Mabadiliko sheria tano za soka kutoka FIFA, kuchezwa dakika 60, kadi za njano na mengine

Mabadiliko sheria tano za soka kutoka FIFA, kuchezwa dakika 60, kadi za njano na mengine

Ukiona hivyo ujue binadamu anazidi kudhoofu,

Niliwahi kuandika mada hapa JF nikiuliza hivi kwanini watu siku hizi wamekua wepesi mno?? Nikadhihakiwa.

Majibu ndio kama hivi.

Kadri siku zinavyozidi kwenda ndivyo ubora wa binadamu unavyozidi kupungua.

Angalia mabadiliko mengi yanaashiria kuwa nguvu hakuna tena.
Na mabadiliko ya katiba mpya yanadhihirisha nini ?
 
Ukiona hivyo ujue binadamu anazidi kudhoofu,

Niliwahi kuandika mada hapa JF nikiuliza hivi kwanini watu siku hizi wamekua wepesi mno?? Nikadhihakiwa.

Majibu ndio kama hivi.

Kadri siku zinavyozidi kwenda ndivyo ubora wa binadamu unavyozidi kupungua.

Angalia mabadiliko mengi yanaashiria kuwa nguvu hakuna tena.
Sure kiongozi
Eti mtu hawezi kuangalia mechi dk 90 anachoka 😳😳😳
 
Sheria ya kuzidi (offside) imepitwa na wakati, iondolewe.

Shirikisho la mpira wa miguu ulimwenguni FIFA, lipo katika kufanya majaribio ya mabadiliko ya baadhi ya sheria ambazo huwenda zikaja kuanza kutumika siku za usoni huku lengo kuu ikiwa ni kuuboresha zaidi mchezo huo pendwa.

WhatsApp-Image-2021-07-20-at-1.58.18-PM.jpeg


Majaribio hayo yameanza kufanywa kwenye Mashindano ya Vijana yanayoitwa ‘Future Of Football Cup’ ambapo SC Heerenveen, AZ Alkmaar, PSV Eindhoven na Club Brugge PSV, AZ Alkmaar, RB Leipzig na Club Brugge ni miongoni mwa timu za vijana ambazo zinashiriki kwenye mashindano hayo ya majaribio ya FIFA yanayo husu mabadiliko makubwa ya sheria.

Mabadiliko ya sheria tano (5) mpya katika mchezo huo wa soka yanakuja ambazo zinaweza baadaye kupendekezwa kuwa rasmi katika mashindano yote ya mpira wa mnguu.

Sheria hizo tano (5) mpya ambazo FIFA wanazifanyia majaribio katika mashindano hayo ya Future of Football Cup ni kama zifuatazo.


1. MECHI KUCHEZWA DAKIKA 60, BADALA YA 90
Moja katiya sheria ambazo Shirikisho la Mpira wa Miguu duniani FIFA inazifanyia majaribio ni mpira kuchezwa dakika 60 badala ya 90 kama ilivyozoeleka.

Kwa maana hiyo kipindi cha kwanza kitakuwa na dakika 30, na kipindi cha pili mwamuzi atachezesha hizo hizo 30 na hatimaye kukamilika dakika 60 na sio dakika 90 tena.

Mwamuzi wa mchezo pia atasimamisha saa yake endapo kuna kitu chochote kitatokea uwanjani kama vile mabadiliko ya wachezaji, mpira kutoka nje nk.

2. IDADI YA WACHEZAJI WA ‘SUB’ KUONGEZEKA (substitution)
Kufuatia mlipuko wa ugonjwa wa Corona duniani, idadi ya mabadiliko ya wachezaji imeongezeka kutoka watatu (3) hadi kufikia watano (5). FIFA inafanya majaribio katika mashindano hayo ya The Future of Football kuangalia kama itawezekana timu kufanya mabadiliko ya wachezaji kadri timu husika itakavyoweza.

3. KADI ZA NJANO
Maboresho yanayofanyika ni kuwa mchezaji anapopewa kadi za njano atatoka nje ya uwanja kwa maana ya kwenda benchi kwa muda wa dakika tano (5) kisha ataruhusiwa kurejea tena uwanjani.

