Mabadiliko madogo Baraza la Mawaziri yanalenga kumsogeza January mahali patakatifu?

Mabadiliko madogo Baraza la Mawaziri yanalenga kumsogeza January mahali patakatifu?

Hiyo Wizara wanapewa watoto wapendwa tu.

Ila Makamba kama atajifunza uzalendo ni Raisi mzuri hapo baadae.

Aache kujisikia na kujifikiria mwenyewe.

Hivi ni kweli ndio Baba J. huyo? Yaani Babra ndio Mama J. [emoji23][emoji23][emoji23]
A little Jokes
 
Kipara wamempeleka akauze sura na kujibrand huko akapige picha na kina Rish sunak, Adesina wa Afdb, ramaphosa na sababu hata gentleman degree yake kule georgetown university ya ya Internationa relations and politics.

Hapo ndio panmfaa toka mwanzo walichelewa sana kumpa hiyo wizara ataenda kusimamamia vizuri Foreign policy and Economic Diplomacy.
 
Kutoka foreign affairs = mara paap hapo badaye presidah

Ova
 
Dotto nyota yake kali ni mnyenyekevu hana majivuno,wengine kila siku kufunga simu na vioo vya gari,siasa haitaki hivyo,Biteko atafika mbali zaidi.
 
JANUARY MAKAMBA Hafai kabisa uongozi wowote

Hata jina lake halifai kupendekezwa kwa nafasi ya Urais

Ametesa sana Watanzania na kuwapa hasara alipokuwa Waziri wa Nishati

Pia hatutaki Ufisadi
 
Heshima sana wanajamvi,

Nayatazama mabadiliko madogo baraza la mawaziri kama sehemu ya mkakati wa kumwinua January Makamba kuelekea kileleni (IKULU) baada ya Wizara ya Nishati kumshinda. Kuendelea kumbakiza wizara hiyo hiyo ilikuwa ni kumharibia kisiasa.

Najua watu wengi wamekimbilia kushangaa nafasi ya Naibu Waziri Mkuu Mh Dotto Biteko,lakini nyuma ya pazia WAZEE wa Msoga Camp safari hii hawataki kukosea kama ilivyokuwa kipindi kile cha 2015.Mzee Magufuli hakuwa chaguo lao mazingira au kivumbi cha Lowassa kiliwasababishia kufanya maamuzi bila hesabu sahihi.

January Makamba anaandaliwa maandalizi kabambe bila WAZEE wa Kanda pendwa kushtuka.Mchezo unaochezwa ni kuanzisha cheo kisichokuwepo kikatiba cha NAIBU WAZIRI MKUU kwa lengo la kuwazubaisha WAZEE wa Kanda pendwa kwamba kumbe wao ni sehemu ya walamba asali,hawana haja ya kulalamika wametengwa, hawapendwi, si sehemu ya watoto pendwa.

Vurugu za chama kileeeee kule kanda pendwa hakika kuwastua wapanga mikakati umuhimu wa kumwandaa mwanasiasa kutokea huko kwa lengo la kumtumia baadae kutimiza malengo yao hasa ahadi ya kuhakikishiwa nafasi ya Mzee wa Korosho.

January Makamba kapelekwa pale Foreign Affairs kupata uzoefu baada ya kushindwa vibaya sana Nishati.Katuachia mgao wa umeme,kashindwa kupanga na kupangika mfumo mzima wa manunuzi ya mafuta.Kaondoka Nishati hali ikiwa tete.

Mtangulizi wake Kalemani kasambaza umeme wa REA karibu vijiji vyote kaingia January REA hakuna kila kitu shabala bagala.NISHATI ilimshanda Makamba hana ujuzi zaidi ya kubebwa na mfumo wa walamba asali.
2030 bado mbali sana mkuu
 
Wizara ya mambo ya nje sio pahala patakatifu acheni kukariri

Membe alikuwa Rais?

Magufuli alikuwa Mambo ya Nje?
Wapumbavu wengi hawatakuelewa hapa ila tuliobarikiwa Akili Kubwa na Mwenyezi Mungu tumekuelewa mno Mkuu na umemaliza Kila Kitu Heko sana.
 
Wanaomshambulia Makamba humu wengi wao zimewashinda hata familia zao tu, ziko shaghala baghala.

Ninaamini sasa Makamba ni moto wa kuotea mbali, wajingawajinga wanajitahidi kuzusha hili na lile lakini wapi, jamaa anasonga mbele tu........wala hawajibu kitu wajinga na wapumbavu hawa.
 
Mimi sio shabiki wa Makamba, lakini sitaki uongo wala unafiki! Ame overpeform kinyume na kile wengi tulitarajia! Sina deni nae na siwezi kuongoea uongo juu yake hadi niwe na facts. Kila lakheri dogo, tumikia nchi sio watu/godfathers!
 
JANUARY MAKAMBA Hafai kabisa uongozi wowote

Hata jina lake halifai kupendekezwa kwa nafasi ya Urais

Ametesa sana Watanzania na kuwapa hasara alipokuwa Waziri wa Nishati

Pia hatutaki Ufisadi
Huyo ndo Rais wenu ajaye mtake msitake.[emoji23][emoji23]
 
Huyu jamaa ana kaskendo ka kuiba mtihani kidato cha nne, ikamlazimu kurudia tena mwaka mmoja baadaye..... Sio msafi hata kidogo hafai kwa hilo tu
 
Mkuu huenda Januari anabebwa na Mama kwa heshima ya Mzee wa Ubatizo wa moto! Lakini hana ambacho kinamsogeza kwenye hiyo nafasi Takatifu kama unavyotabiri.
 
Back
Top Bottom