SAGAI GALGANO
JF-Expert Member
- Nov 13, 2009
- 47,706
- 69,281
Huo ndiyo mchanganuo wa Bashe,na ndiyo hoja iliyopo mezaniKwa mtu mwenye akili akisoma huo mchanganuo uliowekwa hapo anaona kabisa ni wa uongo (Fake!)
Mfano:
1. Hao vijana 800 wanalala wapi (Nyumba & Chakula) kwa gharama zipi
2. Gharama za matibabu ya hao vijana (Bima) zinatoka wapi?
3. Hayo maji ya kunywesha kwa matone yanatoka wapi hadi yafike huko shambani
4. Miundombinu ya kufika huko shambani (barabara) inatengenezwa kwa gharama zipi?
5. Gharama za kununua matractor zinatoka wapi?
Nafikiri tutafute Mchanganuo wa huo mradi badala ya kukaa hapa na kulishwa matango pori.....
Mwongozo ni kila mtu ale kwa urefu wa kamba yakeBashe kaona Mwigulu anapiga hela kule, kaamua kula kivyake
Yule Mwajemi ni genius sana kuchonga line ya kula hela ya serikali hii.Wozara ya kilimo nayo sasa ina pesa nyingi sana ndio maana lazima iingie kwenye upigaji!!mbona miaka ya nyuma hukuwahi kusikia!!sasa kuna mipesa mingi imemwagwa huko watu lazima watafute njia za kuzipiga!!
Sahihi mno Mkuu!Cha muhimu sasa bila kujali tofauti ya vyama vyetu na dini zetu tuungane kudai #KatibaMpya ili angarau tuokoe chenji na maliasili zilizobakia nchi hii. Tofauti na hapo tutapigwa mnada nchi hii pengine tutakosa mpaka sehemu ya kuishi.[emoji848][emoji2827][emoji1545][emoji817][emoji818]
Ndio kuna uwazi kiasi kuliko awamu iliyopita. Na ndio maana tunajadili hapa na kwingineko bila woga.Matatizo yalikuwepo siku zote na awamu zote, labda tu awamu hii watu wanaweza kuzungumza zaidi kuliko awamu iliyopita.
Hata kama atatumia mashine (Tractor 🚜) ila kulima haitazidi shilingi 250,000 kwa Ekari tena hapo imehusisha gharama za awali za kukata miti ili kusafisha hilo shamba.Hii nchi ngumu kweli kwahyo unataka vijana wakalime na ng'ombe???. tunataka tuachane na kilimo Cha 1960 mkuu
Kweli Lisu tumweleweCha muhimu sasa bila kujali tofauti ya vyama vyetu na dini zetu tuungane kudai #KatibaMpya ili angarau tuokoe chenji na maliasili zilizobakia nchi hii. Tofauti na hapo tutapigwa mnada nchi hii pengine tutakosa mpaka sehemu ya kuishi.[emoji848][emoji2827][emoji1545][emoji817][emoji818]
Acha ujinga! Hata kama ungekuwa msitu wa mibuyu huwezi kutumia zaidi ya milioni 4.we kijana legeza ubongo kidogo pale hazikufyekwa nyasi yalikua mapori tena misitu yenye miti mikubwa imetumika technology kibwa hadi likaitwa shamba
Kamanda karibu tena JukwaaniMabadiliko kutoka 𝘽𝙐𝙄𝙇𝘿𝙄𝙉𝙂 𝘽𝙀𝙏𝙏𝙀𝙍 𝙏𝙊𝙈𝙊𝙍𝙍𝙊𝙒 - 𝘽𝘽𝙏 mpaka kuwa 𝘽𝙐𝙄𝙇𝘿𝙄𝙉𝙂 𝘽𝘼𝙎𝙃𝙀 𝙏𝙊𝙈𝙊𝙍𝙍𝙊𝙒- 𝘽𝘽𝙏. TUMEPIGWA BILIONI 13.