Kwa mantiki hiyo kadi za njano zitakuwa na adhabu zaidi kuliko ilivyozoeleka kwa sasa.

4. MIPIRA YA KURUSHA
Inatarajiwa pia kuondoa sheria ya mipira ya kurusha, endapo mpira ukitoka nje utaanzwa kwa kuweka chini kisha kupigwa kwa miguu na sio kurushwa kama ilivyozoeleka hivi sasa.

5. CHENGA KWENYE KONA (Dribbling)
Mipira ya kona mchezaji ataruhusiwa kuanzisha mpira mwenyewe pasipo kupata msaada kutoka kwa mchezaji wa timu yako. Mchezaji anayepiga kona anaweza kupiga chenga mwenyewe bila kumuanzishia mchezaji mwenzake.

Mwanzoni mwa mwaka huu Florentino Perez alikuja na wazo la kupunguzwa kwa muda kwenye mchezo wa soka wakati walipokuwa wakiitengeneza michuano ya European Super League ambayo ilikuja kupigwa marufuku.

Alipozungumza na El Chiringuito, Perez alisema “Mpira lazima ubadilike, lazima tuchambue kwa nini vijana wenye umri kati ya 16 hadi 24 asilimia 40 miongoni mwao hawavutiwi na soka. Wanasema mechi huwa ndefu mno, na hivyo wanaingia kwenye ‘platforms’ nyingine za burudani. Ni lazima tubadilike kama tunahitaji mchezo wa soka uwendelee kuishi.”

Naye Bosi wa kitengo cha maendeleo ya soka ndani ya FIFA, Arsene Wenger aliwahi kusema siku zijazo sheria nyingi za soka zitabadika.
 
Dakika 60 zinatosha kabisa, watu wakachape kazi mpaka tusimamishe uchumi kwanza.
Na hao wanaofanya kazi kupitia mpira wabaki masikini.?

Kuna mitandao ya kuangalia mechi online, muda ukipunguzwa na wao wanakosa pesa.
Kwenye ku-bet hasara/faida itaongezeka.
Nasikia kuna wachezaji (wanalipwa kulingana na muda wanaocheza) kwahy hapo watapata loss.
Uhondo utapungua
 
Yaani hizo dakika 60 ni stopping time ambayo ndombaya zaidi bora hata dk 90...hyo mnachoka kama mbwa...mpira ukitoka muda unasimama...goalkeeper asipopiga mpira muda unasimama...mpira ukitoka muda unasimama...mchezaji akiumia muda unasimama...so inakuwa kama nba...dk 48 zinachezwa kwa masaa hata matatu
 
Dhaaaaaaa hili la 60mnts lipuuzwee kabsa kwakweli ndo nn sasa hiv
Huu ni ujinga kabisa badala waongeza hata dakika ziwe mia halafu sub ziwe kumi ili kuwapa wacheji walioko benchi fursa ya kucheza wao wanataka kupunguza, hivi hii FIFA ya sasa hivi wanaujua mpira kweli?
 
Ikitolewa kagere atafunga goli 50 peke yake
Akifunga itakuwa ni uzembe wa timu pinzani. Kama idadi ya wachezaji ipo sawa na mipaka ya uwanja inafahamika ,kuzidi kunatoka wapi wakati wachezaji wote wapo humo humo uwanjani?
 
Hawa FIFA wanaelekea kuchanganyikiwa sasa, mpira gani wa dakika 60 wakati nimelipa kiingilio changu? wakileta hiyo sheria mechi zote ziwe bure pasiwepo na kiingilio.
 
Na hao wanaofanya kazi kupitia mpira wabaki masikini.?

Kuna mitandao ya kuangalia mechi online, muda ukipunguzwa na wao wanakosa pesa.
Kwenye ku-bet hasara/faida itaongezeka.
Nasikia kuna wachezaji (wanalipwa kulingana na muda wanaocheza) kwahy hapo watapata loss.
Uhondo utapungua
"Imeshasainiwa na rais wa Fifa kama mnaona kwenye netball kuna unafuu hamieni huko" In Mwigulu Voice
 
Back
Top Bottom