Mabadiliko ndani ya CCM badala ya kuleta matumaini yamewavuruga wengi na kesho ya Taifa la Tanzania

Ana maumivu huyo mfuasu wa siasa za kijima.
 
Ben Saanane yupo wapi?
 
na kwa taarifa mpya ni kwamba VYAMA VYA UPINZANI VISHAJIPENYEZA KWENYE IDARA NYETI , chukua hiyo mkuu .

 
Taifa kusambaratika ni suala la muda tuu. Kama muungano una kero na umasikini wa wengi unazidi unafikiri umoja wa taifa utadumu kweli? Hizo ni ndoto tuu.
 
Nini bana? Kwani we pana jua yeye yote iko fisi kwa fisi dudu moja?
 
Matatizo haya yote yalianzia kwa huyo muasisi unayemsema, ana mazuri na mapungufu yake, mapungufu yake ndio yanaendeleza hizi shida..

Watanzania na Tanzania ni moja ya Taifa ambalo watu wake wengi wamechelewa kustaarabika na kuwa wajanja, matokeo yake bado tulio wengi ni primitive na washamba... Kinachosumbua hii nchi ni uprimitive na ushamba..

Bado mtanzania hata asome vipi au atembee vipi atakuwa tu primitive na mshamba matokeo ndio haya tunayoyaona...Mfumo wetu wa elimu na makuzi hautoa mwanya kwa mtu kuepukana na hivyo vitu.... tunahitaji kwanza mabadiriko makubwa kwenye mfumo wa elimu ili bongo za watu zianze kunolewa kuanzia chini huko wakiwa watoto ili wakizeeka wasiwe washamba na maprimitive...
 
Huyu Samia Mwenyekiti wa CCM ni mtoto wa kigogo gani huko nyuma? Sijawahi kusikia habari za Suluhu Hassan. Huyu Daniel Chongolo ni mtoto wa kigogo gani huko nyuma? Tukubali tu kwa mazingira na hali ya Tanzania, ni dhahiri CCM bado ndicho chama kinachopaswa kuendelea kuaminiwa kuongoza Tanzania. Haijawahi kutokea ccm kuwa na uongozi wa pande moja. Kutoka Chato Hadi kizimkazi (Mwenyekiti); kutoka Kagera hadi nyanda za juu Kusini (Katibu) si jambo la kubeza.

Na cha ziada, ccm yenyewe imekuwa na utaratibu wa kuheshimiana kwenye masuala yao hata kama wengine hawapendi. Sioni hatari ya hicho ukisemacho kwasababu yeyote anaweza kuwa yeyote ndani ya chama chao, utamaduni ambao vyama vyengine ni kama haupo.
 
Upo sahihi sana. Nchi ambayo afisa uhamiaji anataka barua ya wazazi inayomruhusu mtoto wake wa miaka 30 kwenda kusoma nje ya nchi ndipo impe pasipoti, ina kazi ya ziada kuachana na adui ushamba. Hii combination ya adui ujinga na ushamba tena kwa kundi la wasomi wetu inaleta athari kubwa sana katika nyanja zote za maendeleo. Unless we tackle this problem, sioni dalili za maendeleo ya kweli kwa miongo mingi ijayo.
 
Ni aibu tupu
 
Kuna mwingine alikuwa Rais akitaka kukusumbua alikuwa anawatuma vijana wake wakuulize Vyeti vya kuzaliwa vya Babu yako na Bibi yako mzaa Mama
 
Kuna mwingine alikuwa Rais akitaka kukusumbua alikuwa anawatuma vijana wake wakuulize Vyeti vya kuzaliwa vya Babu yako na Bibi yako mzaa Mama
Yote ni aina ya ushamba tunaousema. Vyeti vya babu yangu vitamsaidiaje mkulima kupata trekta la kulimia.
 
Majangili yote yamerudi kwa kasi sn
Mkuu usiingie kwenye mtego huu wa ushamba tunaousema. Utashangaa msomi mzima wa kiwango cha PhD anaokota mambo ya vijiweni na kusema eti tumekwisha kwa kuwa Nape, Makamba na Kinana wapo uongozini! Kwanini uishi kwa hisia zisizo na ukweli nazo??
 
Mkuu usiingie kwenye mtego huu wa ushamba tunaousema. Utashangaa msomi mzima wa kiwango cha PhD anaokota mambo ya vijiweni na kusema eti tumekwisha kwa kuwa Nape, Makamba na Kinana wapo uongozini! Kwanini uishi kwa hisia zisizo na ukweli nazo??
Kwani mi ni under 18? acha uzwazwa rushwa imerudi kwa kasi sn na mambo hayaendi, Jambo gani limefanywa na Makamba awamu hii likaeleweka? tabia ya Kinana huijui?
 
Uchambuzi murua kabisa, ila umekosea pale kwenye kusema Jiwe alikuwa na kundi la watu wasomi. Siyo kweli wafuasi wa Jiwe wengi walikuwa wajinga na wasiyo na upeo wowote. Chunguza vizuri wafuasi wake wengi ni masikini na wasiolipa kodi kwa namna yoyote, maana hawana biashara kubwa pia siyo wasomi
 
Kwani mi ni under 18? acha uzwazwa rushwa imerudi kwa kasi sn na mambo hayaendi, Jambo gani limefanywa na Makamba awamu hii likaeleweka? tabia ya Kinana huijui?

hivi ni lini hii nchi Rushwa iliisha?....

Mkuu tunapojadili haya mambo tuweke ushabiki pembeni ili tutatue tatizo..

Rushwa ni kansa iliyopo kwenye ubongo wa watanzania kuanzia mtoaji na mpokeaji... Maisha yetu wengi wetu hayajanyooka kutokana na mifumo na sisi wenyewe hili husababisha wengi kuwa watoaji rushwa wazuri ili mambo yaende, wapokea rushwa nao hutumia mwanya wa kutonyooka kwetu kuchelewesha mambo ili utoe rushwa..

Rushwa haijawahi kwisha Tanzania, inategemea unamishe mishe gani mjini na unaodeal nao akina nani, awamu iliyopita ilikuwa na watu wake wenye uwezo wa kupokea rushwa bila shida na wasifanywe chochote ( hapa nazungumzia rushwa kubwa kubwa) huku chini kila mtu alikuwa na uwezo wa kupokea bila shida.....

Huwezi kuimaliza rushwa bila kuweka mifumo mizuri ya maisha kwa watu wote, tena utamaliza zile ndogo ndogo ila rushwa kubwakubwa never sahau hizi hata USA, CHINA, UK zipo...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…