Acheni habari za kuokoteza na kumpamba mtu kwa mafanikio kidogo sana.
Mafanikio makubwa ya pekee ya Magufuli yapo katika nini?
1) Ukuaji wa sejta ya kilimo umeanguka
2) Ukuaji wa uwekezaji umeanguka
3) Ukuaji wa sekta ya utalii umeanguka
4) Ukuaji wa soko la ajira umeanguka
5) Ukuaji wa mauzo ya nje ya mazao ya kilimo umeanguka
6) Ukuaji wa demokrasia umeanguka
7) Idadi ya km za barabara za lami zilizojengwa awamu hii haujafikia hata 40% ya awamu iliyopita
8) Uwekezaji ulifanyika kwenye sekta ya afya, hospitali zote zilizojengwa awamu hii, katika thamani haufikii hata hospitali moja tu kama ile ya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, iliyojengwa awamu iliyopita. Hapo ukiachilia nyingine kama za Mloganzila na ya Benjamin Mkapa
9) Ndege - mwalimu Nyerere alinunua 13 ndege mpya za kisasa
10) Bwawa la umeme - huko nyuma yalijengwa mabwawa kama Mtera, Kihansi na Kidatu
11) Reli - mwalimu alijenga reli ya kisasa kwa wakati wake ya TAZARA
12) Viwanda - wakati wa mwalimu tulikuwa na viwanda vya kila aina, mpaka vya kuunganisha malori aina ya Scania pale Kibaha, kiwanda cha kuunganisha matrekta ya kiwango cha juu kabisa aina ya Valmet, tulikuwa na kiwanda cha baiskeli aina ya swala, tikuwa na vituo mbalimbali vya utafiti na sayansi, n.k.
Sasa hayo makubwa ya ajabu ambayo Maguguli amefanya ambayo watangulizi wake hawakuwahi kufanya ni yapi?
Wewe unaweza kuwa mjinga lakini usiwafanye watu wote wajinga.
Magufuli amefanya machache amvayo ameweza kufanya. Na kwa kweli amefanya pungufu sana kuliko aliyofanya Mwalimu Nyerere, Mkapa na Kikwete.
Sent using
Jamii Forums mobile app