Mabadiliko ya kweli yana gharama kubwa, yanahitaji mtu jasiri na mzalendo kweli kweli

Mabadiliko ya kweli yana gharama kubwa, yanahitaji mtu jasiri na mzalendo kweli kweli

Amani Msumari

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2016
Posts
1,830
Reaction score
972
Piga picha una familia na kipato chako ni kidogo lakini unataka ujenge nyumba yako. Utaiambia familia tunafunga mkanda, kama mlikuwa mnakula nyama mara nne kwa wiki inaweza kushuka kuwa mara mbili au moja kwa wiki. Utabana matumizi ili lengo litimie.

Kumbuka katika kufanya hivyo sio kweli kuwa wanafamilia wote watakuelewa. Unaweza kuta hata mkeo hakuelewi. Hapa busara na msimamo vyote vinahitajika.

Tukumbuke kuwa msingi wa taifa unaanzia kwenye familia. Rais Magufuli amechukua njia hii. Wapo watanzania wasiomuelewa. Wanataka kila kitu kiende vilevile, mishahara minono, barabara nzuri, huduma za kiafya Bora na orodha inaendelea. Hawa wanasahau kuwa ni lazima kwanza tufunge mkanda ili tufikie huko.

Sifa moja kubwa ya Rais Magufuli ni kuwa muwazi na mkweli. Yeye hajali itakuwaje ila anasimamia falsafa hiyo ya kunyoosha rula, hapindishi. Katika muda huu ambao kama taifa tumegundua tulikosea wapi na kuamua kwa makusudi kujirekebisha, Kuna watu wameibuka kutaka kutukwamisha. Wenyewe ni kupinga kila kitu na sasa wameona haitoshi wanaanza kuhubiri chuki na mafarakano. Hawa tuwakatae.

Rais Magufuli amekuwa na msimamo wa kuhakikisha sheria zinafuatwa na maadili na utamaduni wetu vinalindwa. Haya yakifanyika, maadui na wasaliti wanaibua maneno, oooh! serikali inaogopa. Hebu fikirieni mfano mmoja tuu. Watia nia wengi wa nafasi za ubunge walikuwa watumishi wa umma. Karibu wote walitia nia kupitia CCM. Leo tunaona panga la mshahara. Kama kweli kuna upendeleo hawa si wangeachwa? Kama sio kusimamia sheria na kuwa na msimamo haya yangeachwa uchaguzi upite lakini wapi, sheria ni msumeno.

Rais Magufuli amethubutu na ameweza. Tunamuunga mkono.

#2020 kura yangu kwa John

Amani
 
Amefanya makubwa katika kipindi cha miaka mitano hii
Lissu ni jasri atayeongoza mabadiliko ya kweli nchini,magu hana historia ya kuongoza mchakato wa mabadiliko,uraisi ameupata kwa bahati tu.
 
Kwa akili zako butu lazima utakuwa unakali a vitu vyenye ncha Kama msumari
Maneno yako yanaakisi tabia zako. Mmefanana na mgombea wenu. Cha muhimu ujue n kuwa tumeamua kuwa nchi iende mbele na hatutaruhusu mtu atukwamishe
 
Deni la Taifa kupanda maradufu?huku akidanganya tunatumia fedha zetu kwenye miradi yote..huyu afungwe speed governor la sivyo deni litafika 100 trillion
 
Usijibu mambo yaliyo nje ya uelewa wako, utaliwa nyuma, shauri yako
Hizo ni tabia zenu na zinatetewa huko kwenu. Sisi na vizazi vyetu laana hiyo ituepuke.

Ila nashangaa unavyopaniki na kukosa hoja. Dawa mpaka kiama

😂😂😂😂😂
 
[SUP]Deni la Taifa kupanda maradufu?huku akidanganya tunatumia fedha zetu kwenye miradi yote..huyu afungwe speed governor la sivyo deni litafika 100 trillion[/SUP]
Hakuna nchi ya kiafrika isiyo na madeni
 
Hivi Kama serikali ingeamua kuficha kuhusu madeni yake, we ungejuaje?

Vijana mnafurahisha sana
 
Back
Top Bottom