13.5. Yani dakika ya kwanza kabisa mpira unaanza tunapigwa bilioni 13 na hiyo tu ni awamu ya kwanza maana hatujui mradi huu utahusisha hekta ngapi.

Hapo sijajumlisha gharama za upimaji ardhi na hati miliki ambayo wameweka ni milion 2. Na hapo pia nina mashaka kama hizo ndio bei halisi za kupimia ardhi kwa hekta. Anyway tuachane na mambo ya hati miliki turudi kwenye topic yetu.

Mimi ni miongoni mwa watu ambao naunga mkono wakulima kuinuliwa hasa vijana. Mradi wa Building a Better Tomorrow au BBT lengo kuu lilikuwa ni kuinua kilimo kupitia vijana. Lakini kwa mchanganuo unaonekana ni 𝑩𝒖𝒊𝒍𝒅𝒊𝒏𝒈 𝑩𝒂𝒔𝒉𝒆 𝑻𝒐𝒎𝒐𝒓𝒓𝒐𝒘 - 𝑩𝑩𝑻 na kwamba mradi huu umesukwa kimkakati kuwatumia vijana kufanya ufisadi wa mabilioni. Pengine ndio maana vijana walio wengi kama sio wote waliobebwa au kupewa fursa katika mradi huo hawajui chochote kuhusu kilimo na hawajawahi kulima. Ni wakati sasa wa CAG kwenda kufanya ukaguzi katika mradi huo.

Hawa watu ambao Rais Samia aliwapa ruhusa ya kula kulingana na urefu wa kamba zao imefika mahari sasa wanataka kukata mpaka kamba ili waitafune nchi yote ibaki na mashimo. Kuna wingu zito la ufisadi kuanzia wizarani mpaka nje ya wizara ukiachilia mbali fisadi mmoja mkongwe kupewa tenda ya kusambaza mbolea katika mradi huo.

Imekuwa ngumu sana kumtenga bwana Bashe na ufisadi kwa sababu ya watu waliomlea na kumkuza katika siasa ambao kwa kiasi kikubwa wananuka ufisadi wa nchi hii. Bado nina file zake nazipitia kupata uhakika. Miongoni mwa file hizo zinahusisha baadhi ya viwanda kikiweno kiwanda cha Mbolea ya minjingu somewhere.

Kwa mazingira haya tusitegemee kama kutakuwa na uwajibikaji wowote kwa sababu wazazi wa kisiasa wa Bashe ambao wanazo kashfa nzito nchi hii wameshinda vita dhidi ya mafisadi wa Sukuma Gang ambao nao walitesa kwa miaka mitano.

Cha muhimu sasa bila kujali tofauti ya vyama vyetu na dini zetu tuungane kudai #KatibaMpya ili angarau tuokoe chenji na maliasili zilizobakia nchi hii. Tofauti na hapo tutapigwa mnada nchi hii pengine tutakosa mpaka sehemu ya kuishi.

𝑴𝒅𝒖𝒅𝒆 𝑵𝒚𝒂𝒈𝒂𝒍𝒊 𝟕 𝒙 𝟕𝟎 𝑺𝒖𝒎𝒖 𝒚𝒂 𝑵𝒚𝒊𝒈𝒖

View attachment 2617458
Bashe ni wa asili ya kisomali wa Somalia. Amezaliwa katika biashara na atafia humo, sasa, unafikiri yupo hapo kutangaza dini?
Wizara ya Kilimo ngumu sana, aidha, hakuna wizara nzuri kupiga na kutajirika ukiwa ktk ngazi kama ya Bashe kama kilimo.
 
hakuna shamba Wala ndugu yake shamba alilo pewa kijana yeyote Tang mwezi wa 3 zaidi ya kiwapotezea muda na future zao vijana, alaf Leo anawaambia waende kwao wakapumzike bila hata 100 bila kujali vijana wana familia waliko toka na tangu mwezi wa 3 hawajaingiza hata 100 sijui wanaenda kuishi vipi uko makwao
 
Wizara ya kilimo ingetumia hayo mabilioni kuwapa mbolea na madawa wakulima ambao tayari walishaanza kulima wenyewe. Hata kama sio bure kabisa wangeongeza hela zaidi kwenye ruzuku ya mbolea. Au wangewawezesha mitaji wakulima ambao tayari wako shambani na sio serikali kuingia field na kufanya yenyewe. Pia ingetumia pesa kiasi kufanya utafiti wa masoko na kuwatafutia wakulima masoko.

Kilichofanywa na Bashe na kinachoendelea kufanywa hakina faida yoyote kwa nchi zaidi ya kujijenga kisiasa. Hiyo BBT haina tofauti na zile kampeni feki za utunzaji mazingira kuvaa Tshirts zenye maneno ya kiharakati na kwenda kufagia lami au kusafisha beach huko Msasani. Mimi nilisafisha shamba lilikuwa pori kama eka 6 sikutumia zaidi ya milioni. Hiyo milioni 4.75 kwa hekta moja ni upigaji.

Mawaziri wajitazame kama wanafaa. Vinginevyo Rais anaweza akawapiga chini na kuwateua hata wapinzani wazalendo kama Yericko Nyerere au Fahmi Dovutwa.
 
Bashe anachukua mawazo ya nadharia ya kina Carol Ndossi na kuyatekeleza kwenye wizara, hatari sana, hichi kilimo cha iPad sijui kitatufikisha wapi?? Tanzania ni kichwa cha mwendawazimu kila kinyozi anaweza kujifunzia kunyoa

[emoji23][emoji23]
 
Bashe anachukua mawazo ya nadharia ya kina Carol Ndossi na kuyatekeleza kwenye wizara, hatari sana, hichi kilimo cha iPad sijui kitatufikisha wapi?? Tanzania ni kichwa cha mwendawazimu kila kinyozi anaweza kujifunzia kunyoa

[emoji23][emoji23]
 
wizara ya kitapeli tu hiyo isha haribu ndo za vijana zaidi ya 700 kwa kuwateka tangu 17/03/2023 hadi leo hamna hata kijana Alie pewa hata heka 1
 
Back
Top Bottom