Kwa mujibu wa wizara ya Kilimo chini ya waziri @HusseinBashe ni kwamba serikali inatumia milion 16.4 kufadhili shamba la
Kwa mujibu wa maelezo yakoHuo mchaganuo haihusiani na malazi au chakula cha hao watu. Huo ni mchanganuo kwa hekta na yeye bashe kupitia wizara ndio walioutoa. Pia sio kwa Dodoma tu huo ndio mchaganuo wataotumia kufanya kwenye mikoa mingine yote
Lengo ni hekta milioni 1 na wamepanga kutumia trillion 17
Mkulima BASHE ndio keshapiga hesabu zakeKulima shamba kwa mil 4.2 unalimia na NDEGE au unalimaje? mwenye taarifa naomba kujua
Sasa kuna unafuu gani ambao mkulima ameupata?!!hizo pembejeo tu kuzipata kwa wakati bado ni mtihani?!!na fungu kubwa bado liko kwenye matumizi ,kuliko kwenye maendeleo.Kwa mipango hii ya kiza moto usitegemee mkulima atakuja faidika!!Budget ya kilimo ilikua ndogo.
Ndiyo maana wakulima wakawa maskini .
Acheni sasa iwe zamu yao
Labda anafanya green house. Pia okumbuka mradi wa pampja kama huo kuna gharma z pMoja zinapumguaKuna Utapeli mkubwa katika hili. Kama mradi upo sehemu moja kawaida udongo hupimi kila hekari. Unachukua sampuli za kuwakilisha eneo zima la mradi. Sasa milioni mbili ya kupimia afya ya ardhi kila Hekari ni utapeli mkubwa. Kwa nini wafunge system ya matone isiyo na uhalisia. Tuna mito mingi, wangetafuta sehemu wafunge burrow irrigation. Mradi mzuri ila hauna uhalisia na umejaa ufisadi.
Si hela za uchezea bana zipoKulima shamba kwa mil 4.2 unalimia na NDEGE au unalimaje? mwenye taarifa naomba kujua
Jiepushe na unabii wa kushindwaSasa kuna unafuu gani ambao mkulima ameupata?!!hizo pembejeo tu kuzipata kwa wakati bado ni mtihani?!!na fungu kubwa bado liko kwenye matumizi ,kuliko kwenye maendeleo.Kwa mipango hii ya kiza moto usitegemee mkulima atakuja faidika!!
Kula usawa wa kamba yako. HujakatazwaDuuuh,wazee wanajilia tu
Pamoja na kuwa hizo gharama za BBT zipo juu
Ila kuna vitu muhimu hujaeleza kuhusu huo mradi. Kwanza kikubwa ni kutayarisha shamba na kuweka miundombinu, ya kulifikia na muhimu zaidi kuweka mfumo wa UMWAGILIAJI. Sina hakika kama wanatumia maji ya mto au wamechimba visima ambapo ni ghali sana kununua miundombinu ya Solar kwa ajili ya kuvuta maji au pengine kupeleka umeme huko mashambani.
Mradi kama huu, hauhitaji kubahatisha Mvua kama wakulima wetu wengi wanavyolima lakini pia; gharama hizo ni kama mtaji; inamaana, wakilima tena gharama nyingi hazitakuwepo
Muhimu pia: kwa kuwa na miundo mbinu sahihi, kuna uwezekano wa kulima mara mbilli kwa mwaka na hata mara tatu kutegemea na aina ya mazao
Mwisho; Kuna wale vijana (Wengi) waliopelekwa huko, ujue kuna gharama za kuwatengenezea mazingira ya kukaa huko shambani (Nyumba/Mahema Chakula, Bima ya Afya nk)
Binafsi najua huu mradi unaweza kuwa na changamoto kadhaa kwa sababu bado tunajifunza ila kutoka rohoni kwangu naamini ni moja ya miradi bora kabisa ya majaribio na inayoweza kutusaidia kama Nchi.
Angalizo: Mimi sihusiki huko kwa mradi, napambana kivyangu huku nje/Private